Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini Cameroon kufuatia uchaguzi wa urais uliofanyika Oktoba 12, 2025, ambapo Rais aliyepo madarakani, Paul Biya, anatafuta kuendelea kushikilia madaraka baada ya miaka 43 uongozini.
Biya, mwenye umri wa miaka 92 na anayejulikana kama Rais mzee zaidi duniani, anakabiliwa na wagombea wengine tisa. Ikiwa atashinda, ataanza muhula wake wa nane mfululizo, huku uchaguzi unaofuata ukitarajiwa kufanyika mwaka 2032
Waziri wa Mambo ya Ndani, Paul Atanga Nji, alisema kuwa zoezi la kupiga kura lilifanyika “bila matatizo makubwa” nchini kote. Hata hivyo, kulitolewa wito wa kususia uchaguzi huo katika maeneo yanayozungumza Kiingereza upande wa magharibi, na kulikuwa na taarifa za mapigano katika kaskazini mwa nchi.
Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa ndani ya siku 15 baada ya upigaji kura
Kabla ya uchaguzi, vyama vya upinzani vililalamika kuhusu juhudi za kuwakandamiza wafuasi wao. Mwezi Agosti, Baraza la Katiba lilimzuia Maurice Kamto mwenye umri wa miaka 71, ambaye alionekana kuwa mpinzani mkuu, kushiriki katika uchaguzi huo.
Oktoba 12, 2025 wafuasi wenye hasira wa mgombea kinara wa upinzani na aliyewahi kuwa mshirika wa karibu wa Biya, Issa Tchiroma Bakary (76), walijitokeza barabarani katika ngome yake ya Garoua. Wal clash na vikosi vya usalama vilivyolazimika kutumia gesi ya machozi, baada ya nyumba ya Tchiroma kuwekwa chini ya ulinzi mkali
Mapema siku hiyo, Tchiroma alisema amekuwa akipokea vitisho
Hata hivyo, Waziri wa mambo ya ndani alisisitiza kuwa uchaguzi ulifanyika kwa amani bila matukio makubwa katika mikoa yote 10 ya nchi hiyo
Hakuzungumzia moja kwa moja hali ya Garoua, bali alirudia kauli za awali kwamba baadhi ya wagombea wa urais wanapanga kutangaza matokeo kabla ya tangazo rasmi la serikali.
Nji alionya kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayekiuka sheria hiyo
Katika mikoa miwili ambako wanaharakati wa kujitenga walijaribu kuwazuia wananchi kupiga kura, baadhi waliamua kujitokeza kwenye vituo vya kupigia kura, lakini wengi walibaki majumbani kwa hofu ya kulipiziwa kisasi
==========
Vote counting is under way in Cameroon following Sunday's presidential election in which incumbent Paul Biya is seeking to extend his 43 years in power
Biya, who at 92 is the world's oldest head of state, is being challenged by nine candidates. If he wins, it will be his eighth consecutive term in office, with the next election due in 2032
Interior Minister Paul Atanga Nji said that voting took place "hitch-free" across the country. But there was a call for a boycott in the English-speaking regions in the west and there were reports of clashes in the north.
The final result should be known within 15 days of the vote.
In the run-up to the election there were complaints from the opposition of attempts to suppress their support
In August, the Constitutional Council barred 71-year old Maurice Kamto, widely viewed as the main challenger, from taking part
On Sunday, angry supporters of leading opposition candidate and former Biya ally, Issa Tchiroma Bakary, 76, took to the streets in his stronghold of Garoua. They clashed with security forces, who fired tear gas, after his residence was cordoned off
Earlier in the day, Tchiroma had said he was the subject of threats.
"It is not Tchiroma who is the problem, he told reporters, adding that he "places himself under the protection of God and the Cameroonian people."
"I am at home; I will not move. If they intend to come and take me away from home, I will not move," he declared.
Despite this Interior Minister Nji said the polls were held without major incidents in all 10 regions of the country.
He did not comment on the situation in Garoua but rather repeated previous claims that some presidential candidates were planning to publish the results of the election ahead of the official declaration.
Nji described this as a major red line, threatening action against anyone suspected of breaking the law.
In the two restive Anglophone regions, where separatists attempted to bar residents from voting, some did turn out at the polling stations. But many others stayed away for fear of reprisals
Soutrce: BBC