SAGAI GALGANO
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 47,706
- 69,281
I cant imagine ni mawazo ya kiasi gani yanapita kwenye kichwa cha SP Bageni muda huu
Kila akifumba macho anamuona Iddi Amin akimnyooshea mkono kumkaribisha makao mapya
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
I cant imagine ni mawazo ya kiasi gani yanapita kwenye kichwa cha SP Bageni muda huu
sisi wakazi wa mji wetu tunajuana vizuri ,
Umenena vyema ila hawazingatii matokeo kama hayaPole Sana kwa aliyehukumiwa kunyongwa lakini haya ndiyo matunda ya kufanya kazi kwa kutaka kuwafurahisha baadhi ya watu ambao baadaye mambo yanapokuwa magumu wanakuruka.
Ndo maana tunaelezwa kuwa akili za kuambiwa changanya na zako...Pole Sana kwa aliyehukumiwa kunyongwa lakini haya ndiyo matunda ya kufanya kazi kwa kutaka kuwafurahisha baadhi ya watu ambao baadaye mambo yanapokuwa magumu wanakuruka.
Mahakama ya Rufaa imemhukumu aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni, Christopher Bageni kunyongwa hadi kufa katika kesi ya vifo vya wafanyabiashara wa madini iliyokuwa ikimkabili yeye pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi Abdallah Zombe na maofisa wenzake wawili.
Katika hukumu hiyo, Zombe na maafisa wengine wawili wameachiwa baada ya kushinda rufani hiyo dhidi yao.
Hukumu hiyo imehitimisha mvutano wa muda mrefu wa kisheria kati ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na maofisa hao kwani baada ya kimya kirefu hukumu hiyo imetolewa.
Watuhumiwa wengine katika kesi hiyo walikuwa ni, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Kituo cha Polisi Urafiki, Mratibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Ahmed Makelle na Rajabu Bakari.
Hukumu hiyo imekuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu, wakiwamo ndugu wa marehemu hao, wanasheria na jamii kwa jumla baada ya miezi minne, majuma mawili na siku mbili, tangu rufaa iliposikilizwa.
DPP alikata rufaa akipinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyowaachia huru Zombe na wenzake wanane katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wawili wa madini kutoka Mahenge, Morogoro na dereva wa teksi, mkazi wa Dar es Salaam.
Katika kesi ya msingi, Zombe na wenzake walidaiwa kuwaua kwa kukusudia wafanyabiashara Sabinus Chigumbi, maarufu Jongo na ndugu yake, Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na Juma Ndugu, aliyekuwa dereva wa teksi wa Manzese.
Walidaiwa kutenda makosa hayo Januari 14, mwaka 2006, katika msitu wa Pande, uliopo wilayani Kinondoni baada ya kuwakamata wafanyabiashara hao Sinza, walipokuja Dar es Salaam kuuza madini.
Agosti 17, 2009, Mahakama Kuu iliwaachia huru washtakiwa hao ikisema baada ya kusikiliza ushahidi na hoja za mawakili wa pande zote iliridhika kuwa hawakuwa na hatia ya mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili.
Badala ya kosa la mauaji ambalo adhabu yake ni kunyongwa hadi kufaa, DPP aliiomba Mahakama imtie hatiani Zombe kwa kosa la kuwalinda wahalifu, ambao adhabu yake ni kifungo kisichozidi miaka saba jela.
Wakili wa Serikali Mkuu (PSA), Timon Vitalis alidai DPP alifikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa hakuna ushahidi wa kumtia hatiani Zombe kwa kosa la mauaji.
Chanzo: HiviSasa Blog
Kilichomsaidia Zombe ni kukubali kufuta kesi ya kudai fidia kutokana na hukumu ya awali. State made a deal with him wakampa option moja kati ya mbili kabla hukumu ya rufaa haijatoka. Either rufaa imkute na hatia aende jela or akubali kudrop off madai ya fidia yale ya billions dhidi ya state.... You don't need a degree kuona kuwa alikuwa na hatia kabisa.
Nimewaza tu
Du, Bageni kijana mdogo aliyekuwa anainukia.I cant imagine ni mawazo ya kiasi gani yanapita kwenye kichwa cha SP Bageni muda huu
Ni watu wangapi hawakutendewa haki na judiciary (courts of law) katika taifa hili masikini!!!! Ni wangapi wamefungwa kwa hila na kukosa uwezo wa kiuchumi!!! Nenda mahabusu/jela kafanye utafiti then leta mrejesho.This is a serious allegation, kama huna uhakika ifute. Ni insult kubwa kwa judiciary. Meaning kwamba haki haikutendtka na aliyehukumiwa kunyongwa ni maonevu.
Ni watu wangapi hawakutendewa haki na judiciary (courts of law) katika taifa hili masikini!!!! Ni wangapi wamefungwa kwa hila na kukosa uwezo wa kiuchumi!!! Nenda mahabusu/jela kafanye utafiti then leta mrejesho.
Nawaza....
I reserve my comment. Let's end up here for the sake of the ”system".Nakubaliana na contention yako. Lkn for Zombe case you can not say for sure kuwa haki haikutendeka kuwa alipewa options mbili na mahakama ikaangukia kwenye options hizo.
I reserve my comment. Let's end up here for the sake of the ”system".