Zitto: Ushauri wangu kuhusu Mlipuko wa Korona

Zitto: Ushauri wangu kuhusu Mlipuko wa Korona

PROPAGANDA VS UHALISIA
"Nchi yetu ina akiba ya US$5.4bn zinaweza kununua bidhaa kwa miezi 6, hatujawahi kuwa na kiasi hicho cha fedha tangu tupate Uhuru" Magufuli

GHAFLA👇

"Ukizuia watalii kuingia nchini kwa mwezi mmoja italeta shida kiuchumi. Tunaomba Mungu ugonjwa (COVID-19) uondoke" Polepole
Weee umekuwa msemaji wa serikali? Weee nyumbani kwako hata ugali huna unakuja hapa kuchonga na kisimu chako cha tecno
 
When kolona come marchin in , tuta tafutana. Ndugu watanzania huo ndio ukweli.
 
PROPAGANDA VS UHALISIA
"Nchi yetu ina akiba ya US$5.4bn zinaweza kununua bidhaa kwa miezi 6, hatujawahi kuwa na kiasi hicho cha fedha tangu tupate Uhuru" Magufuli

GHAFLA👇

"Ukizuia watalii kuingia nchini kwa mwezi mmoja italeta shida kiuchumi. Tunaomba Mungu ugonjwa (COVID-19) uondoke" Polepole
makosa yalifanywa October 2015.
tusirudie makosa October 2020.
 
Ushauri wangu kuhusu Mlipuko wa Korona- Zitto

#COVID19TZA Serikali imethibitisha uwepo wa virusi vya Korona Tanzania. Utulivu ni muhimu kwani kukiwa na maandalizi ya kutosha tunaweza kukabili madhara ya mlipuko huu. Nashauri mambo 3 muhimu sana, kwa maoni yangu.

- Tunaona Nchi nyengine kukiwa na ‘panic’ ya chakula. Watu wetu ni fukara sana, bei za chakula zitapanda na wengi hawatamudu.

Pia Serikali haina Akiba ya kutosha ya chakula kwenye ghala la Taifa. Kuna nafaka ya kutosha Siku 3 tu kwa kila Mtanzania. Ni vema Serikali kufanya uamuzi wa haraka kununua chakula ili kukigawa maeneo itakapohitajika.

- Tanzania inategemea Sekta ya Utalii kwa kiasi kikubwa katika Mapato ya Fedha za kigeni na ajira kwa raia wake. Mlipuko huu unaathiri sana sekta hii ambayo inaingizia Taifa wastani wa Dola za Marekani 2.5 bilioni kwa Mwaka sawa na 25% ya Mapato yote ya Fedha za kigeni yanayoingia nchini.

Naishauri Serikali kukutana na Wafanyabiashara wote kwenye sekta ya Utalii na Vyama vya Wafanyakazi kwenye sekta hiyo kwa lengo la kupata tathmini ya Pamoja ya madhara ya mlipuko huu kwa sekta ya Utalii na huduma zake.

Serikali itazame namna ya kuwafidia ( stimulus package) wafanyabiashara Katika sekta hiyo ili kulinda ajira za Wananchi. Ikiwezekana fidia iwe ni kulinda ajira kwa kufidia gharama za wafanyakazi ( payroll costs).

- Waziri wa Fedha na Uchumi apeleke Bungeni Taarifa ya utafiti wa madhara ya mlipuko wa Korona kwa Uchumi wa Tanzania kwa ujumla na Bunge lijadili Kwa maslahi ya Taifa ili kutoa mapendekezo ya kibajeti kuhami Uchumi wa Nchi yetu na haswa kulinda biashara ndogo, Wafanyakazi kwenye sekta zilizo hatarini kama Utalii, huduma za vyakula, usafirishaji na uchuuzi.

Zitto Kabwe, MP
Kiongozi wa Chama
ACT Wazalendo
17/3/2020
Nilichoambulia hapa: Wafanyakazi kwenye sekta zilizo hatarini...addendum
Utalii: Ni rahisi kujua watalii hawa wanatoka wapi-dhibiti wale wanaotoka kwenye nchi zilizoathirika, zinajulikana.
Kweli wafanyakazi katika sekta hii wapewe kipaumbele, iwe ni elimu kuhusu madhara na kujikinga au kufidia gharama kama wataathirika kiuchumi na kiafya. I second.
Kwasasa, walio mstari wa mbele ni wa huduma za Usafirishaji na uchukuzi, wajue kwamba wao ndio wataweza kuondoa ufinyu wa Chakula na gharama ziambatanazo na usambazaji. Wajizatiti kwa kinga na walewe umuhimu wao katika hali hii....sio mbaya hata JKT wakasaidia.
Hakuna siasa wakati kuna janga kama hili, bali Uzalendo.
Aluta continua.
 
Kwanza nipende kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutupa zawadi ya uhai na kukuwezesha wewe mpaka unasomaa ujumbe huu.

