Zuchu afungiwa kujihusisha na shughuli za sanaa Zanzibar

Zuchu afungiwa kujihusisha na shughuli za sanaa Zanzibar


Baraza la Sanaa, Sensa, Filamu na Utamaduni la Zanzibar, limemfungia msaanii wa kizazi kipya Zuhura Othman Masoud maarufu Zuchu kuendesha shughuli zote za sanaa visiwani Zanzibar.

Mbali na kumfungia kuendesha shughuli za sanaa, pia imepiga marufuku redio na televisheni za Zanzibar kupiga nyimbo zake zote kwa kipindi cha miezi sita.

Hatua hiyo imekuja baada ya tukio la Februari 24 mwaka huu Zuchu wakati akitumbuiza katika usiku wa Fullmoon Kendwa Mkoa wa Kaskazini Unguja kudaiwa kuimba nyimbo, kutoa matamshi na kuonyesha ishara mbaya ambazo ni kinyume na maadili ya kizanzibari.

Akizungumza leo Machi 5, 2024 ofisini kwake na waandishi wa habari, katibu mtendaji wa baraza hilo, Omar Abdalla Adam amesema baraza limemfungia kwa kipindi cha miezi sita kuanzia sasa.

“Baraza lina wajibu wa kusimamia mila, silka desturi na utamaduni wa Mzanzibari, kwa hiyo linatamka rasmi kumfungia msanii Zuhura Othman Soud (Zuchu) kufanya shughuli yoyote ya sanaa kwa Zanzibar kwa kipindi cha muda wa miezi sita kuanzia leo Machi 5, 2024,” amesema.

Amesema wanafanya hivyo kutokana na tabia yake kuimba nyimbo ambazo hazina maadili, hazifuati misingi na hazina afya njema kwa jamii ya Wazanzibari.

Pia, amesema licha ya msanii huyo kutokuwa na usajili Zanzibar lakini amekuwa akiendesha shughuli zake za sanaa bila kupata kibali.

Mbali na adhabu hiyo, pia msanii huyo ametakiwa kulipa faini ya Sh1 milioni moja kwa Baraza la Sanaa na aandike barua ya kuomba radhi na kuthibitisha kwamba hatafanya kosa hilo ndani ya kipindi alichofungiwa.


View attachment 2925088
Zuchu hana adabu huyu ni wa kupigwa marufuku maisha yake yote asikanyage ardhi ya zanzibar, anafanya umalaya sana na yule muhuni mwenzake diamond, ni vile kama amelaaniwa ni muhuni sana hana dalili ya uislamu, kusema yeye ni muislamu ni kuudhalilisha uislamu, zuchu sio muislamu halafu nashangaa sana mtu kama Haji manara anapewa microphone msikitini kuongea na waislamu haliyakuwa naye yule jamaa ni malaya mbwa muhuni anaishi kimalaya na mwanamke anayetaka wanastarehe clip za video zinaenea duniani kote
 
LEO AMEFUNGIWA
KESHO YUKO KWENYE MAJUKWAA YA CCM ANATUMBUIZA.

KWA UPANDE MWINGINE,
NI HUKO HUKO KWENYE MASHARTI YA DINI
NI HUKO HUKO KWENYE MATUMIZI YA MIKUND**
NI HUKO HUKO TU.
 
Zanzibar jamani tangu lini kula ushuzi ikawa mwiko? Mbona watu wanazibuana kama wale vijana walofumwa wakitafunana wakawekwa mahabusu Moja na wakaliendeleza libeneke ndani ya mahabusu
 
Freemasons kazini...ataruhusiwa hivi karibuni na ujumbe kashaufikisha...ushoga utaanzia kule ndio utakuja bara baada ya dunia kuelemewa....nimekaa pale yangu macho.
 
TV ya mwanzo africa mashariki ilitizamwa Zanzibar tv za bara kule hazina mpango wowote mnaeka makwaya saa zote na uhuni wa nyimbo za matusi kukaa uchi saa zote
Kwa hyo Zanzibar hawaskilizi clouds FM au wasafi FM?
 
Sub haanallah, ni mtihani haswaa

Waislamu Nyimbo ni haram, mtaenda kujibu nini kwa Allah! Mavazi mnayovaa ni aibu kwa Muislamu jamani, kwanini hatumuogopi Mwenyezi Mungu, life is too jamani tubuni!

Zanzibar, pigeni marufuku wanamuziki kuingia Zanzibar, Zanzibar ni nchi ya kiislamu.

Allah atujaalie mwisho mwema!
 
"Mtamaliza mikao mtamaliza utundu, huyu kwangu haondoki hata mkimpa mku..."

Nimefuatilia vina na mizani pamoja na ushairi Zuchu ana kesi ya kujibu hapa

Na Ile ishara kwenye video pamoja na walivyocheza wacheza show wake anastahili adhabu kali
 
Niliusikia kwa mara ya kwanza huu wimbo mpaka nilishika kichwa. Na anavyopendwa na vitoto vya shule maskini, mtawaambia nini kwa huyu mdada, ilaaaa


Naona sasa hivi wadada ndio imekuwa sound track kwenye video nyingi za wadada wanaojirekodi, hawa nao inaendaje?
 
Back
Top Bottom