Zuhura Yunus aolewa na Fumbuka Ng’wanakilala

Zuhura Yunus aolewa na Fumbuka Ng’wanakilala

Yah sisi ni watu wa hovyo sana ndoa ni jambo la heri lakini ajabu comments nyingi ni za kumsema dada wa watu
Akili ndogo hujadili watu!

Akili ya kati hujadili matukio!

Akili kubwa hujadili "ideas"

Nafikiri umeshajua sababu.
 
Ni hatari sana kuishi kwenye jamii kama hii ya watu kama hawa........

Yaani mpaka nafsi yangu imepata woga jinsi ya kuwatazama watu huko barabarani........

Comments za huku zinasikitisha sana kama sio kuhudhunisha.....

Jamii inaelekea kubaya sana kama sio imeshaelekea kubaya.......

Hizi roho ndio zipo mitaani tunamoishi na maofisini tunakotafutia ridhiki....ni hatari sana.....

Jamii imejaa majungu, chuki, fitina, umbea na roho mbaya mpaka unashangaa huyu aliyeandika hapa ni binadamu au ni shetani........!!!

Hii mitandao ya kijamii na fake I'ds zinatufunilia sana uhalisia wa namna Gani jamii zetu Zina watu wenye roho mbaya mithili ya nyoka mwenye sumu kali.........

Yaani mtu humjui na wala hakujui, kaamua kuachana na njia mbaya na kufanya jambo la kheri lakini bado watu baada ya kumtakia kheri wanamuombea mabaya........

Wengine wanasema kuchelewa, wengine wanasema hatazaa tena, wengine utasikia alikuwa msagaji, wengine kaolewa kuondoa aibu, wengine utasikia kijana kafuata fedha yaani ili mradi majungu , fitina na kushindwa kuificha roho mbaya.......tunaenda wapi wanadamu.........

Sentensi ndogo tu ya kumtakia mtu kheri inakushinda mtu mpaka unalaani kana kwamba mtu mna ugomvi naye..........

Ndio maana miaka ya kuishi imepungua sana....mizigo ya chuki ,majungu, roho mbaya, na fitina tuliyoibeba vifuani mwetu vinatuangamiza sana......yaani mtu unaumia kwa neema au baraka za kiumbe mwenzio mpaka unalaani.....???
Watu wengi ni "wachawi" japo hawajifahamu kuwa ni wachawi.
 
Zuhura habadiliki....enzi hizo kanaandaa matamasha
Anakusisitiza mnunue ticket

Ova
 
Sikuwa nafahamu kuwa Zuhura Yunus kaolewa. Nimefahamu leo nilipokuwa nikiisikiliza clip ya Makongoro Nyerere.

Nimefurahi kusikia hilo. Hongera zao.
 
Nimeshangazwa na kusikitishwa na comments za baadhi ya wachangiaji kwenye huu uzi. Sijui kama ni chuki, wivu, ubinafsi au utoto!

Kuna waliocomment kwa kukejeli!

Wengine wameonekana kama wamekasirika!

Lakini kuna wachache waliofurahi kufahamu kuwa Zuhura kapata mume.

Nini kilichowakwaza waliokasirika?

Hawakutaka Zuhura aolewe?

Ikiwa Zuhura kaona ni jambo jema, na ndugu zake wakaridhia, na wanaomtakianmema wakafurahia, na yumkini hata mama Samia naye alifurahia, hao wanaomkejeli wanamtakia nini?

Wanajua kumzidi Zuhura Yunusu?

Zuhura ni mtu mzima na mwelewa. Yeye ndiye anayefahamu kilicho bora kwake. Aachwe aifurahie ndoa yake kwa kadiri awezavyo.

Hajavunja Sheria za nchi wala za imani yake wala ya familia yake. Ni haki yake! Ni maisha yake! Aachwe ayafurahie.
 
Kwenye maisha, usihangaike wala kuzingatia sana walimwengu, hawana jema.

Watu wana asili ya roho mbaya, hata yule anaeonekana anakuchekea, usishangae hali haiko hivyo moyoni, si kila mtu anafurahia mafanikio yako.
 
Back
Top Bottom