Ziwa Nyasa limeporwa kikamilifu?

Kila kitu kinaanzia kama punje. Ilianza kama chokochoko. Lakini Malawi naona wakakomaa kulidai hilo hilo ziwa kimataifa. Imeanzia kwanza kutambulikana mipaka waliyoidai kisheria. Baadae wanaweza wakaanza utaratibu mwingine kisheria utakaowatambua wao kabisa kwamba ndio wenye ziwa. Kwa sasa shughuri zote zinaweza zikawa zinaendelea kama zilivyozoeleka,kwa pande zote,ila kwa mipaka hiyo tegemea lolote kwa watoto wako au hata wajukuu. Wenyewe hawataki vita vya mabunduki kama mlivyojitapa nyie. Wanaenda taratibu kisayansi
 
Hao maaskari wanaolindaga mipaka walikuwa wapi hadi wamalawi wahamishe mipaka?

Ina maana hamna wanajeshi kabisa kwenye hilo ziwa!? Kama ni hivyo, basi hatuko salama!
Mpaka sio ukuta kama mtu atakuja kuujenga usiku! Hayo ni mambo ya kwenye makaratasi
 
MTOA mada naungana nae Jambo hili latakiwa fiatiliwa kwa kina na utatuzi wake kufanyika kwa haraka,Amin pia alianza mdogomdogo ,hakuna kitu hufanyika kwa bahati mbaya ,Kama wanaleta za kule Serikali itwambie mapema sie jeshi la akiba tuanze kupasha,wenda hawana nia njema mipaka ya kiwanja ,nchi sio vitu vya kuchezea chezea,lazima kueshimiana katika ilo
 
Kwa jinsi dunia inakoelekea now,tunatakiwa kukuza jeshi.Tuwe na jeshi kubwa la kisasa.For the next 10 years ni muhimu kukuza jeshi la Tanzania.
Huenda post yangu ikaeleweka baadae sana after those 10 years.
 
Kwa jinsi dunia inakoelekea now,tunatakiwa kukuza jeshi.Tuwe na jeshi kubwa la kisasa.For the next 10 years ni muhimu kukuza jeshi la Tanzania.
Huenda post yangu ikaeleweka baadae sana after those 10 years.

Sioni tatizo lolote likitokea kwenye huu utawala wa Lazarus Chakwera. Ni mtu mtulivu na anaiheshimu sama Tanzania na JPM.

Hasara ni kubwa kwao kuliko faida. Wana watu wao wengi sana wanafanya kazi Tanzania na kutuma pesa nyumbani, wanatemegea biashara, usafiri wa kuaminika kutoka Tanzania hadi Malawi na ushikiano mzuri.

Watu wa mpakani wanashirikiana vizuri tu. Ni kweli Tanzania ijiandae kwa zaidi ya miaka 20 ijayo kijeshi na kuwa na jeshi la kisasa.
 
Haya sasa ndo mambo yanayopaswa kujadiliwa kizalendo sio,zile mambo za kupiga kura BET wakati nikipiga kura kwa burnaboy haiathiri usalama wa nchi yangu,swala la BET halihusiani kabisa na uzalendo,uzalendo upo hapa sasa..


By the way,hii ni hatari na inatia wasi wasi+hasira.Kipindi nasoma primary hilo nililitambua kama ziwa Nyasa lkn haya yanayoibuka yanatakiwa tuyatafakari,tuyajadili,tuipigie serikali na vyombo husika kelele waamke juu ya hili...kwekweli wazalendo tutahitaji maelezo juu ya hili,nna uhakika kupitia uzi huu taarifa zitawafikia na siku chache zijazo tutafafanuliwa...[emoji110][emoji1241][emoji110]
 
Sio kweli haya uliyoandika na ramani yako, mpaka uko palepale, na kwa sheria za kimataifa mipaka ya majini kwa nchi mbili huwa katikati kutokana na jiografia ya sehemu husika. Kama ni hivyo unvyosema tungekuwa tunaona shughuli za Wamalawi kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa kwa upande wa Tanzania, kuhusu jina miaka mingi wao huliita hili ziwa Lake Malawi kutukuza nchi yao kwani hawana ziwa lingine kubwa kama hili ni sawa na sisi Watanzania tunapoliita Lake Victoria, Lake Nyanza ilihali Waganda na Wakenya bado wanaliita Lake Victoria, jina halifanyi ziwa kuwa la nchi moja pekee.
 
