Zitto: Serikali ya awamu ya Tano yatia fora kutofikia malengo ya Bajeti


Ni aibu kuwa na wananchi wasiojitambua kama wewe. Ni aibu kuwa unaona ni muhimu kuzungumzia mtu kuliko dhana. Nilidhani utasema kuna uongo umesemwa, kumbe wewe ulitaka ukweli uwekwe pembeni na mtu aanze tu na ushauri.

Nikukumbushe hili. Wakati bajeti zikipingwa tena kwa sababu muhimu bungeni - Spika na watu wa upande wake hupiga kelele “kama unapinga bajeti, hatutaleta maendeleo jimbo i kwako”. Ni mara ngapi hotuba za upinzani zimekataliwa kusomwa eti kwa kuwa sina lugha isiyopendwa, zinachochea wananchi dhidi y serikali?? Ni mara ngapi wabunge wametolewa nje kwa sababu wametaka wasikilizwe na kulazimika kuvunja taratibu?? Unasema tu watoe ushauri - wautoe kwa nani na katika njia ipi?? Nawe umeangukia walipoangukia wenzako - kutoa maoni yasiyojibu maswali ya lini, wapi na kwa njia gani!! Zitto afanyeje hayo??

Mkuu, makadirio hayajafikiwa. Pamoja na kuwekwa chini ili yafikiwe. Eti nchi tajiri, eti dona kantri. Really????
 
Yeye ndiye waziri wa kudumu wa wizara ya ujenzi na uchukuzi,hataki kuona chochote cha wizara hizo kikikwaishwa na yeyote awaye yeyote.
 
Ishu ripoti kila mtu ameona check ripoti za CAG kila miaka kwa miaka 5 Sasa ni upigaji tu na Querres hazijibiwi.Tulitegemea kwa awamu ipambanayo na ufisadi isisikike hata harufu ya upigaji au madudu yeyeto,Sasa madudu yanapotokea tena kwa wateule wa karibu tunapata shaka je ule ukali ni wa kwenye camera tu au maana tulitegemea watu wa karibu ndo wawe mfano.Ukuaji wa makusanyo utegemea na ukuaji wa sector binafsi kama ziko hoi zimeuliwa kwa kuukumbatia uchumi wa monopoly hayo makusanyo yatoke wapi Hali private y chali,export chali, kilimo kimekufa.hakuna foreign investment wachina nk wamekimbilia Mozambique,Congo,nk wamekimbia sera mufilisi za kutaka tu kukusanya kikubwa maramoja ili kesho usipate cha kukusanya kwann usichukue kidogo umwache akue ili kesho ukusanye tena.We L7 vipi au uko nje ya nchi huoni yaliyofanyika.Uzuri uchumi ni hesabu sio siasa
 
Yeye ndiye waziri wa kudumu wa wizara ya ujenzi na uchukuzi,hataki kuona chochote cha wizara hizo kikikwaishwa na yeyote awaye yeyote.
Hio wizara ndio Ina madudu lkn hawezi gusa kuna maswaiba wake kule wanamjua fika.Sijawahi ona katumbua huko
 
Na wewe unababaisha kama Zito tu; kama kweli unaamini hesabu basi ni hizi hapa kwa miaka kumi iliyopita. Kuna upungufu gani wa ukusanyaji wa kodi zaidi ya kuwa na malengo makubwa. Makusanyo ya kodi yamekuwa yanaongezeka kila mwaka kwa karibu asilimia hamsini katika miaka mitano iliyopita- Yaani kutoka trilioni 10 hadi trilioni 15 katika miaka minne tu.

MwakaMalengo
(Trilioni TSh)
Makusanyo
(Trilioni TSh)
Upungufu
(Trilioni TSh)
Asilimia
2009-20105.0284.6370.3917.776452
2010-20115.8495.550.2995.111985
2011-20126.4566.703-0.247-3.8259
2012-20138.4328.0520.384.506641
2013-201410.4129.2891.12310.78563
2014-201512.12110.321.80114.85851
2015-201613.36613.383-0.017-0.12719
2016-201715.10514.2710.8345.521351
2017-201817.31515.3861.92911.14063
2018-201918.2915.742.5513.94204
 
Kutofikia malengo ni Jambo la kawaida Sana. Maana hata wewe kwako unataraji kupata magunia 10 na ukipata chini ya hapo sio mbaya.
Kitu kibaya ni kushuka mfululizo kwa mapato na sio malengo mkuu.

