Ziwa Nyasa limeporwa kikamilifu?

Ukiona hivyo ujue tulishindwa hiyo kesi kwenye kile kikao cha usuruhirishi. Shida iko kwenye serikali yetu haina uwazi hata kidogo,hata kwa jambo la hatari kama hili,ilipaswa wananchi wajulishwe ile kesi ya usuruhishi kuhusu hilo umefikia wapi?. Zaidi hatuna habari na hayo mambo. Tulikuwa tunapambana kumbana sana Mbowe na watu wake.
 
Acha kudanganywa na hiyo mipaka ya Satelite
 
wamalawi wasije kutumiwa kutaka kuchota gesi yetu na nchi kubwa. wakifanya hivyo watatusumbua .
maana kama labda wameshindwa kuchota kupitia tanzania watapitia malawi ili tu wafanikiwe lengo lao .
 
Acha kudanganywa na hiyo mipaka ya Satelite
Wewe upo dunia ya wapi? Satellite ndio hipima karibia kila kitu siku hizi hadi viwanja.
Kama camera za satellite zimeelekezwa kupitisha mpaka pembeni ya ziwa ujue wale wale waliokufanya mtumwa wanaihakikishia dunia kwamba hatuna mamlaka na hilo ziwa tena.

Ni suala la muda tu tutakuja kuona vitendo
 
Sasa wewe amini hizo satelite zako tulioko field tunajua
 
Sasa wewe amini hizo satelite zako tulioko field tunajua
Amiri jeshi wenu siku akiwaambia mrudi nyuma kilomita 20 kwa maana mpo ndani ya nchi nyingine utapinga?

Aliyekupitisha kuwa mwanajeshi alikosea sana
 
daah upana wa 20km ni kutoka mwenge to daraja la kigamboni na urefu wa 220km ni dar to moro. huu ni utani sasa
 
Amiri jeshi wenu siku akiwaambia mrudi nyuma kilomita 20 kwa maana mpo ndani ya nchi nyingine utapinga?

Aliyekupitisha kuwa mwanajeshi alikosea sana
Wewe hujui kuwa Google imenakili Ramani ya Waingereza? Au unazani satelite inajichorea yenyewe
 
Si tuingie vitani tu zipigwa aisee Kwan kuna tatizo gan majeshi tunayo tatizo nn aisee tunapiga mpaka mji mkuu na makao makuu ya malawi au tupeleke bibalaka huko waingie madalakani tubadili mipaka
Lowassa tu ndio alithubuti kumtishia yule mama
 
Kama ipo hivyo siku zote mbona Tanzania tunafanya shughuli zetu kama kawaida kwenye hilo ziwa?

Ingekua uongeayo ni kweli, basi tusingedhubutu kufanya shuguli za kiuchumi kwenye hilo ziwa
Huujui huu mgogoro Upo siku nyingi tangu enzi za Nyerere na Ndio maana shughuli zinaendelea.
 
Kama wanajiamini Ziwa lote ni lao waanze kufanya mishe mishe zao ziwa zima waone MOTO [emoji91][emoji91]
Wanachofanya wao ni vita ya kisayansi. Nyie subirini hapo hapo hiyo vita yenu ya kishamba ya mabunduki.
Nataka niwaambie hapo ndio tujijue sisi bado hata uelewa tu tunashuka kwa kasi kwenda chini. Hata Malawi wametupiga bao sasa. Tumekazana tu kutekana humu humu ndani.
Sisi tumepanga wanajeshi mpakani. Malawi wanaendelea taratibu kujimilikisha ardhi yetu kisheria kwenye jumuia za kimataifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…