Tatizo si Chakwera wala wamalawi.
Tatizo ni hawa watu weupe wenye macho ya blue na nywele za dhahabu.
Kuna mapinduzi ya nne ya kimaendeleo duniani yanaendelea now,na yanahusu teknolojia ambazo raw materials ni huku huku Afrika.
Kama wana jambo lao wale hawashindwi kupandikiza mtu in either of the countries in great lakes na mtu huyu akatumika kuleta usumbufu mkubwa.
Angalia kinachoendelea Mozambique.
Nimesema tuimarishe jeshi kwa maono ya mbele sana.kuna kitu kinakuja huko mbele.
 
Mzee wa kujishuku.
 
Huo mkata
Hiyo heligoland treaty ya mwaka 1890 ndiyo iliyotukosesha ziwa sisi watanganyika. Ni kweli kipindi Cha mkataba huo Tanganyika ilikuwa chini ya wajerumani na hao wajerumani ndiyo wakaridhia upuuzi huo bila kuangalia haki za asili ya watu wa tanganyika wanaolizunguka ziwa. Waingereza walilithi hiyo mipaka Kama ilivyo walivyoitawala Tanganyika. Na kwa wao haikuwa tatizo kwa kuwa makoloni yote yalikuwa chini yao
 
Wewe hujui kuwa Google imenakili Ramani ya Waingereza? Au unazani satelite inajichorea yenyewe
Na mwaka 2014-2015 ilikuwa inanakili mipaka ya wapi maana mpaka wa hapo ziwani ulipita katikati ya ziwa?
 

Kwa Malawi hilo linawezekana huko mbeleni sababu Kamuzu alishirikiana sana na Wareno na Makaburu kuithibiti Mozambique.

Lakini sio in immediate future. Ni nchi maskini na dhaifu kupambana na Tanzania, yoyote kwa sasa.

Pia tupo pamoja SADC, COMESA, AU na UN.
 
Kwahiyo wewe ndiyo unajua kuliko mtoa mada kwa hiki ulichoandika ?
Article 2 of paragraph 1 of the heligoland treaty, states that" the boundary between nyasaland and tanganyika ran along the eastern, western and northern shores of the lake until it reached the northern bank of the mouth of songwe river
 
Huujui huu mgogoro Upo siku nyingi tangu enzi za Nyerere na Ndio maana shughuli zinaendelea.
Kumbuka comment yako ya juu ulisema ramani ipo hivyo muda wote kitu ambacho nimekupinga maana hilo eneo niliangalia 2014 nikaona mpaka umepita katikati ya ziwa.
Leo mpaka umesogezwa hadi nchi kavu ambapo kilomita kama 20 zinaonekana zimemegwa Tanzania
 
a
Acha uchochezi, hujaonyesha chanzo cha ramani hizo mbili ulizotuwekea. pia practicability ya mpaka ni shughuli za kiuchumi za nchi. practice haionyeshi kuwa we are restricted that much beyond as you have just shown. acha uchochezi.
 
Asante mkuu, japo sijawahi kupita jeshini nipo tayari pia katika hili
 
Na hizi tasisi zetu za umoja wa kikanda tuzipe nguvu zaidi.Tukiwa wamoja na kushirikiana mambo mengi then itawawia vigumu "wale mabwana" kuja kutuhujumu.
Mwalimu Nyerere alikuwa na maono sana.Alitumia mpaka intelijensia kuhakikisha nani anakuwa kiongozi katika eneo hili lote la SADC.
Yote hii ni kuhakikisha tuna viongozi wanaojuana na kujiona kama familia.Kwa dunia ya leo maslahi ndio yanaunganisha watu.Ifike mahali mmalawi aione Tz ni muhimu kwake kuliko kuihujumu.Na mtz aione Malawi hivyo hivyo.Ni suala la regional integration kiuchumi,kijamii etc.
 
Umetembelea hilo eneo kwa kutumia Google map? Au Google map kwako unaona haina nguvu yoyote katika hili?

Unasikitisha sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…