Pesanyingi
JF-Expert Member
- Apr 15, 2023
- 1,157
- 1,983
Exactly ni wapuuzi. Eti mtu kafungua account hajamaliza hata mwezi una hakiki , una hakiki kitu gani??? Some time nikupotezeana muda tu. Mambo ya kizamani sana .....Nmb badilikeni otherwise mtakosa wateja ....kama mnafanya utafiti watu wengi wana kimbia Nmb kwasababu ya usumbufuWanahakiki taarifa ili iweje?
Na kwa nn wafanye hivyo.
Hii benki ya NMB ni wapuuzi sana aisee
Hata uko uliko enda ni usumbufu tu nduguMm niliisha achana nao.nikakomba pesa yangu nikapeleka crdb preassure imepungua
Umeshasema wilaya nzima tawi la benki ni moja. Hakuna namna pambaneni na NMB.Kwamfano hapa nilipo wilaya nzima tawi la nmb ni moja watoa huduma ni kituo kimoja tu,malalamiko makubwa ni wingi wa wateja,pia mtandao kusuasua ,zoezi linachukua dkk 15 hadi 20 kuhakiki mtu mmoja.
Sasa kwa mwendo huko zoezi ni gumu kukamilika kwa wakati mana watu ni wengi foleni ni kubwa na wengi wanaondoka kwa kuchoka kukaa foleni au kuwa na majukumu ya muhmu zaidi.
Ushauri waongeze vituo vya kuhakiki,pia wahakikisha mashine zao zina mtandao wa kutosha..waache kusumbua wateja benki zipo nyingi sana hii kero itawafanya wapoteze wateja.
Wanapenda kuwaona mmejazana nje na ndani kuwaringishia washindani waoHii bank niliachana nayo nilipomalizana na bumu la chuo. Hivi kweli unaenda kupanga foleni kuhakiki taarifa zako kwenye bank ya NMB kwenye nchi yenye banks lukuki?
Vijana wa siku hizi hamna ubunifu enzi zetu tulikuwa tunaweka mawe kama foleni kusubiri unga wa Yanga national milling na kwenye kusubiri sukari utafikiri unapewa bure then unaenda kupiga mishe jiwe linakuwa linasogezwa tu no kupoteza muda ukirudi unakuta jiwe lipo namba 2 unakaa dk 2 unahudumiwa unaenda sasa ninyi mnashinda Nyerere squareZoezi la uhakiki wa taarifa bank ya NMB ni kero kwakweli, foleni ni ndefu kila branch, watendaji hawajipanga, inchukua hadi dk 20 kwa mtu mmoja kuhudumiwa na wahudumu kwa kila branch ni mmoja.
Mara waseme mtandao unasumbua kwahyo mshine inachelewa.
Nimezunguka NMB branch zote Dodoma, msururu wa foleni ni mrefu, uwe umekula umeshiba n uwe n nguvu za kusimama ili kusibiri foleni yako ifike.
Wajipange upya na waongeze muda wa zoezi.
Niliwauliza why mnafanya hivi wakasema moja ya kitu hawataki ni kuchukuliana fedha kwenye mashine hivyo soon wataondoa PIN ibaki FPBongo kila siku ni kuchukuliwa finger prints, kila sehemu halafu unaambiwa ni kuhakikisha namba ya nida, sasa finger prints za nini wakati ziko Nida?
Walipaswa watumie watu link waingie kuhakiki taarifa zao, nilienda branch 2 nikakuta ni ujinga kama huo nikaachana na hiyo biashara. Nimeona wamwongeza muda ila sitaenda pia.
Haiwezekani ulimwengu wa sasa unataka niende branch physically?
Au MstaafuHii bank niliachana nayo nilipomalizana na bumu la chuo. Hivi kweli unaenda kupanga foleni kuhakiki taarifa zako kwenye bank ya NMB kwenye nchi yenye banks lukuki?
Reality is: Hii bank inawachukulia powa. Maybe inajua kila customer ni mwalimu na nesi au mfanyakazi wa halmashauri Mpwayungu Village.
Mashine zao zote zina FP Option ama watabadili walete mpya?Niliwauliza why mnafanya hivi wakasema moja ya kitu hawataki ni kuchukuliana fedha kwenye mashine hivyo soon wataondoa PIN ibaki FP
π€£π€£Nimejaribu kwenda mara kadhaa, Mlimani city branch, Sinza, U/Plaza na pale UDSM, foleni haivumiliki. Nikaishia kujiondokea mara zote.
Nangoja wafunge hiyo account ili tujue kama wao ni benki ya biashara au ofisi ya serikali. Kama wao ni benki ya biashara basi wajue benki ziko nyingi, sioni shida kihamia hata Azania Bank!!
Maana kwa namna walivyoendesha hili zoezi lao la kujinga ni kama wanashindana na taasisi kama NIDA, TANESCO, Ardhi na nyinginezo kwenye kusumbua wananchi kwa huduma mbovu.
π€£π€£Mbona tunashangaa?ππππ Hii nchi!
Kuhakiki taarifa mteja anatakiwa akapange foleni bank???
Nitahamia hukoKuna benki inaitwa Equity hawa jamaa wako mbele sana ya muda hasa hasa upande wa teknolojia nakumbuka kuna wakati nilpata changamoto ya kadi yangu hasa hasa kuhusu kuhuisha taarifa sikulazimika kufika kwenye tawi lao mambo yote yalifanyika online tu, Nilitamani hata niwape ya soda.
NMB sio vibaya mkaenda kupata semina elekezi pale Equity ili kusudi mjiimarishe kiteknolojia zama za kupanga foleni ndefuuu kupata huduma ni ushamba sana
Equity ni wakenya huwezi linganisha na watanzania hata siku moja,jamaa wapo mbali sana.NMB na CRDB ni bank za waswahili, zinaendeshwa kiswahili sana.
Hamia Equity Bank au ABSA Bank, utakuja kunishukuru.
kama mkoa ulipo hakuna equity, hamia hata NBC Bank
π inashangaza sana shemeji.ππππ Hii nchi!
Kuhakiki taarifa mteja anatakiwa akapange foleni bank???
Hapa tutarudi tarehe 27.09.2024 π