Zuio la mahindi kwenda Kenya tusiwatupie lawama Wakenya. Nchi yao inayo haki kulinda raia wake

Zuio la mahindi kwenda Kenya tusiwatupie lawama Wakenya. Nchi yao inayo haki kulinda raia wake

Mlipowachomea moto vifaranga wao na kupiga mnada ng'ombe wao mliowakamata viongozi walimtegemea Mungu? Ni Chadema walishauri mfanye hivyo? Pili je tokea hii taarifa itoke wanasayansi wetu wametoa taarifa yoyote ya kiutafiti kuonyesha kwamba mahindi yetu hayana hiyo mycotoxins?? Je hapa nchini tunao utaratibu wa kupima mahindi yetu kujua status ya mycotoxins??
 
Ni wakati muafaka sasa Mipaka ya hawa jirani zetu ifungwe km alivyofanya Mwl. Wabaki na yao na sisi tubaki na yetu
 
Biashara za kimataifa hazifanyi kinyama hivyo, huwezi kukurupuka tena kwa nchi unayoitegemea kiuchumi ukata waya kama vile haitakuathiri pia. Walikuwa na muda wa kuongea na balozi au hata serikali. Inawezekanaje wakulima wa Watanzania na Wauganda ghafla washinwe kulinda mazao yao? Kwani wameanza kuuza mazao yao nje leo? Ni muda wa sisi kuvaa mawani ya mbao
Unao uhakika kwamba kwenye vikao vyao vya kazi hawajawahi kuzungumzia hilo? Wewe ambacho umeshudia ni katazo la Kenya but huna uhakika wa official correspondences kwani ni vikao vya siri.
 
Kabla ya kuchukuwa maamuzi haya kwanini mawaziri wa pande zote mbili hawakuitana kuangalia jinsi ya kutatua suala hili au jinsi ya kurekebisha tatizo hili 'JAMAA WAMEFANYA UHUNI MBAYA SANA"kwanza bidhaa zao nyingi hazina uhalisia halisi wa zao husika wakikwambia haya ni maziwa 100% full cream ujue ni 15% na 85% ni unga wa mihogo
Si TBS wapo?
 
Kabla ya kuchukuwa maamuzi haya kwanini mawaziri wa pande zote mbili hawakuitana kuangalia jinsi ya kutatua suala hili au jinsi ya kurekebisha tatizo hili 'JAMAA WAMEFANYA UHUNI MBAYA SANA"kwanza bidhaa zao nyingi hazina uhalisia halisi wa zao husika wakikwambia haya ni maziwa 100% full cream ujue ni 15% na 85% ni unga wa mihogo
Mnamimina Omo simchezo

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Watanzania ni viumbe special na tunajiona tunahaki zaidi ya mtu yeyote hapa duniani,Sasa jeuri hii sijui inatokana na sisi kuongozwa na kiongozi wa malaika mtarajiwa? Sijui
 
watu wamejikita katika kushangaa huo uamuzi.sio kulaumu uamuzi huo.

hii ni sawa na umelelewa mama yako mpaka unakua,kisha unamshutumu uchawi,haijalishi ni kweli anakuroga au vipi ila hutaeleweka.
 
Huu ndo ujinga tulionao, badala ya kutafuta kiini cha tatizo na kukitatua wewe unanyooshea wenzio vidole. Hii tabia ya kujifanya kuwa ninyi ndio wazalendo zaidi ndo imetufikisha hapa
 
Ni sawa kabisa na sisi tulivyozuia chanjo za Covd19 au barakola za kutoka nje ya nchi zilizowekewa virusi. Wakenya wapo sahihi
 
Maneno mengi point kusoda na kuwalaum wanachadema. Kwahiyo Mungu aliumba Tanzania tu, kukaaa Tanzania peke yake?
 
Well said mkuu [emoji120] [emoji120] Mimi nalima sana mahindi, kiukweli changamoto kubwa ya mahindi ni namna ya kuyahifadhi maana yanabunguliwa haraka sana, na wakulima wengi wanapovuna bei huwa chini sanaaaaa, yaani sometimes mpaka elfu 30 au 35 kwa gunia, wakati production costs yaweza kuwa elfu 40.

