Zitto: Ushauri wangu kuhusu Mlipuko wa Korona

Zitto: Ushauri wangu kuhusu Mlipuko wa Korona

Hivi unaweza ukamzuia mbongo ukamwambia akae Ndani kipindi cha wiki 2 asitoke kwenda popote huku ukimsisitiza aweke stock ya nahitaji yake na Chakula?

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi tayari Tanzania imeshaptwa na mlipuko wa virusi vya korona? Nilisoma jana mgonjwa mmoja aliyekuja nao kutoka Ubelgiji kwa kupitia Rwandair akawekwa karanatini, lakini kumbe leo siku moja tu gonjwa limeshalipuka.

Hatari kabisa
 
Zitto,
Nacho ona hapa huu ni mwaka wa uchaguzi, hivyo Maneno mengine ni ni nifike vipi kwenye kila tukio ili Mimi nionekane bora kuliko mwingine, na ndio hawa hawa wanakuja na deni is taifa halivumiliki, chakula kime baki cha siku tatu n.k.

Bila kuelewa uchumi wa Tz bado ni mdogo kuweza kuhimili anacho kisemea zana za kilimo.

Hapo awali alikokuwa mwenyikiti wa PAC aliiachia mashirika ya pensheni yafanye madudu yasiyo elezeka na kuharibu uwezo wa mashirika hayo kuweza kuwalipa wastaafu mafao mazuri na ktk wakati.

Pili maslahi ya wabunge vs maslahi ya wafanyakazi , na kuna wakati nilisikia kasusa per diem, badala ya kuichukua na kuiwekeza kwenye huduma ya jamii au stimulus package angalau kwenye Jimbo lake.
 
ngusillo,
Umeongea point lakini jambo moja kubwa sana ni sustainability kwa nchi yetu kuwa ktk hali hiyo na hata hizo nchi nyingine, ndio maana inaitwa janga la kitaifa/ kimataifa, hivyo tuachane na siasa tuwe wa kweli kwa nafasi zetu.
 
Umefafanya vizuri kuwa vifo vingi vinatokana na kuwa na afya isiyo njema au kwa lugha nyingine afya yenye kinga hafifu( compromised immunity) kwa ulaya unaona wazee ndio wengi hivi umewaza kuwa kusini mwa sahara watu wenye compromised immunity ni wengi sana na wanahusu karibu makundi yote ya umri?

HIV, Malnutrition, low SES haya ni mambi tatakayozidisha vifo vya Corona kusini mwa Sahara.
Wiki mbili za kwanza baada ya maambukizi zitatupa majibu na direction ya kufuata. Kwenye compromised immunity kuna mambo mengi ya kuconsider ili kupata muelekeo wa kiwango cha athari na factors nyingine bado ni subject of research.Kwa mfano suala la extent gani covid 19 anaweza kumuathiri mtu mwenye HIV akawa severe bado liko kwenye research, halijawa proved either way. Pia nchi kama India waliamua kuruhusu hiv antiviral drugs kutumika kusupress covid 19 kwa waathirika wa hiv waliopatwa na corona,na matokeo yakawa yanatia moyo, lakini bado is a subject of research.

Huko Ulaya imeonekana watu wenye "very serious healthy conditions" kama vile leukemia,ndio wako vulnerable to covid 19 severe effects,na still age matters, kwamba mwenye magonjwa mengine akapata covid 19 akiwa age kubwa anakuwa vulnerable kwa severe conditions kuliko mgonjwa mwenye magonjwa mengine akapata covid 19 akiwa na umri wa chini.

Haimaanishi hakuna vifo ata lower age ila fatality rate inapishana kwa kiwango kikubwa sana hata kwa wale wenye compromised immunity at different age with exceptional cases considered.
So still our young generation inaweza kuwa advantage kubwa kwetu.

We really need our heads here aisee.Hii kitu tunahitaji kutuliza vichwa sana.
 
Stimulus package eee mmmhhhh stimulus package mhhhhh
Bongo bado hamjafika huko waachieni nchi zilizoendelea ambapo kama mwananchi hana kazi analipwa marupurupu ya kujikimu kila mwezi
LAKINI TUNARUHUSIWA KUOTA USINGIZI SI BURE SILIPII KODI
 
Salary Slip,
Uzuri ni kuwa hapa Europe penyewe tayari wamesha chukua hizo hatua, hakuna mtu kuingia hapa ambaye si mkazi wa Europe, especial shengen countries, inamaana kuwa hakuna ndege toka hapa Ulaya zitakuja huko Afrika labda kwa safari muhimu sana. Schiphol airport Amsterdam imeshefungwa, labda Heathrow airpot England, lakini mipaka yote ya EU imeshafungwa.
 
