TheChoji
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 5,771
- 17,849
Leo nilienda Mlimani City kwa shughuli zangu binafsi, niliyoyaona yamenisikitisha sana. Watu wamejawa na ulimbukeni wa ajabu, wanavaa zile mask kama fashion huku wakiwa hawazingatii tahadhari nyingine.
Mentality ya watu wengi ni kwamba corona itakuja na kupita ndani ya siku/wiki chache. Niliwahi kusema humu kwamba endapo corona ikilipuka hapa kwetu na ikaathiri watu na kuua kama kule China ama Italy, hali itakua mbaya sana!!
Najaribu kuangalia watu wanaofanya maigizo sasa hivi ya kujidai kuvaa mask, najiuliza hivi corona iki persist angalau kwa miezi sita tu, je watakua na hela za kununua mask mpya kila siku? Kwanza hata hela ya kula watakua nayo? Na hizo mask zitakuepo? Ikiwa sasa hivi tu ugonjwa haujasambaa tayari mask zimeadimika? Hizo mask watu wanazochezea watakuja kuzikumbuka.
China wamepambana na corona tangu november mpaka sasa na bado hawajaimaliza, sisi tunacheza cheza hapa na ujinga ujinga mwingi we ngoja tu.