Zitto: Ushauri wangu kuhusu Mlipuko wa Korona

Zitto: Ushauri wangu kuhusu Mlipuko wa Korona

Duh! Zitto umeongea jambo la msingi nimeona tija ya wewe kuwa mchumi! ukweli njaa inakuja.
20200317_230451.jpg
 
Kwa vile shughuli za kuingiza kipato zitakua interrupted, muswada pia ujumuishe kupatia kila familia/kaya cheki ya walau laki mbili za matumizi, au kusitisha tozo za umeme, maji na huduma za afya.
Uchumi wetu hauruhusu hayo.
 
Panic haitatusaidia sana.

Vitu vya muhimu kujua kwa uzoefu wa wenzetu Ulaya na China.

Ugonjwa huu unaambukiza kwa kasi sana ila unakuwa severe zaidi kwa watu walio above 50.

Kesi za vifo 90% ni kwa wazee na watu wasio na afya njema kama wagonjwa wa HIV etc.

Below 50 wengi wanapata nafuu na kupona kama mafua ya kawaida tu.

Mataifa ya wenzetu kama China na Italia yamepata kesi za vifo nyingi sababu ya idadi kubwa ya wazee katika nchi zao.Nchi kama Italia wazee ni wengi kuliko vijana.

Tanzania ni kinyume chake,we have a very young society.Hili linaweza kuleta matokeo tofauti pale ugonjwa huu unapoingia kwa jamii yetu, maambukizi yakawa mengi lakini athari zikawa ndogo.Ila tahadhari ni muhimu lakini tusipanic na kujaribu kufanya sana comparison na wenzetu, tutakosea.Hili tuhangaike nalo kwa kuzingatia mazingira yetu.

Kuwe na effort ya pamoja kwa nchi zetu za maziwa makuu,guided by same policies ili kuhakikisha eneo lote liko salama na ugonjwa unakuwa contained.Ni rahisi mtu akashuka na ndege Kenya na kuingia Arusha, then Dar, lakini kama Kenya na Tanzania zote zikifunga mipaka, inakuwa effective zaidi.

Kuwe na strategic plans kwa maeneo korofi yanayoweza kusumbua kama Dar yafuatiliwe na kuweka strict measures zaidi ili kuepuka maambukizi mengi humo ambamo control itakuwa ngumu sana.Suala la kudhibiti mikusanyiko ni la msingi maeneo haya yenye population kubwa,ila tahadhari ichukuliwe kuhakikisha hatua hizo hazitaathiri utendaji kazi wa shughuli za kiuchumi kupita kiasi.Hapa ni pa kutumia akili sana.

The first two weeks zitumike kuisoma vizuri athari ya ugonjwa kadri zinavyojitokeza.

Baada ya kupata skeleton picture ya uhalisia wa tatizo kwa jamii yetu katika siku za mwanzo, wenye "vichwa vyao" wakae chini na kutumia elimu kukisia athari za kiuchumi kwa muda mfupi na mrefu,na kuandaa mikakati kuhakikisha inakuwa minimized kwa ubunifu wowote unaowezekana ili kuokoa taifa.

Tusisahau hii ni global crisis kijamii na kiuchumi,hivyo tathmini lazima izingatie mazingira na matokeo ya ndani na nje.

Sio ishu rahisi hata kidogo. Ni vema tukawa serious na kuvaa vibwaya haswa.

Tusithubutu kuchukulia advantage za kisiasa kwa suala hili, kila uamuzi wetu ufikiwe na kutekelezwa kisayansi, period.

Sambamba na ugonjwa huu,kuna ugonjwa mbaya zaidi wa "matumizi mabaya ya media".Tujiandae kupambana info war kuhakikisha jamii inalichukulia suala hili katika usahihi na hali ambayo itaifanya jamii yenyewe iwe msaada mkubwa kwetu kuwalead into victory.

Jinsi tutakavyopambana vita ya taarifa ndio italeta positive au negative impact kwa uchumi wa nchi. Hili tulizingatie sana. Ndugu zetu wa eagle house hapa mnapaswa kuonyesha umahiri wenu kwa kiwango kikubwa sana.
 
Kweli Hon. Zitto. Pia, nafikiri hio inaweza kua reference nzuri ya baadaye kama litatokea tena tatizo kama hili, lakini hawa vichwa panzi magoigoi wasiposema uchochezi, hii ngoma ya corona ilikua ni kuikwepa sababu imekuja kama ngumi nzito kwenye masumbwi, daah nchi yangu.
 
Mh Zitto kwa serikali hii iliyoko Hoi kinapato na kifedha na matumizi mabaya ya Fedha unadhani inaweza jambo kama hili.

Labda ungewambia kuna wabunge kumi wa upinzani wanataka pesa za kununuliwa hadi World Bank zingekopwa kwa kuunga juhudi.
 
Umeongea vizuri sana MP, lakini katika swala hapo la kununua na kugawa chakula chakula, ukweli nchi yetu bado haijapata nguvu ya kukidhi jambo hili, pengine pia ningeongeza ushauri kuwa, serikali ingejikita zaidi kuwezesha ndugu zetu walioko kijijini ambao corona wanaisikia kwa majirani pengine hawana taarifa wawezeshwe kupata vifaa vya kinga (mask, elimu n.k) chukulia mf. Hapa moshi mask inauzwa 10k, kijijini pesa hiyo inapatikana wapi!?

Yule babu asiye na ndala, alielima mahindi ndizi, ngogwe na nyanya shamban kwake ili apate kuishi mwenye akiba ya 1k ya chumvi na mbege ataipataje mask!?

Nadhani zaidi serikali ikiangalia juu ya protection zaidi itakua imeokoa sana, (maana yangu vifaa kinga vitolewe bure kwenye zahanati) hapo tunaweza kupata ujasiri wa kuendelea kufanya kazi sisi mafundi ujenzi, bodaboda, mafundi cherehani ambao hata hiyo precautional reason for cash hatuikidhi kwa umaskini wetu.

Ahsante.
 
kerubi afunikaye,
Umefafanua vizuri kuwa vifo vingi vinatokana na kuwa na afya isiyo njema au kwa lugha nyingine afya yenye kinga hafifu(compromised immunity) kwa ulaya unaona wazee ndio wengi hivi umewaza kuwa kusini mwa sahara watu wenye compromised immunity ni wengi sana na wanahusu karibu makundi yote ya umri?

HIV, Malnutrition, low SES haya ni mambi tatakayozidisha vifo vya Corona kusini mwa Sahara.
 
Wangemsikiliza Msigwa, kwasasa bunge lingekuwa lineshajadili na kutoka na maazimio ya pamoja!
Ushauri mzuri!
Ila walisikiliza ushauri wa Bulembo wa kumuua Zitto huku mchungaji Lwakatare akishangilia , matokeo yake Zitto hajafa bali corona imeingia .
 
Back
Top Bottom