Serikali ipange tu wananchi wote tupewe chochote japo kila wiki mambo ya kubagua hayafai


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Zitto, Umetoa ushauri mzuri sana ila mimi nina wasi wasi na hili moja la kupeleka bungeni hoja hii ya corona.

Waswasi wangu ni kwamba bunge letu kwa sasa siyo tena chombo huru cha kujadili hoja nzito kwa weledi. Limegubikwa na itikadi za vyama na ushabiki wa ki kambi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zitto,

Brother Zito ni ushauri mzuri, lakini lazima tujue kuwa sasa hivi dunia imeingia kwenye vita vya tatu vya Dunia, tofauti na vita vingine vya dunia vilivyo pita sasa hivi dunia inapigana vita na adui asiye onekana kwa macho yaani nature au kama upepo lakini impact yake ni kama vita ya dunia nzima, tofauti ni kuwa hatu hitaji kujificha kwenye maandaki au bankers kwa hapa Ulaya,

miji yote mikubwa dunia ipo empty japo kuwa adui haonekani wala harushi mabomo, lazima wachukue hizo hatua wapende wasipende sababu dunia nzima imesimama katika shughuli za kiuchumi, Europe yenyewe na Amerika ambao wanashikiria %80 ya uchumi wa dunia kila kitu kime simama au kina simama vipi kuhusu Tanzania?

EU imeshafunga mipaka yake yote angani, majini na ardhini, kwa hiyo hata Tanzania wasipo funga mipaka yao lakini automatic imeshwa fungwa sana sana wajiandae kuhusu jinsi gani wanaweza kukabiliana na hiyo hali. labda waruhusu connection na China sababu kule hali imetulia.

Mimi ni Bongo lakini nimehamia hapa Ulaya muda mrefu na mke wangu ni mrupe wote tunafanya kazi kwe sector muhimu kwa sasa inabidi tuende kazini watoto wetu wote wapo nyumbani tumejitoa mhanga labda tukiambukizwa na kufa watoto watapata fidia.
 
Umeegemea katika taaluma yako ya Uchumi, Naona umesahau jambo moja la muhimu zaidi, elimu zaidi kuhusiana na virusi hivi, Watanz
Hana lolote huyu, anatafuta kik ya kisiasa tu. He is one of best opportunists we have in our country. Angekuwa anajali maisha ya watu angetumia nafasi yake kuelimisha watu jinsi ya kujikinga na maambukizi, badala yake anatafuta cheap popularity kwa hoja ambazo haziwezi kutusaidia wananchi kujikinga na maambukizi.

Watu smart wanahamasisha watu wajikinge wasiambukizwe; cheap assumption za kuanza kuamini kwamba tumeshatoka kwenye janga na tuangalie manufaa ya kiuchumi is just political gimmicks. I hate politicians like this dude!
 
Zitto,
Mkuu hili bunge si ndilo lilishauri akiwepo yule Mbunge mchungaji Wa kuteuliwa kuwa wewe uuawe ukufe,Je wamebadilisha nia yao au vipi.Nakushauri usiende huko kwa usalama wa maisha yako.

Mkuu hongera naona uzalendo mkubwa ulionao kwa nchi yako.
 
Nifah,
Ni kweli elimu inahitajika haraka sana,watu hawana elimu sahihi kuhusu njia za kujikinga dhidi ya virus hivyo matokeo yake wanafanya mambo ya kijinga na kama taifa tunaonekana kama watu wasiojitambua.
 
Ndugu yangu Zitto mbunge mwenzio Mb Msigwa alitaka bunge lijadili ugonjwa wa Corona, CCM kwa uwingi wao wakasema hatutaki habari hizo hapa bungeni sasa atakusikia nani? Watanzania bado hatujitambui labda mpaka aseme Kibajaji.
Wakati nyie mnajadili habari za kuthibiti corona wenzenu wabunge haohao hawaelewi.Nimesoma jinsi ambavyo kamati ya bunge wanaendelea kwa pamoja kufanya ziara kwenye Chuo Cha Maendeleo ya Jamii na kusababisha mkusanyiko usiokuwa wa lazima.Nadhani ni vema na wao wakaepuka mkusanyiko.
 
Salary Slip, Usijumuishe Afrika kwa umoja wetu...sema baadhi ya nchi Duniani.

Afrika kuna nchi zimefunga. Ulaya kuna nchi hazijafunga. Afrika kuna nchi hazijafunga Ulaya kuna nchi zimefunga.

-SA Ramaphosa alishatangaza kufunguia nchi zenye athari cases nyingi....Masisi alishafanya hivyo pia...Museveni naye alishaweka masharti ya safari Uganda.
 
Back
Top Bottom