Zitto: Ushauri wangu kuhusu Mlipuko wa Korona

Zitto: Ushauri wangu kuhusu Mlipuko wa Korona

Huna Akili hata chembe. Nilidhani unataka kusema Jambo la maana kumbe unataka kuwachangisha watz washibishe matumbo ya kina bashite na kina ole sabaya na babu yao meko.
 
... duh! Kila mtanzania kwa sasa ni profesa wa covid-19!
 
Kutokana na janga la ugonjwa wa Covid-19, napendekeza Vyama vya siasa, Makampuni, Mashirika, asasi na wadau mbalimbali kuiunga mkono serikali na mapambano dhidi ya Coronavirus.

Napendekeza serikali ianzishe njia mbalimbali za uchangiaji ikiwemo M-PESA, HALOPESA, TIGOPESA, AIRTEL MONEY, T-PESA, Account za Bank nk.

Fedha hizo zitumike kwa ajili ya kupambana na Coronavirus tu. Kama fedha hizo zitabaki, zitumike kwa ajili ya miradi ya Afya.

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa ushenzi waliofanya wakutofunga mipaka .
Mpaka athali zinatukuta.
Siungi mkono
Na naomba watu wasichangie
.Kama wameamua Tufe acha tufe wote tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutokana na janga la ugonjwa wa Covid-19, napendekeza Vyama vya siasa, Makampuni, Mashirika, asasi na wadau mbalimbali kuiunga mkono serikali na mapambano dhidi ya Coronavirus.

Napendekeza serikali ianzishe njia mbalimbali za uchangiaji ikiwemo M-PESA, HALOPESA, TIGOPESA, AIRTEL MONEY, T-PESA, Account za Bank nk.

Fedha hizo zitumike kwa ajili ya kupambana na Coronavirus tu. Kama fedha hizo zitabaki, zitumike kwa ajili ya miradi ya Afya.

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
... lakini si kuna mfuko wa maafa? Mfuko ambao fedha zake zinatengwa moja kwa moja kutoka hazina ya taifa kila mwaka? Fedha hizo zimeenda wapi? Pili, si tunaambiwa nchi haina shida ya fedha kwa sasa? Kwamba nchi hii ni tajiri sana? Ya nini kuwachangisha wananchi wanyonge?
 
sisi ni tajiri. naona matajiri wanataka kuchangishana!
 
Wazo zuri lakini kuna watu fulani wanaweza kuzitumia kwenye uchaguzi na kununua wanasiasa.
1584623180612.png
 
Kununua ndege hatuchangishani. Ila kupambana na magonjwa tuchangishane. Maana yake ni kwamba hatujui tofauti kati ya vitu muhimu na vitu vya lazima!
 
Jambo muhimu na la haraka ambalo Serikali inataliwa kulitolea tamko ni kuhusu kodi wanazolipa wafanyabiashara kila mwezi, mwaka nk.
Je ni muhimu Serikali kutoa Tax holiday kwa wafanyabiashara kwa kipindi Fulani?
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu wa mwisho (last born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty. Eti ndugu zangu;

Mitandao ya simu Tanzania tusaidieni katika kupambana na Coronavirus Outbreak.

(1) Emergency Number ya kutoa taarifa juu ya uwepo wa mgonjwa mwenye dalili ya Corona NI NDEFU NA NGUMU SANA KUKARIRI (Almost seven digits) hivyo iwekwe katika Menu za Mobile Money (M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money, Halopesa) kwa muda mpaka tatizo litakapoisha.

Kwenye Menu za huduma za Mobile Money kinaweza kuongezwa kipengele za Corona Msaada

(2) Maelezo juu ya njia sahihi za kujikinga na Coronavirus yanaweza kuwekwa katika customer caring number 100 kama ambavyo watu hupiga simu na kupata maelezo juu ya huduma mbalimbali zitolewazo na mtandao husika.

KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Mbona thread yangu imegeuzwa na kuwa comment? Tatizo ni nini labda? Au sisi wengine haturuhisiwi kuanzisha topic kwa maana mawazo yetu ni finyu au?
 
Ushauri wangu kuhusu Mlipuko wa Korona- Zitto

#COVID19TZA Serikali imethibitisha uwepo wa virusi vya Korona Tanzania. Utulivu ni muhimu kwani kukiwa na maandalizi ya kutosha tunaweza kukabili madhara ya mlipuko huu. Nashauri mambo 3 muhimu sana, kwa maoni yangu.

- Tunaona Nchi nyengine kukiwa na ‘panic’ ya chakula. Watu wetu ni fukara sana, bei za chakula zitapanda na wengi hawatamudu.

Pia Serikali haina Akiba ya kutosha ya chakula kwenye ghala la Taifa. Kuna nafaka ya kutosha Siku 3 tu kwa kila Mtanzania. Ni vema Serikali kufanya uamuzi wa haraka kununua chakula ili kukigawa maeneo itakapohitajika.

- Tanzania inategemea Sekta ya Utalii kwa kiasi kikubwa katika Mapato ya Fedha za kigeni na ajira kwa raia wake. Mlipuko huu unaathiri sana sekta hii ambayo inaingizia Taifa wastani wa Dola za Marekani 2.5 bilioni kwa Mwaka sawa na 25% ya Mapato yote ya Fedha za kigeni yanayoingia nchini.

Naishauri Serikali kukutana na Wafanyabiashara wote kwenye sekta ya Utalii na Vyama vya Wafanyakazi kwenye sekta hiyo kwa lengo la kupata tathmini ya Pamoja ya madhara ya mlipuko huu kwa sekta ya Utalii na huduma zake.