2020
 
Hizo ni data ukusanye toka wapi,
 
Hizo ni data ukusanye toka wapi,
Ndiyo maana nilikwambia soma ripoti hizo za CAG zinazopindishwa na Zitto wako. Nitakupa mifano michache tu siyo kwa miaka yote kumi niliyokuonyesha hapo juu ila zimeandikwa kwa kiingereza, sielewi kama utazielewa sawasawa.

Mwaka 2018/2019



Mwaka 2017/2018

Mwaka 2016/2017



Chini kabisa ya jedwali hilo ni hii kwa mwaka 2009/2010


Hiyo miaka ya katikati unaweza kujaza mwenyewe kwa ksuoma ripoti za CAG ambazo nimekuonyesha ziko wapi


.
 
Tofu
Tofautisha data na Hali halisi
 
Tofu

Tofautisha data na Hali halisi
Zito alitoa uchambuzi wa ripoti ya CAG na nimekupa ripoti zote za CAG zinapatikana za miaka 12 iliyopita. Kwa sasa unachotaka kusema kuwa ripoti ya CAG ni ya uwongo. Na kama ni hivyo basi Zito asizitumie. Katika ripoti hizo zipo ripoti tatu za Utuoh, sita za Assad na moja ya Kichere, na zote ziko consistent.

Ndiyo maana nikakushauri uwe unatafuta ukweli mwenywe kuliko kusubiri kulishwa ujinga na wanasiasa uchwara na wewe ukawa unameza tu.
 
Moja ya Sakata la Korosho, fedha za wananchi :

Fedha za Umma lazima ziingie ktk Mfuko Mkuu wa Serikali yaani Consolidated Fund

Hoja :
SIKUBALIANI NA MAJIBU YA MWANASHERIA KUHUSU SERVICE LEVY YA KOROSHO.

Mwanasheria Mkuu (AG) wa Serikali, Dr. Kilangi, gwiji na mbobezi wa sheria ninayemheshimu sana tena sana lakini sikubaliani na majibu yake kuhusu swala la Cashewnuts Export Levy. AG ametoa hoja kuu 3 za kisheria lakini nitafanya uchambuzi wa hoja moja tu ili nisiwachoshe kusoma maana mimi huwa ninaandika kurasa nyingi sana linapofika swala la sheria ninaweza kuchambua hoja zingine mbili iwapo wajumbe wa jamvi hili watataka hivyo. Hoja ya AG ni kama ifutavyo ”Makusanyo yote ya cashewnut export Levy in fedha za umma na serikali ndo ina mamlaka ya kuamua matumizi ya pesa hizo”.

MSIMAMO WANGU.

AG anasema kuwa kwenye kesi ya Registered Trustees of the Cashewnut Industry Development Fund Vs Cashewnut Board of Tanzania , Civil Appeal No. 18 of 2001 Mahakama ya Rufaa iliamua kuwa Makusanyo yote ya cashew nut export Levy (CEL) in fedha za umma na serikali ndo ina mamlaka ya kuamua matumizi ya pesa hizo, na huu ndo msimamo wa kisheria kwa sasa. Ninaukataa msimamo huu wa AG kwa sababu kuu nne.

Kwanza, mwaka 2010 the Finance Act, 2010 ilibadilisha msimamo wa kisheria (legal position) uliokuwepo wakati na baada ya Kesi tajwa kufanyiwa uamuzi na Mahakama ya Rufaa. Section 4 of the Finance Act, 2010 iliifanyia mabadiliko the Cashewnut Industry Act, 2009 na kuongeza Kifungu cha 17 A (2) (a) and (b) ambacho kimeifanya asilimia 65% ya Cashewnuts Export Levy kuwa ni fedha za Cashewnuts Industry Development Fund na kuifanya asilimia 35% kuwa fedha za umma na ndo maana sheria inasema 65% ziwekwe kwenye mfuko binafsi kwa sababu sio pesa za umma na ndio maana sheria inasema 35% ziwekwe kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali ( Consolidated Fund) kwa sababu 35 % ni pesa za umma. Pesa za umma lazima ziwekwe kwenye Mfuko wa Serikali au kwenye mfuko ulionzishwa na sheria ya bunge au na Waziri wa Fedha, hii ni kwa mujibu wa Ibara ya 135 (1) na (2) ya Katiba ya JMT na Vifungu vya 11 na 12 vya the Public Finance Act, 2001, hivyo, ni marufuku kisheria na kikatiba kuwe pesa za umma kwenye mfuko binafsi ambao haujaanzishwa na sheria au katiba au waziri wa fedha. Hivyo basi, kwa sababu sheria imeelekeza 65 % za CEL ziwekwe kwenye Cashewnuts Industry Development Fund ambao sio mfuko wa umma bali ni mfuko binafsi basi 65% za CEL sio mali ya umma bali ni mali ya Cashewnuts Industry Development Fund.

Pili, AG alisema bunge kwamba Mahakama ya Kuu katika kesi ya Registered Trustees of the Cashewnut Industry Development Fund Vs Cashewnut Board of Tanzania, Civil Case No. 204 of 1999 iliamua kuwa ”Makusanyo yote ya cashewnut export Levy in fedha za umma na serikali ndo ina mamlaka ya kuamua matumizi ya pesa hizo”. Ni kwa bahati mbaya sikuweza kupata nakala ya uhumu ya Mahakama kuu, hatahivyo, kama kauli ya AG ni kweli kuhusu uamuzi wa Mahakama Kuu basi uamuzi huo wa kwamba Cashenut Export Levy ni pesa za umma ulitenguliwa na Umauzi wa Mahakama ya Rufaa katika Civil Appeal No. 18 of 2001 ambapo Mahakama ya Rufaa ya Rufaa katika ukrasa wa 18 wa hukumu iliamua kuwa cashewnuts export levy ni pesa za wakulima na sio pesa za serikali kwa sababu levy sio kodi (tax revenue), ninanukuu uamuzi huu wa kama ifuatavyo;

“Whatever the case, the cashewnut export levy money was not revenue from taxation so it was not, and is not government revenue. Ordinarily the money would belong to the cashewnut farmer.”

Mahakama ya Rufaa ina mamlaka kikatiba na kisheria ya kutengua uamuzi wa Mahakama Kuu, rejea Ibara ya 117 (3) ya Katiba ya JMT na Kifungu cha 4 cha the Appellate Jurisdiction Act, 1979. Pia Kunga ya kisheria ya Stare Decisis inaelekeza kuwa iwapo uamuzi wa Mahakama ya Rufaa una nguvu dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu na iwapo kuna mkinzano basi umuzi wa mahakama ya Rufaa ndo utachukuliwa kuwa halali kisheria na hule wa mahakama kuu utakuwa batili kwa kiwango unachokinzana na uamuzi wa Mahakama ya Rufaa. Kunga ya inatambuliwa na Kifungu cha 2 (3) cha Judicature and Application of Laws Act, Cap. 358 na katika kesi ya NBC Limited Vs Kalunga & Company Advocates, Misc. Civil Application No.225 of 2004 Mtukufu Jaji Kiongozi, Manento katika ukrusa wa 5 aliamua kuwa Stare Decisis ni kunga takatifu ya kisheria katika mfumo wa sheria wa Tanzania, hivyo Mahakama zote ikiwemo Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa Hazinabudi kuheshimu kunga hii.

Tatu, for the sake of argument only, hata kama Mahakama ya Rufaa katika kesi ya Registered Trustees of the Cashewnut Industry Development Fund Vs Cashewnut Board of Tanzania, Civil Appeal No. 18 of 2001 ingelikuwa imeamua kuwa export Leavy ni pesa za serikali bado 65 % ya pesa za export levy haziwezi kuwa pesa za serikali hii ni kwa sababu uamuzi huu ulifanywa mwaka 2006 miaka 4 kabla ya the Finance Act, 2010 kutungwa na the Finance Act, 2010 ilipotungwa ilibadilisha msimamo wa kisheria wa awali kama ambavyo ungelikuwa umetafsiriwa na mahakama ya Rufaa kwenye kesi hii kwa kufanya 65 % ya CEL kuwa fedha binafsi za Cashewnut Industry Development Fund. Hivyo basi, uamuzi wa Mahakama ya Rufaa katika kesi ya Registered Trustees of the Cashewnut Industry Development Fund) Vs Cashewnut Board of Tanzania ungelichukuliwa kuwa UNAKINZANA na Kifungu cha 17 A (2) (a) and (b) cha Cashewnut Industry, 2009 kama kilivyofanyiwa mabadiliko na Kifungiu cha 4 cha the Finance Act, 2010. Kwenye kesi ya NBC Vs Jackson Nahimawa Sinzo Bakwila [1978] LRT 38 iliamuliwa kuwa iwapo uamuzi wa mahakama UNAKINZANA na Sheria iliyotungwa na bunge basi uamuzi huo ni batili kisheria na sheria ya bunge ndo itachukuliwa kuwa halali kisheria. Kwa lugha ya Kiingereza tunasema Where case law is at variance with the statute the later prevails over the former and the former perishes to the extent of variance Hivyo basi, uamuzi wa Mahakama ya Rufaa katika kesi ya_Registered Trustees of the Cashewnut Industry Development Fund Vs Cashewnut Board of Tanzania_, ungechukuliwa kuwa batili na kutokuwa na nguvu ya kisheria kwa sababu ya ukinzani wake na Kifungu cha 17 A (2) (a) and (b) cha Cashewnut Industry, 2009.

Nne, Mahakama ya Rufaa kwenye Kesi tajwa hapo juu (Civil Case No 18 of 2001) ili tafsiri Export Levy ya kiwango cha 3 % of F.O.B ambayo uwepo wake ulisababishwa na Section 8 and 29 of the Cashewnut Board of Tanzania Act, 1984 na Rule 21 (1) the Cashewnuts Marketting Regulations, 1996 (G.N. 369 of 1996). Mahakama ya Rufaa hakutafsiri na haijawahi kutafsiri Cashewnuts Export Levy ya kiwango cha 15 % of F.O.B ambayo uwepo wake ulisababishwa na Kifungu cha 17 A (2) (a) and (b) cha Cashewnut Industry, 2009 kama kilivyofanyiwa mabadiliko na Kifungiu cha 4 cha the Finance Act, 2010. Hivyo basi, kesi ya Registered Trustees of the Cashewnut Industry Development Fund Vs Cashewnut Board of Tanzania, Civil Appeal No. 18 of 2001, kwenye swala hili ni irrelevant na haihusiki kabisa.

https://www.JamiiForums.com.com/ind...a-mkuu-swala-la-export-levy-ya-korosho.81448/
 
21 Dec 2016
Serikali yasimamisha shughuli zilizokuwa zikifanywa na mfuko wa uendeshaji wa zao la Korosho nchini.


Serikali imesimamisha shughuli zote zilizokuwa zikifanywa na mfuko wa uendeshaji wa zao la Korosho nchini baada ya kubaini kuwa mfuko huo umekuwa ukijihusisha na matumizi mabaya ya fedha za umma, kuhujumu wakulima wa Korosho wakati wa manunuzi ya pembejeo, kununua viatilia kwa bei kubwa pamoja na kupokea mali ambayo haikidhi viwango na kuisababishia serikali hasara kubwa.

Source : ITV Tanzania

N.B
Maamuzi hayo na serikali kuingia kununua korosho yamezidi kulididimiza soko na sekta ya kilimo ya korosho
 
The glass is either half empty or half full kwa mtazamo wa economist na wanasiasa.

Kwa jicho la Zitto its half empty

Ukweli ni kwamba makusanyo kwa miaka minne ya Magu na minne ya mwisho ya JK; leo makusanyo yameongezeka kwa wastani wa asilimia 71% kila mwaka tofauti na ilivyokuwa miaka minne ya mwisho kwenye awamu iliyopita.

