Ziwa Nyasa limeporwa kikamilifu?

Ninachojiuliza mbona wanamega juu na sio chini Mozambique..tumekuwa wapole sana au mazoba
 
Nakubaliana na wewe. Sisi cha kufanya ni kusema malawi wanapotosha umma na dunia kwa kuchapisha ramani zinazoonesha uongo.
Yes, tukinyamazia mwisho lazima hili eneo lije kuleta matatizo makubwa pande zote mbili
 
Hata jina la Nyasa si la kwao pia maana huwa nasikia nchi yao wanajiita Nyasaland
 
Fuatilia kwa makini huu mgogoro utagundua baadae huu mgogoro utatuelemea.

Wenzetu wao wanaweka mpangilio fulani huko umoja wa mataifa ili waonekane wana haki na eneo lote
 
Kwenye hilo ziwa kuna oil na gesi ndo maana jamaa wamefanya hivyi na wameshaanza kifanya exploration kwenye sehemu iliokua mpaka na Tanzania yaani kati mati ya ziwa
 
Fuatilia kwa makini huu mgogoro utagundua baadae huu mgogoro utatuelemea.

Wenzetu wao wanaweka mpangilio fulani huko umoja wa mataifa ili waonekane wana haki na eneo lote
Kuonekana una haki haimaanishi hiyo haki unayo, kumbukumbu za mgogoro na sehemu ulipofikia zipo. Sasa huwezi kukurupuka kivyako vyako ukaendelea na mipangilio yako ya kumiliki ziwa zima, labda ulimiliki kimoyomoyo. Kasheshe ni pale utatakapotaka kulimiliki kivitendo ndo sebene linapoanza kuchezwa hapo na ile ngoma ya sindimba, naamini wamalawi bado wanaupenda ugali..
 
ramani iko hivyo miaka yote tangu tunapata uhuru.wakoloni ndio walichora hivyo ila Tanzania tuliikataa hiyo ramani kutokana na sheria ya kimataifa inayosema kama kuna, water body mpakani basi mpaka ni katikati ya hiyo water body ili nchi zote zinazopakana zitumie resources za hiyo water body ndio maana huu mgogoro upo tangu tunapata uhuru
 
Nafikiri walifanya hivyo kwa kuona Tanganyika ina water bodies nyingi hivyo kutaka nchi za ndani ndani na zenyewe ziambulie waterbodies kidogo sema walichokosea wangemega kabisa na meneo ya nchi kavu ya huku Tanganyika ili wananchi wanaozunguka hilo ziwa wanufaike vizuri na kutokuwepo migogoro.
 
Kwenye hilo ziwa kuna oil na gesi ndo maana jamaa wamefanya hivyi na wameshaanza kifanya exploration kwenye sehemu iliokua mpaka na Tanzania yaani kati mati ya ziwa

Kama Wamalawi wanafanya exploration ya mafuta katikati ya Ziwa huku sisi tuko kimya tukiwa tumezubaa bila kupinga kwa nguvu zote basi maana yake ni kuwa watatengeneza precedence na reality on the ground na itazoeleka, kisha baada ya hapo watosegea ndani ya maji tunayodai ni yetu, na kisha watasogea mdogomdogo kuelekea upande wetu.
HUU NI MUDA MUAFAKA WA KUPINGA KWA NGUVU ZOTE EXPLORATION YA MALAWI KWENYE MAJI TUNAYODAI NI YETU, TUKIZUBAA HAO JAMAA WANACHEZA LONGTERM PLAN, WATAENDELEA KUSOGEA MDOGO MDOGO HUKU WAKIJIDAI WANATAFITI MAFUTA!

Ni lazima tupinge sasa hiyo move yao, la sivyo miaka 50 ijayo hatutakuwa na basis ya kuclaim hilo ziwa!
 
Atakuwa anaungwa mkono na Ujerumani na washirika wake
 
Asante sana mkuu
 
Mgogoro ni wa mataifa ya Ulaya baada ya kutamani rasilimali zilizopo chini ya ziwa hilo.

Wanawatumia viongozi wa Malawi huku raia wakiwa fresh tu
 
Mgogoro unaonesha Uingereza ndio inatengeneza huu mgogoro ikishirikiana na viongozi wa Malawi
 
Chanzo cha hii ramani ni wazungu wenyewe kwa kutumia picha za satellite wameonesha ziwa lote ni la Malawi
 
Ndio tatizo letu kubwa!

Ramani imebadilishwa kwa nchi yetu kumegwa raia wanasema mbona maisha yapo kawaida... Ukija kwa viongozi ndio kabisa hata hawaelewi kama mambo yamefika huko 😢
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…