So solution ni kuyapiga dawa na kuweka ghalani ukisubiria bei ichangamke kidogo. Sasa kama ulivyosema, kukosekana kwa wataalam wa kilimo, hasa ngazi ya kila kijiji, kumefanya wakulima kutumia hovyo au bila utaalamu wa kutosha hizi dawa za kuhifadhi mahindi.

Kuna maajenti pia hupita huko vijijini na kutumia fursa hiyo kusambaza madawa bila uratibu mzuri wa serikali. Hapa ndipo madawa yasiyofaa yanapotumika maana mtu anataka aweke dawa ambayo mahindi hayatabunguliwa hata yakikaa ghalani kwa miezi 6 ili aweze kuyauza na kupata bei nzuri. Sasa kama kweli haya madawa yanachangia kwenye kuleta sumu ya mycotoxins then this is very serious problem.

Mimi shambani kwangu mahindi ya kula nyumbani kwangu kamwe siweki hizi dawa, nahifadhi kwenye ile mifuko maalumu au air tight containers. Yaani hizi dawa unapopiga kwenye mahindi ili uyaweke ghalani lazima ufunge kitambaa na mask juu kuziba pua na mdomo, ni kali sana.
 
Wangeanza na kuondoa sembe yote iliyo madukani na kuwaambia watu wamwage na wasile sembe iliyotoka Tanzania au Uganda. Lakini mpaka muda huu, bado kuna sembe madukani Kenya na majumbani kwa watu iliyotokana na mahindi hayo hayo yanayosemwa yana sumu.
Kenya kwa muda sasa wanaagiza mahindi from Mexico, hata DRC nao wanaagiza kutoka huko, wanasema huko bei ni cheaper...
 
Nimependa hoja yako, pia serikali yetu idhibiti matumizi mabaya ya hayo madawa kwakuwa case za cancer zinaongezeka kwa kasi mwisho wa siku sisi tutapukutika na hao wakenya watakuja kuishi huku
 
Acha upuuzi, unga huohuo tunakula watanzania. Nenda Ocean Road kaulize kansa ipi inaongoza na kama ina uhusiano wowote na hizo sumu za Unga.
Hiii ni very technical issue, je kuna any report or survey iliyofanywa na wataalamu wetu kuonyesha madhara ya sumu ya mycotoxins ya kwenye mahindi? Kumbuka mahindi yanahifadhiwa kwa zile dawa ambapo hata panya hasogei hapo, kuna any university hapa nchini au wataalam kutoka other research centers waliofanya detail study ya hizi sumu za kuhifadhia mahindi?? Kumbuka pia sumu from mycotoxins huuwa slowly..
 
At least wewe umeongea point. Kuna wapuuzi wao washa'conclude kweli mahindi yana sumu wakisahau ugali wanaokula hawajalima wao hayo mahindi.
Mkuu labda wewe ndo hujui na kwa hali hiyo hata uchukui tahadhari,Ila watu wote wenye Akili timamu nchi hii huwezi kuwakuta wakifakamia ugali hasa wa Dona ambao hawajui utayarishiwa wapi? Na ni kutokana na hiyo awareness ndo maana hata TBS iliset standard ya acceptable aflotoxins level kwenye vyakula vyetu vya nafaka na mafuta
 
Nimependa hoja yako, pia serikali yetu idhibiti matumizi mabaya ya hayo madawa kwakuwa case za cancer zinaongezeka kwa kasi mwisho wa siku sisi tutapukutika na hao wakenya watakuja kuishi huku
Mkuu siyo matumizi ya madawa bali ni fungus zinazokuwa developed kutokana na wakulima kushindwa kuadhere to Good agricultural practices.kumbuka tatizo hili pia lipo kwenye karanga na mazoa mengine.mfano pale unapotafuna karanga ukakuta inaukakasi au something like imevunda,jua hiyo umetafuna aflatoxins mazee
 
Ona unavyoharisha kupitia tundu la mdomo!
 
Hawa watu wataendelea na chuki na serikali ya Nchi hii na sababu ni kuibiwa kwa kura, wanaamini ingekuwa serikali yao haya yasingetokea, na serikali mbili zingeweza ongea kutatua shida hii, na si kama walivyofanya
 
Back
Top Bottom