Serikali itazame namna ya kuwafidia ( stimulus package) wafanyabiashara Katika sekta hiyo ili kulinda ajira za Wananchi. Ikiwezekana fidia iwe ni kulinda ajira kwa kufidia gharama za wafanyakazi ( payroll costs).

- Waziri wa Fedha na Uchumi apeleke Bungeni Taarifa ya utafiti wa madhara ya mlipuko wa Korona kwa Uchumi wa Tanzania kwa ujumla na Bunge lijadili Kwa maslahi ya Taifa ili kutoa mapendekezo ya kibajeti kuhami Uchumi wa Nchi yetu na haswa kulinda biashara ndogo, Wafanyakazi kwenye sekta zilizo hatarini kama Utalii, huduma za vyakula, usafirishaji na uchuuzi.

Zitto Kabwe, MP
Kiongozi wa Chama
ACT Wazalendo
17/3/2020
Kiongozi wa chama, mshauri na mtaalamu wa kila jambo. Iwe uchumi, iwe siasa, iwe sayansi, ni mwandishi habari, mtunzi wa vitabu, n.k.
Nionavyo hakuna anachojua. Ni kama wale warembo wa kurasa za magazeti.
 
Ushauri wangu kuhusu Mlipuko wa Korona- Zitto

#COVID19TZA Serikali imethibitisha uwepo wa virusi vya Korona Tanzania. Utulivu ni muhimu kwani kukiwa na maandalizi ya kutosha tunaweza kukabili madhara ya mlipuko huu. Nashauri mambo 3 muhimu sana, kwa maoni yangu.

- Tunaona Nchi nyengine kukiwa na ‘panic’ ya chakula. Watu wetu ni fukara sana, bei za chakula zitapanda na wengi hawatamudu.

Pia Serikali haina Akiba ya kutosha ya chakula kwenye ghala la Taifa. Kuna nafaka ya kutosha Siku 3 tu kwa kila Mtanzania. Ni vema Serikali kufanya uamuzi wa haraka kununua chakula ili kukigawa maeneo itakapohitajika.

- Tanzania inategemea Sekta ya Utalii kwa kiasi kikubwa katika Mapato ya Fedha za kigeni na ajira kwa raia wake. Mlipuko huu unaathiri sana sekta hii ambayo inaingizia Taifa wastani wa Dola za Marekani 2.5 bilioni kwa Mwaka sawa na 25% ya Mapato yote ya Fedha za kigeni yanayoingia nchini.

Naishauri Serikali kukutana na Wafanyabiashara wote kwenye sekta ya Utalii na Vyama vya Wafanyakazi kwenye sekta hiyo kwa lengo la kupata tathmini ya Pamoja ya madhara ya mlipuko huu kwa sekta ya Utalii na huduma zake.

Serikali itazame namna ya kuwafidia ( stimulus package) wafanyabiashara Katika sekta hiyo ili kulinda ajira za Wananchi. Ikiwezekana fidia iwe ni kulinda ajira kwa kufidia gharama za wafanyakazi ( payroll costs).

- Waziri wa Fedha na Uchumi apeleke Bungeni Taarifa ya utafiti wa madhara ya mlipuko wa Korona kwa Uchumi wa Tanzania kwa ujumla na Bunge lijadili Kwa maslahi ya Taifa ili kutoa mapendekezo ya kibajeti kuhami Uchumi wa Nchi yetu na haswa kulinda biashara ndogo, Wafanyakazi kwenye sekta zilizo hatarini kama Utalii, huduma za vyakula, usafirishaji na uchuuzi.

Zitto Kabwe, MP
Kiongozi wa Chama
ACT Wazalendo
17/3/2020
Kaka Zitto, muishinikize serikali ifunge mipaka kwa muda jamani tunaangamia! Uhai wa raia ni zaidi ya haya mambo ya uchumi.
 
Haya ndiyo maneno, hizi ndizo hoja tunahitaji wana CCM, siyo mipasho wa wakatikia kuni akina Lema na Mbowe.

Nadhani Mmawia na genge la wahuni wenzako akina Nyonyoma mnaelewa sasa maana ya hoja, mwezenu kaleta maoni yaliyojaa hoja na serikali lazima itie jicho hapa.
Sasa kwanini mnamtishia kifo?
 
Nawaza tu kama tuna akiba ya kutosha ya fedha za kigeni kusaidia nchi endapo janga hili litakuwa endelevu huku uchumi wa dunia ukiendelea kuyumba.

Hata hali hii ya kushindwa kuzuia ndege kuingia nchini,kufunga mipaka,n.k, bila shaka ni matokeo ya hofu ya serikali kukosa mapato na hali hii inaathiri nchi nyingi sana za kiafrika na ndio maana zinashindwa kuchukua hatua kama ilivyo kwa nchi za Ulaya na Marekani zenye uchumi imara.

Wakati nchi za Ulaya na Marekani wanazuia ndege kuingia katika nchi zao pamoja na kufunga mipaka huku baadhi yao wakikiri walichelewa kuchukua hatua kama hizo,Afrika, sio kama tunashindwa ku-take advantage na kujifunza,bali umasikini ndio unaotufanya tunasita kuchukua kama zinazochukuliwa na mataifa hayo yenye uchumi mkubwa.

Swala la hii serikali kutoa stimulus package sio rahisi labda kwakuwa huu ni mwaka wa uchagu.

Usisahau serikali haijaleta coronavirus!!!
Mbona serikali haijaleta mvua lakini mafuriko yakisomba daraja mnajenga na kuwatumbua watu wa ujenzi? Kwani nani kasema Corona imeletwa na serikali? Huko ni kutusanifu wananchi.
 
Back
Top Bottom