Zoezi la uvaaji barakoa kwenye vyombo vya usafiri linazingatiwa huko ulipo?

Zoezi la uvaaji barakoa kwenye vyombo vya usafiri linazingatiwa huko ulipo?

Crimea

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Posts
25,874
Reaction score
36,030
Wakuu kufuatia tangazo la Serikali kwamba marufuku mtu kupanda kwenye chombo cha usafiri bila barakoa, vipi linazingatiwa huko ulipo?

Mimi huku daladala za Gongo la Mboto hamna kitu, maisha ni kama zamani tu.
 
Wakuu kufautia tangazo la Serikali kwamba marufuku mtu kupanda kwenye chombo cha usafiri bila barakoa, vipi linazingatiwa huko uliko?

Mimi huku daladala za Gongo la Mboto hamna kitu, maisha ni kama zamani tu.
Kwa matamko yasiyo serious kama haya ya Waziri Gwajima na nyongeza ya maneno ya kejeli ya kaka yake wa kufikia Askofu Gwajima usitegemee la maana kwa sasa. Maisha ni yako na wachangiaji makini wa JF bado tunakuhtaji utuchallenge na tukuchallenge, hivyo VAA BARAKOA.
 
Watanzani wana roho ngumu, hawaogopi kabisa kufa. We fikiria tu tunavyokana bila zana huku mtaani yaani! Kama hamna ugonjwa wowote!
Kwani ni corona tu inaua??? Msitishe watu bhana, mbona watu wanakufa kila siku na ajali, na magonjwa mengine, mbona mnaikuza sana corona??? Mm na familia yangu nilishaawambia hamna cha barakoa wala chanjo hapa!! YESU muumba mbingu na nchi aliyetuvusha 2020 ataendelea kutulinda hata leo
 
Kwa matamko yasiyo serious kama haya ya Waziri Gwajima na nyongeza ya maneno ya kejeli ya kaka yake wa kufikia Askofu Gwajima usitegemee la maana kwa sasa. Maisha ni yako na wachangiaji makini wa JF bado tunakuhtaji utuchallenge na tukuchallenge, hivyo VAA BARAKOA.
Barakoa!! Jana pale Kigoma mashabiki walivaa barakoa?? Mimi hata barakoa sina mpango wa kuvaa.
 
Yaani ni janga. Kwenye vyombo vya usafiri hakuna anayejali kuvaa barakoa

Kinachotokea ni kwamba kila mmoja anayo mfukoni lakini sijui ni kuona aibu au kutoona umuhimu, au kutokuwa na imani kama kweli unaweza ambukizwa... hapa inachanganya kwa kweli;

Juzi tu nilipanda mwendokasi, barakoa yangu mfukoni, nimetokea mbezi... kufika ubungo basi limejaa kichizi akaingia mtu mmoja anakohoa sana sana... watu tukaaanza kuangaliana kama vile tunaulizana ; "kuna usalama hapa".... yule mtu alivyozidi kukohoa sana pamoja na kwamba alikuwa anajizuia kwa mikono lakini mmmmm ..... kila mtu aliogopa.... nikaona isiwe tabu nikatoa barakoa yangu nikavaaa.... kile kitendo cha kutoa barakoa na kuvaa nikashangaa basi zima kila mtu anatafuta barakoa yake! wengine kwenye mapochi wengine mfukoni .... ndani ya dakika moja basi karibu lote watu walivaa barakoa.... nilicheka kwa sauti ... maana dah.... basi zima tulicheka! kimya kikapita....

Sasa bado najiuliza tuna nini watanzania??!!!!
 
Hapana
Huku kwetu sidhani kama kuna mtu mwenye hiyo taarifa maana hakuna utekelezaji
 
Wakuu kufautia tangazo la Serikali kwamba marufuku mtu kupanda kwenye chombo cha usafiri bila barakoa, vipi linazingatiwa huko uliko?

Mimi huku daladala za Gongo la Mboto hamna kitu, maisha ni kama zamani tu.
Hayo ni matamko kuonesha tunafuata matamshi ya watoa misaada. Wewe amua mwenyewe kama unaona barakoa ni muhimu kwako.
 
Kwani ilikuwa ni lazima kuvaa barakoa au ni hiari?
 
Watanzani wana roho ngumu, hawaogopi kabisa kufa. We fikiria tu tunavyokana bila zana huku mtaani yaani! Kama hamna ugonjwa wowote!

If you don't read the newspaper, you're uninformed. If you read the newspaper, you're mis-informed.​

Back
Top Bottom