Zizini TV: Kwenye zizi la ng'ombe, Chui ndiye Mhubiri mkubwa wa "Amani na Utulivu"?

Zizini TV: Kwenye zizi la ng'ombe, Chui ndiye Mhubiri mkubwa wa "Amani na Utulivu"?

Kwanza naunga mkono hoja, pili yule mtu wetu ni muumini wa haki kwa mawazo, maneno na matendo, tatizo sio yeye bali wasaidizi wake wamemdanganya, akadanganyika.
Mwanzo alianza vizuri Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki

Wakupongeza, tukampongeza Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?

Tukaendelea kufagilia Haki Huinua Taifa! Rais Samia kwa Kauli na Matendo ameonesha ni mtu wa Haki. Akitekeleza hili kama alivyosema, atabarikiwa, Tanzania itabarikiwa

Rais Samia ana nia njema Watanzania wapate haki, ila Watanzania hawajui Haki! Je, Tumsaidie kuelimisha umma Katiba, Sheria na Haki au? watu tukajitolea kusaidia.

Mara mambo yakaanza kubadilika, tukashauri ,Ombi kwa Rais Samia, tunakushukuru kwa mahubiri mazuri kuhusu haki, tunakuomba utende unachohubiri yasibaki kuwa maneno tuu lakini vitendo ni tofauti

Ndipo akadanganywa kuhusu uhaini Uhaini My God!. Kuna Uwezekano Anadanganywa na Kadanganyika? I Don't Believe This!. Sitatizwi na Uongo Wao, Natatizwa na The Motives Behind Such Lies!

Tukasaidia kuelimisha PreGE2025 - Wazalendo Wapenda Haki, Msiwe na Wasiwasi, Uhaini ni Matendo na Mipango Mkakati wa Kuutenda, Sio Maneno!, Maneno ni Sedition tuu na Sio Treason!

Tumsamehe bure, sio yeye, ni wasaidizi wake Inawezekana ni Kiburi na Jeuri or Real Busy? Wasaidizi wake hawajamwambia ukweli wa ubatili wa Katiba na Sheria ya Uchaguzi?,Tufanye nini kupata Haki?

Ile October 29, wakamdanganya tena kuwa Gen Zii wanakuja kukuondoa Ikulu, mtoa amri akatoa amri ya zitumike za moto!. Ili Haki Itendeke, Sio Tuu Itendeke, Bali ni Lazima Ionekane Imetendeka!, Kama Tumewashitaki Waandamanaji, Pia Tuwashitaki na Wauaji!

Haki Huinua Taifa. Kilichotokea ni matokeo na sio chanzo. Kama matokeo yanapandishwa kizimbani na chanzo pia kipandishwe!

P
Changamoto ilianza pale vyeo na teuzi zilipotolewa kwa vigezo vya kuropoka kwa kujitoa ufahamu dhidi ya upinzani, ukatili dhidi ya upinzani bila hoja. Utamaduni wa kindugu wa kitanzania ukaanza kumomonyoka.
Hali hii ilizaa uchawa ambao kwao matumizi ya akili siyo kipaumbele na zaidi sana ni mapambano yanayotumia fikra kama za mbwa badala ya za kibinadamu.
Wakati mwingi mbwa hushambulia wageni halali na watu ambao bwana wake angependa wawe salama.
Kazi ya kudhibiti mbwa wakikata kamba na hasa wakiwa wengi siyo rahisi na humsababishia mmiliki lawama, hasara za kulipa na hata mashitaka ya jinai.
Nimetumia lugha kali kuwasilisha, siyo kwa nia ya kuwakwaza wengine, bali ni kufikisha ukweli wenyewe.
 
Somalia na Somaliland zilitengana kutokana na kutokuwepo haki.

Sudan kusini na Sudan zilitengana ziliachana kutokana na kutokuwepo haki.

Kuna mifano kama Nigeria na Biafra , Catalunya na Spain miaka kadhaa napo kulikuwepo mivutano ya kutengana yote hiyo ni sababu ya haki maana haki huleta usawa ambao huzaa kuheshimiana na ndio amani hutokea kama hatua ya mwisho.

Sijawahi kusikia wanaoitwa "waasi" kama vijana walioandamana walioitwa waasi , wahamiaji haramu, vibaka na mengineyo mengi.

Ukichunguza chanzo cha makundi kama M23, Al Shabab, Al Qaeda , Houthis , Hamas na mengineyo mengi yanapambania haki.

NRM ya Yoweri Museveni ilianzia msituni wakipigani haki sio amani walipopata haki amani ikaja na sasa ndio wanataka kuivuruga tena.

CNDD- FDD ambao ndio washirika wapya wa CCM wakiongozwa na Pierre Nkurunzinza walichukua dola wakianzia kama political wing ambayo waliitwa waasi pia.

Hadi hapo hakuna mahali watu wanapigania amani bali haki .
 
Na hata "tukitulia kimya", wao ndio watakaokuwa wanaamua ni HAKI ipi upewe, na ipi unyimwe. Hawa ni miungu.
Ukiwasikiliza sana hawa watawala utaona kuwa haki ni kama zawadi ambayo wao wanaitoa kwa wananchi. Ili update zawadi hiyo ni lazima usiwasumbue, kuwaudhi hata kuwaulizia. Ukimuahidi mtu zawadi halafu akawa anakuuliziaulizia mwisho unaamua kumnyima...
 
Ukiwasikiliza sana hawa watawala utaona kuwa haki ni kama zawadi ambayo wao wanaitoa kwa wananchi. Ili update zawadi hiyo ni lazima usiwasumbue, kuwaudhi hata kuwaulizia. Ukimuahidi mtu zawadi halafu akawa anakuuliziaulizia mwisho unaamua kumnyima...
Hawa wanatumia kutawala Tanzania wakifuata taratibu za tawala za kiarabu. Tatizo lipo hapo.
 
Aliposema walioandaman wametoka nje alikua na ushahidi na kidhibiti gani?
Rais wa nchi akisema kitu ni ameambiwa na wasaidizi wake, hivyo baada ya wasaidizi wake kujua kiwango cha akili za bosi wao, wamekuwa wanamdanganya sana!.

Hata issues za uhaini, walimdanganya Uhaini My God!. Kuna Uwezekano Anadanganywa na Kadanganyika? I Don't Believe This!. Sitatizwi na Uongo Wao, Natatizwa na The Motives Behind Such Lies!

Angalia jinsi Rais Samia Anavyodanganywa na wasaidizi wake na jinsi tulivyotaka kumsaidia Rais Samia Mgeni Rasmi AGM ya TLS: Wanasheria Tumweleze Ukweli Kuhusu Ubatili wa Katiba Yetu na Sheria Zetu, Turudishe Haki Kuu ya Msingi

Aliingia mitini, hakuja kwenye hii event!.

P
 
Sasa kama anaweza kudanganyika kiasi hicho, yeye akili zake ziko wapi? Na je ana sifa za kukalia hicho kiti?
Sifa za mtu kuwa zimeainishwa kwenye ibara ya 21 na 63 ya katiba yetu, kipimo cha kiwango cha IQ, sio sehemu za sifa za uongozi.

P
 
Back
Top Bottom