Watanzania hawa wenzetu wanaofanya kazi katika sector ya utalii hasa mahotelini,wengi wako majumbani kwa Sasa hasa huko kaskazini na hawajui Ni lini ugonjwa huu utaisha nao watarudi kazini na kuendelea kupata kipato kitachowawezesha kuendelea kutunza familia zao.kama tutaweza kuwatafuta kwa kupitia njia yoyote tukawapa elimu ya ujasilia Mali na tukawapatia mikopo itakuwa vyema kipindi hiki tunapopita katika changamoto hi.mabosi wengi wa sector hii wamekuwa wakilia mambo magumu hata kabla ya Corona ,wengi walipunguza wafanyakazi au mishahara kwa hili la Corona nategemea ndio kabisa watanzania wenzetu wanawafanya watalii kuendelea kuusifu ukarimu wetu kwa matabasamu na huduma Bora, mda huu natumaini mishahara ya mwezi wa 4 au wa 5 wataisikia kwenye Bomba.Naomba Kama tunaweza wafanyia kitu kundi hili labda kwa kuwapeleka kwenye miradi mbali mbali inayoendelea basi tuwapeleke huko wasahau kwa muda habari za kubeba tray mradi wapate chochote kitu Cha kujisukuma kipindi hiki kigumu kwao.maana kazi hizi nyingi zina mishahara midogo ya chini isiyotosha kusema kuwa wana akiba ya kutosha kuweza kuendesha maisha yao kipindi hiki kigumu.Naiomba serekali iangalie namna ya kusaidia kundi hili la vijana hata kupitia ofisi ya wakuu wa mikoa.