Ndio ujue kuna watu wao kazi yao ni kupinga tu, data kila mtu anaweza zipa tafsiri yake na Zitto ni mzuri kwenye kuzitumia kupotosha watu.

Maneno mingi ukimsikiliza wakati hana solution zaidi ya kulaumu tu.
 

Salute mkuu hizi nondo unazoweka kuna wengi wanaona maluelue tu. Tuna hatari kubwa kuliko Corona maana wengi wamejazwa ujinga. BTW usiwe unapotea sana JF.
 


Bagamoyo utafurahia lolote ZK atakalosema kwa sababu moja kubwa, mlikuwa mnaneemeka na kuifilisi NSSF. Mnatakiwa muwe wakweli, its not about you guys and your families.
 
Hebu tuambie Mkuu JK alikua akikusanya kiasi gani kwa mwezi na alikua akizirumia kwenye nini hasa na JPM anakusanya kiasi gani na zinatumika kwenye nini! Haya makabrasha hayatoagi taswira kamili.

Ndio maana hata kanuni ya GDP naitilia shaka sana kwakua haiko fair kabisa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huna vyanzo vya kukusanya mapato,utafikiaje malengo ya kukusanya mapato mengi ?Vitu vingine hauhitaji uwe na degree ya uchumi kuvifahamu.
Wakati wa JK vyanzo vya mapato vilikua Sigara, Pombe na Nishati kwa mfululizo wa miaka 10 tumeshuhudia hili lilitokea.

JPM ameongeza vyanzo vingi vya mapato ikiwemo;
1. TRANSACTION ZA MITANDAO YA SIMU Kama vile tuma pesa toka mtandao mmoja kwenda mwingine au kwa mtandao huo huo.

2. Kuongeza salio kwenye simu

3. Bank transaction zilikua zikipita juu kwa juu na faida kubwa kuingia bank zaidi na Serikali ikiwa haipati kitu.

4. Share za Serikali katika mashirika yasiyokua ya Serikali na yale ya kiserikali yamekua yakitoa gawio.

5. Tumeshuhudia udhibiti wa mapato mengi yaliyokua yakipotea kwenye sekta ya Madini na Utalii

Labda kweli huhitaji kuwa na degree bali unahitaji kuacha kuwa na chuki ili uweze kuyaona haya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali ya Awamu ya Tano yatia fora kutofikia malengo ya Bajeti


View attachment 1416458
Wewe tuambie juu ya wizi wako na rushwa ulizobeba kwenye kamati za Bunge la mshikaji wako. Uliinua uchumi gani. Haya uliyoandika mbona ndo hayo hayo tangu mwaka juzi? Any news?

Uchumi wa darasani! No! Hujawahi kufanya kazi ya uchumi popote! Kaa kimya! Tunaweza sikiliza habari za mchumi anayejua uchumi, siyo mchumi anayesoma kwenye internet na kukumbuka notes za darasani. Hadithi nyingi bila hata muelekeo. Uchumi wa principles hauko ofisini. Ofisini tunataka ukweli badala ya kusimulia SGR na Ndege.

Nionavyo mimi unastahili kuelewa kwamba kila kitu kinachuja. Wewe umekwisha chuja! hutainuka tena kisiasa. Mihemuko ilikuinua, ukabebwa na ukajisahau ukiamini uko bora. You are no longer colourful!
 
Wewe ndio umejitia aibu na fedheha. Wapi ZZK anashangilia? Wewe na wenzio wengine msio na uzalendo hanpendi kuona wananchi wanapata elimu ya uraia. Wanaioachambua ripoti ya CAG kama Zitto wako wengi. Yeye anaxhambua kilichofanywa na kuonwa na CAG. Haiongei kilicho chake. Umeacha kuchambua alichochambua, unamshambulia mtu. Labda wewe na wenzio CCM mkienda sokoni au dukani mnaonyesha kadi cha CCM na mnapewa discount nono so hamuoni uchumi wa nchi ulivyoyumna
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…