Zuhura Yunus kudai uteuzi wake ulikuwa wa kushtukiza, hakuwa na taarifa ni kweli? Kwanini hakujuzwa?

Zuhura Yunus kudai uteuzi wake ulikuwa wa kushtukiza, hakuwa na taarifa ni kweli? Kwanini hakujuzwa?

Sidhani kama nikweli cos tayari alishaaga BBC.......alijua anakoenda bila shaka
Tanzania kila mtu akichaguliwa huwa anadai hakujua. Mpaka Vice President. Kama ni kweli basi huo ni utamaduni mbaya. Lakini kwa yeye kujiuzuru ina maana tayari alishajua. Unless anazungumza watu wa ndani ndiyo waliompigia simu.

Halafu haiwezekani akaondoka kwenye shirika kubwa kama BBC kwa shirt notice. Probably, Alisharesign a month or three months ago.
 
Nyerere miaka yake yote ya Utawala Personal Secretary wake alikuwa Mdada mrembo wa Kiingereza hadi alipostaafu bado aliendelea nae…

cha kushangaza zaid yule Bibi aliandika kitabu cha Maisha yake na mengi kuhusu uhusiano wake wa 'kikazi' na Kambarage na akaomba kizunduliwe 30 years baada ya kufa kwake…wachambuzi wana bashiri kina mengi sana
Joan Wicken.
 
Joan Wicken.Ndiye aliyemsaidia kuanzisha chuo cha Kivukoni college. Mama huyo alikuwa ni MJAMAA/Socialist usiseme. Alizunguka nchi nzima akichangisha michango ili apate hela ya mambo ya Elimu. Iwe ni mbuzi, kuku, Ng'ombe ama Bata zote alipewa alisimamia. Tanganyika Education Trust/Foundation
 
Wenzetu huko Duniani utaskia Rais anategemewa kumteua Fulani kuwa fulani…hii inasaidia Mhusika kujiandaa kisaikolojia na wakati mwingine watu kutoa taarifa zake muhimu kabla ya Uteuzi

Nimewahi kumsikia Fedrick Sumaye kuwa aliitwa saa 9 kamili jion kwny Makazi ya Rais wakati huo Mpambe wa Rais alikuwa kishaelekea Bungen kwa Mzee Msekwa kupeleka jina

The same to Mzee Pinda anasema akiwa na Rafiki yake Mh.Paul Kimiti wanajadili nani atamrithi Lowassa akashangaa Gari za 'Kaunda suti' zinakuja kumbeba

Tabia hii iliwahi kumgharimu jamaa aliekataa uteuzi wakati wa Mwamba bwana Maendeleo akajikuta kapoteza kazi Tigo

Hayati Mzee wetu yeye alikuja na kali kuliko…anatumbua Jumapili usiku hadi nguo za kazini ushaandaa
Ni kweli wenzetu duniani wanafanya hivyo, nadhani ni sababu ya ukubwa wao, nguvu na mifumo yao ilivyo imara. Sasa fikiria udogo wetu huu ulivyo ktk nyanja zote halafu mtu yupo Ulaya uanze kusema Fulani anatarajiwa kuteuliwa kuwa ......

Hizi Surprise ni Muhimu kwa Maslahi Mapana
 
Inawezekana aliahidiwa kuwa kuna uteuzi unatakuja kwake lakini hakujua wapi hasingeweza kuondoka BBC hivi hivi tu bila uhakika wa ajira mpya nzuri zaidi
Hiyo "h" ya Nini kwenye neno "hasingeweza"?

Kiukweli huwa naboreka sana na watu wanaoshindwa kutifautisha na kujua matumizi ya hayo maneno.

Kuna jamaa mmoja naye ana ujinga kama huo huwa ananikera sana!!

Hebu jifunzeni kiswahili bhana mnatudhalilisha aaaalaaaaaaaaaaaah

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Wenzetu huko Duniani utaskia Rais anategemewa kumteua Fulani kuwa fulani…hii inasaidia Mhusika kujiandaa kisaikolojia na wakati mwingine watu kutoa taarifa zake muhimu kabla ya Uteuzi

Nimewahi kumsikia Fedrick Sumaye kuwa aliitwa saa 9 kamili jion kwny Makazi ya Rais wakati huo Mpambe wa Rais alikuwa kishaelekea Bungen kwa Mzee Msekwa kupeleka jina

The same to Mzee Pinda anasema akiwa na Rafiki yake Mh.Paul Kimiti wanajadili nani atamrithi Lowassa akashangaa Gari za 'Kaunda suti' zinakuja kumbeba

Tabia hii iliwahi kumgharimu jamaa aliekataa uteuzi wakati wa Mwamba bwana Maendeleo akajikuta kapoteza kazi Tigo

Hayati Mzee wetu yeye alikuja na kali kuliko…anatumbua Jumapili usiku hadi nguo za kazini ushaandaa
Umenena vyema.
 
Nyerere miaka yake yote ya Utawala Personal Secretary wake alikuwa Mdada mrembo wa Kiingereza hadi alipostaafu bado aliendelea nae…

cha kushangaza zaid yule Bibi aliandika kitabu cha Maisha yake na mengi kuhusu uhusiano wake wa 'kikazi' na Kambarage na akaomba kizunduliwe 30 years baada ya kufa kwake…wachambuzi wana bashiri kina mengi sana
Is she still with us?
 
Kuna ukakakasi.
Je, mteuaji ni kichaa?
Je, mteule angekataa uteuzi huku umeshaweka jambo public inakuwaje?
Kuna usanii hapa
 
Huyu hasitufanye sisi wote watoto,aliachaje kazi BBC kama alikuwa hajui kinachoendelea. Sema ajue Tanzania ni kugumu. Wenzake waliomtangulia kutoka BBC na kuteuliwa kuwa wasemaji wa ikulu ni marehemu Afsa Mosi(Burundi) na Lubunga Boaombe (DRC).
 
Huyu mama hasemi ukweli mbona mimi nilisoma mahali tangu December, 2020 wakati ametoa notice ya kuacha kazi BBC walisema amepewa kazi na SSH sasa leo anasema alistukizwa sio kweli
Umepoteza kumbukumbu kamanda, SSH alikuwa hana mamlaka ya kuahidi au kutoa kazi 2020 alikuwa ni mshauri tu
 
Hapa JK alidanganya waziwazi.
Inawezekana utawala wa JPM ulikuwa na mambo ya kitoto mengi sana.

Mojawapo ni wananchi kutopewa taarifa kama rais wa nchi ni mgonjwa wanakuja kupewa taarifa ya kifo tu tena usiku wa manane.
 
Usiamini kila jambo, asilimia kubwa ya mambo hapa duniani ni "fake",ni hadaa, hizo ni fiksi tupu ndugu yangu, huyo aliandaliwa ndio maana akajistahafisha.
 
Back
Top Bottom