Zitto: Ushauri wangu kuhusu Mlipuko wa Korona

Zitto: Ushauri wangu kuhusu Mlipuko wa Korona

Kumekuwa na kawaida ya kubadilisha matumizi ya pesa.

Posho za watumishi wa afya tunaomba zisicheleweshwe bila kisingizio. Wako vitani wanahitaji pesa iwatie morale kwenye majanga.

Sahau yaliyofanyika huko bukoba, na ajali ya Arusha.

Nimetanguliza kutoa tahadhari ili wajue kuwa pesa isije leta corona part two.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ambae ana mtazamo wa lumumba aache huu uzi. Maana wengine kule walilinganisha virus vya corona na vyama vya upinzani hasa chadema. Huu ndio muda nenda hospital na shati lako la kijani tukushangilie!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa watu kweli wana hali ngumu, kupambana na adui asiyeonekana sio mchezo. Bora hata vita vya bunduki unamuona adui yule pale then unaamua umuapproach vipi.

Hawa ndio wanajeshi sasa, tafadhali serikali waajirini na wale walioko mtaani ili wakaongeze nguvu kazi.
Unforgetable
 
Napenda kuanzisha mada juu ya wote wenye mapenzi mema na taifa letu.

Tutoe ushauri, maoni, mapendekezo juu ya wajibu wa serikali na sisi wananchi juu ya wajibu wa kila mmoja ktk kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huu wa virusi vya korona.

Natumai jamiiforums inatembelewa na viongozi wa kisiasa, kidini na kijamii, itatoa picha ni hatua gani za kujadili na kuchukua.

Mods, ikiwapendeza mnaweza weka mada hii hapo juu

Karibuni
 
Kutokana na janga la Corona, taasisi, makampuni na mashirika binafsi yametoa likizo bila kikomo bila malipo au kusitisha ajira za wafanyakazi wao bila kufuata taratibu.

Ni wakati sasa wa serikali kutoa kauli juu ya jambo hili ili kulinda soko la ajira nchini. Ukimya wa serikali kwenye suala hili utaweza kuwaumiza wafanyakazi wengi kwenye sekta binafsi.

Aidha serikali kupitia mifuko ya hifadhi ya jamii hususani NSSF iweze kuwalipa wafanyakazi wote waliopo kwenye sekta binafsi ambapo ajira zao zimeathirika moja kwa moja hususani sekta ya utalii na usafirishaji.

Kauli na maagizo ya serikali juu ya muelekeo ya sekta binafsi nchini inahitajika sana kuokoa mkwamo wa kiuchumi nchini.
 
Back
Top Bottom