Nimejaribu kutafakari kwa kina madhara ya coronavirus mpaka nimeingiwa na hofu. Mungu atuepushe tusifike kama Italy.

HAYA NI BAADHI YA MADHARA

Watanzania tulio wengi hatuna tabia ya saving. Nikipiga picha shughuli za kiuchumi zikisimama kwa muda wa miezi kadhaa, tutaishi vipi wale ambao mpaka tutoke ndio tupate mkate wa kila siku?

Vyakula vitapanda bei. Je, tutamudu vipi?

Je, tukiugua magonjwa mengine mbali na Corona tutaweza kujigharimia matibabu?

Mpaka muda huu fear & life insecurity imetawala.

Kuna watu wameanza kujitenga na watu tunao fanya shughuli zetu Kariakoo.
Binafsi mimi kuna watu wameanza kuniepuka.

Jana tu face mask zimepanda mara dufu kutoka shilingi elfu 5 mpaka kufika shilingi laki moja kwa kibox kimoja chenye 50 pieces.

Hand sanitizer nazo ndio zinazidi kupanda bei na hazipatikani.

Corona ni zaidi ya tunavyo fikiria.

Unaweza na wewe ukashusha nondo zako kwenye huu uzi nini kifanyike pia madhara gani ili tuweze chukua tahadhari.

MUNGU

#TANZANIA
#AFRICA
#All over the world

Tuepushe na hili balaa.
Na kwa wale wapenda kuvaa mask wasikilize hii
 
Mataifa mengi duniani yamehimiza raia kufanya kazi wakiwa majumbani na viwanda kufungwa na mikusanyiko mbalimbali kuhairishwa vile vile usafiri wa umma kufungwa hadi corona itakapothibitiwa.

Tanzania tumeambiwa tufanye kazi na miradi yote iendelee na viwanda kuendelea na kazi na mikusanyiko mbalimbali kuendelea.
Kwani tukisimamisha shughuli mbali mbali kwa ajili ya corona mapato yataporomoka na uchumi utayumba, serikali itakosa mapato, wafanyakazi hawatalipwa hali itakua mbaya kiuchumi serikali itafilisika. Mwisho wa siku watu watajazana majumbani bila pesa hali itakua mbaya watu wataandamana na hakutakua na wakuwazuia kwani hakuna pesa ya kuwalipa polisi/jeshi mshahara kuzuia maandamano, mwisho wa siku watu wataandamana hadi maeneo nyeti bila kizuizi.

Cha muhimu tuendelee kufanya kazi acha tufe na corona ila tuhakikishe uchumi hauyumbi serikali ikakosa mapato ikashindwa kujiendesha, ikafilisikamwisho watu wakaandamana ikawa balaa, tujitahidi corona isiturudishe nyuma tukashindwa kufika 2025.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mataifa mengi duniani yamehimiza raia kufanya kazi wakiwa majumbani na viwanda kufungwa na mikusanyiko mbalimbali kuhairishwa vile vile usafiri wa umma kufungwa hadi corona itakapothibitiwa.

Tanzania tumeambiwa tufanye kazi na miradi yote iendelee na viwanda kuendelea na kazi na mikusanyiko mbalimbali kuendelea.
Kwani tukisimamisha shughuli mbali mbali kwa ajili ya corona mapato yataporomoka na uchumi utayumba, serikali itakosa mapato, wafanyakazi hawatalipwa hali itakua mbaya kiuchumi serikali itafilisika. Mwisho wa siku watu watajazana majumbani bila pesa hali itakua mbaya watu wataandamana na hakutakua na wakuwazuia kwani hakuna pesa ya kuwalipa polisi/jeshi mshahara kuzuia maandamano, mwisho wa siku watu wataandamana hadi maeneo nyeti bila kizuizi.

Cha muhimi tuendelee kufanya kazi acha tufe na corona ila tuhakikishe uchumi hauyumbi serikali ikakosa mapato ikashindwa kujiendesha, ikafilisikamwisho watu wakaandamana ikawa balaa, tujitahidi corona isiturudishe nyuma tukashindwa kufika 2025.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe ndiyo unaelewa sasa watu ndio chanzo cha vitambi vyenu na bado hamuwaheshimu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaiabisha ngazi ya elimu yake kwa kuwa na mawazo ya kitoto namna hiyo! Wala hana wasi wasi yuko baridi kabisa, hajali, haoni, ni kama alien asiyejua yanayoendelea duniani!

Huyu hatutakii mema hata kidogo ni Rais wa hovyo sana.

Ndio maana hili janga wanaliendesha kisiasa badala ya kuwa na Daktari wa kitengo husika kuwa msemaji wa Corona!

What a pathetic regeme with poor leaders!

Ni bora mkafie tu kwa corona kuliko serikali ifilisike hata uchaguzi bado mkikaa majumbani mwezzi tuu mtaandaman serikali iwape pesa mwisho wake mtaingia magogoni. Hatutaki habali hizo bado tuna miaka mingine mitano magogoni kafieni tu viwandani na corona muombeni mungu shetani ashindwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom