Zizini TV: Kwenye zizi la ng'ombe, Chui ndiye Mhubiri mkubwa wa "Amani na Utulivu"?

Zizini TV: Kwenye zizi la ng'ombe, Chui ndiye Mhubiri mkubwa wa "Amani na Utulivu"?

Kukiri kuua kwa sababu waliandamana haikuwa data kwamba kichwa cha mnenaji kimejaa kamasi tu
According to utii kwa mamlaka, sababu ya kuuliwa kwa risasi za moto, sio kwasababu waliandamana, no!, wameuliwa kwa kupigwa risasi za moto kwasababu walikuwa wanakwenda Ikulu kumuua yeye na kupindua serikali, hivyo ilibidi itumike nguvu kubwa stahiki kuzuia nchi kupinduliwa!. Hivyo nguvu iliyotumika ni nguvu stahiki na sahihi!

Naendelea kusisitiza, kufuatia wasaidizi wake kuujua uwezo wake, wanamdanganya sana kwa kisingizio kuwa wanamsaidia, lakini kiukweli, sio tuu hawamsaidii, bali wengine ndio kwanza wanamppteza.

P
 
Yaani kitu hiki ni cha ajabu sana...yaani tusidai haki hadi tutulie kimya...
Tukae kimya kwa amani ili ''wapate nafasi nzuri ya kutafakari'' ni haki ipi tupewe na ipi ni hisani.
Wamefikia mahali wanageuza haki ya Mikutano ya siasa kama hisani wakinena '' mikutano imeruhusiwa''
 
L
Mimi namtazama mfugaji wa chui aliye zizini, sijui ana jisikiaje kuona wananchi waki teswa au kuuliwa na mgeni wa visiwani.

una mlinda chui ili uendelee kupata ulaji wa muda mfupi, una sahau historia haitafutika na kisasi kitalipwa.
Unajua ni kwa sababu wanaomlinda chui wanafaidika na chui; lakini historia inatufundisha kuwa kuna siku chui hula wanaomfuga!
 
Tukae kimya kwa amani ili ''wapate nafasi nzuri ya kutafakari'' ni haki ipi tupewe na ipi ni hisani.
Wamefikia mahali wanageuza haki ya Mikutano ya siasa kama hisani wakinena '' mikutano imeruhusiwa''
Mkuu, siyo tu hilo uhai wetu wenyewe ni hisani yao. "Nguvu iliyotumika (mauaji tuliyoyafanya) inaendana na matukio yenyewe". Yaani, sasa hivi kuvuta kwetu pumzi ni hisani yao. Wakikorofishika tu wanaweza kutuondolea...
 
Kwanza naunga mkono hoja, pili yule mtu wetu ni muumini wa haki kwa mawazo, maneno na matendo, tatizo sio yeye bali wasaidizi wake wamemdanganya, akadanganyika.
Mwanzo alianza vizuri Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki

Wakupongeza, tukampongeza Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?

Tukaendelea kufagilia Haki Huinua Taifa! Rais Samia kwa Kauli na Matendo ameonesha ni mtu wa Haki. Akitekeleza hili kama alivyosema, atabarikiwa, Tanzania itabarikiwa

Rais Samia ana nia njema Watanzania wapate haki, ila Watanzania hawajui Haki! Je, Tumsaidie kuelimisha umma Katiba, Sheria na Haki au? watu tukajitolea kusaidia.

Mara mambo yakaanza kubadilika, tukashauri ,Ombi kwa Rais Samia, tunakushukuru kwa mahubiri mazuri kuhusu haki, tunakuomba utende unachohubiri yasibaki kuwa maneno tuu lakini vitendo ni tofauti

Ndipo akadanganywa kuhusu uhaini Uhaini My God!. Kuna Uwezekano Anadanganywa na Kadanganyika? I Don't Believe This!. Sitatizwi na Uongo Wao, Natatizwa na The Motives Behind Such Lies!

Tukasaidia kuelimisha PreGE2025 - Wazalendo Wapenda Haki, Msiwe na Wasiwasi, Uhaini ni Matendo na Mipango Mkakati wa Kuutenda, Sio Maneno!, Maneno ni Sedition tuu na Sio Treason!

Tumsamehe bure, sio yeye, ni wasaidizi wake Inawezekana ni Kiburi na Jeuri or Real Busy? Wasaidizi wake hawajamwambia ukweli wa ubatili wa Katiba na Sheria ya Uchaguzi?,Tufanye nini kupata Haki?

Ile October 29, wakamdanganya tena kuwa Gen Zii wanakuja kukuondoa Ikulu, mtoa amri akatoa amri ya zitumike za moto!. Ili Haki Itendeke, Sio Tuu Itendeke, Bali ni Lazima Ionekane Imetendeka!, Kama Tumewashitaki Waandamanaji, Pia Tuwashitaki na Wauaji!

Haki Huinua Taifa. Kilichotokea ni matokeo na sio chanzo. Kama matokeo yanapandishwa kizimbani na chanzo pia kipandishwe!

P
Uchawa tuu
 
Back
Top Bottom