Binafsi hiki kitu kilinifikilisha Sana enzi za jk na kujaribu kufuatilia habari mbalimbali, mwishowe nilifika kwenye ukweli mchungu ya kwamba ziwa nyasa lote ni la Malawi ingawaje wagawaji wa mipaka kipindi hicho yaani wakoloni walifanya makosa ya ugawaji kwa kutozingatia baadhi ya kifungu. Kifungu hicho ni kwamba mipakani Kama Kuna ziwa au bahari basi mpaka lazima upite katikati ili kila nchi inufaike na maji. Kwa kuzingatia kifungu hicho wareno ambao walikuwa watawala wa msumbiji walikaa mezani na waingereza ambao walikuwa watawala wa Malawi na kukubaliana kuchora mpaka upya ndiyo maana utaona katika ziwa,msumbiji na Malawi mpaka umepita katikati. Lakini kipindi hayo yanafanyika Tanganyika na Malawi zote zilikuwa chini ya waingereza, kwahiyo hawakuona haja ya kubadili mpaka yote ni makoloni yao na hali hiyo iliendelea mpaka hizi nchi zikapata uhuru. Sasa Malawi hawataki kukaa mezani kugawana ziwa nyasa wanadai kwa mujibu wa mipaka ya mkoloni ziwa ni mali yao, ni kweli lakini mbona walikubali kufanya marekebisho enzi za wakoloni Kati yao na msumbiji? Hii inaonesha haki haikutendeka ndiyo maana Hilo liliwezekana ila halikufanyika enzi za muingereza kwa sababu hakuona haja ya kufanya hivyo nchi zote mbili ziko chini yake. Sasa tukae mezani tugawane ziwa,Malawi hawataki wanasema tufuate mpaka wa wakoloni. Tukumbuke mgogoro huu upo tangu enzi za Nyerere na Kamuzu Banda