Uchaguzi 2020 Zitto: Wagombea wote 18 wa ACT-Wazalendo kisiwani Pemba wameenguliwa

Uchaguzi 2020 Zitto: Wagombea wote 18 wa ACT-Wazalendo kisiwani Pemba wameenguliwa

Ninachoamini mimi hakina mashiko kwa sasa, Jambo la msingi ni Mwami kutoa sababu za kwanini wagombea wao wameondolewa kugombea na Tume ya Uchaguzi Zanzibar.

Hilo la kukosea kujaza fomu ni swala la kiufundi sana na kilugha na huwezi kulisemea bila kujua specifics zake!
Blah blah blah....
 
Kisiwani Pemba, majimbo 18/18, Wanaenguliwa wagombea wa @ACTwazalendo systematically. Tutafuata hatua zote za kisheria kuzuiwa kinachofanywa. Halafu tutajua la kufanya. Mpaka sasa Tanzania nzima wameshaengua wagombea ubunge 44 wa ACT Wazalendo kwa sababu za kipuuzi sana

From zitto kabwe

View attachment 1550045
Ni sababu za kipuuzi lakini zinazokidhi sheria au ni za kipuuzi lakini hazikidhi sheria?
 
Sie tunasubiri taarifa ya Tume, hizi za akina Zitto ni ukiukwaji wa maadili na sheria za uchaguzi. Hizi ni mbinu za kutaka kuvuruga uchaguzi.
 
Sie tunasubiri taarifa ya Tume, hizi za akina Zitto ni ukiukwaji wa maadili na sheria za uchaguzi. Hizi ni mbinu za kutaka kuvuruga uchaguzi.
Kwa yanayoendelea tume ndo chanzo cha uvurugaji amani
 
CCM mnachofanya hapa ni kuunganisha upinzani ambao mpaka sasa wameshindwa kuungana kwa hiari yao. Huu uzembe mnaoufanya mtaujutia.

Kinana uko wapi, wakati mauzembe haya yanafanywa na akina Bashiru na Polepole.
 
Naona tume imekuwa Na hasira kama mamba aliyekosa target ya kukamata windo!
 
Back
Top Bottom