Zuio la mahindi kwenda Kenya tusiwatupie lawama Wakenya. Nchi yao inayo haki kulinda raia wake

Zuio la mahindi kwenda Kenya tusiwatupie lawama Wakenya. Nchi yao inayo haki kulinda raia wake

Mbona Tz ilichoma vifaranga na nyavu za uvuvi za Kenya je haya hayakuwa mambo ya kinyama, je Tz haikuwa na muda wa kuongea na balozi wa Tz/Serikali??
Hivyo vifaranga vilichomwa ndani ya ardhi ya Kenya au ardhi ya Tanzania? Kenya walishalipwa pesa hao inamana hivyo vifaranga sio mali ya Kenya tena.
 
Hakuna cha utaifa na majizi ya Kura na wamwaga damu. Kama waganda wangeendekeza huu upuuzi unaoita utaifa, wangesimama upande wa Iddy Amini wakati wa Vita vya Uganda. Hakuna cha umoja wa kitaifa na majizi ya kura, na kwa taarifa yako wakija maadui tutawaunga mkono mpaka mjue kutenda haki fullstop. Haki huinua taifa.
 
Kabla ya kuchukuwa maamuzi haya kwanini mawaziri wa pande zote mbili hawakuitana kuangalia jinsi ya kutatua suala hili au jinsi ya kurekebisha tatizo hili 'JAMAA WAMEFANYA UHUNI MBAYA SANA"kwanza bidhaa zao nyingi hazina uhalisia halisi wa zao husika wakikwambia haya ni maziwa 100% full cream ujue ni 15% na 85% ni unga wa mihogo
Wakati mlipochoma vifaranga vyao mawaziri hawakuwepo?
 
Tanzania ikizuia all imports from Kenya kutulinda raia wake tusisikie mnamlalamikia Meko na nyie

Zuieni hata leo, na akizuia tutampa ukweli wake maana bidhaa za Kenya tunanunua kwa hela zetu, na sio kwa mshahara wake.
 
At least wewe umeongea point. Kuna wapuuzi wao washa'conclude kweli mahindi yana sumu wakisahau ugali wanaokula hawajalima wao hayo mahindi.

Yana sumu, bali ni kwakuwa watu hawafanyiwi medical checkup ndio maana hawajui madhara waliyo nayo.
 
Hivyo vifaranga vilichomwa ndani ya ardhi ya Kenya au ardhi ya Tanzania? Kenya walishalipwa pesa hao inamana hivyo vifaranga sio mali ya Kenya tena.
kama hii ilikuwa sawa basi na wao Kenya wasilalamikiwe wanapowalinda wananchi wao dhidi ya mahindi ambayo yanasababisha kansa. Tz ibaki na mahindi yake.
 
kama hii ilikuwa sawa basi na wao Kenya wasilalamikiwe wanapowalinda wananchi wao dhidi ya mahindi ambayo yanasababisha kansa. Tz ibaki na mahindi yake.
Kuna kundi dogo la watanzania wanakuwa wapole sana likija swala la Kenya. Sitaki kuchanganya moja na moja, nitawaachia nyinyi wenyewe.
 
Hawa watu wataendelea na chuki na serikali ya Nchi hii na sababu ni kuibiwa kwa kura, wanaamini ingekuwa serikali yao haya yasingetokea, na serikali mbili zingeweza ongea kutatua shida hii, na si kama walivyofanya

Hilo ni kweli, na chuki yetu dhidi ya serikali ya majizi ya kura iko wazi. Na hatutakaa tuiunge mkono serikali ya majizi ya kura mpaka wajue haki huinua taifa. Tuko tunasubiri na kuombea mambaya dhidi ya serikali hii ya majizi ya kura.
 
Hongera kwa hili somo maana wengi hawajui.
 
Kuna kundi dogo la watanzania wanakuwa wapole sana likija swala la Kenya. Sitaki kuchanganya moja na moja, nitawaachia nyinyi wenyewe.
Ni kweli watu wanataka kulazimisha na wanalialia mahindi yauzwe Kenya kwani wakulima wakiyala wenyewe watapungukiwa na nini au yakiuzwa Tanzania au nchi zingine kwanza huenda hata yakawa ni kinga dhidi ya changamoto za upumuaji, hivyo yaliwe/kuuzwa Tanzania Kenya wasije wakafaidi bure.
 
Hata mimi nanga mkono hoja yako. Kilichokosewa na Wakenya, ni jinsi walivyotoa taarifa kwa Watanzania. Walitumia mfumo usio sahahihi.
 
Wa Kenya wana hoja ya msingi sana na wamezi umbua mamlaka zetu za viwango yaani TFDA, TBS sijui wizara ya kilimo etc mijitu imekaa maofisi na matumbo yao makubwa badala ya kufanya kazi imekalia kusoma magazeti tuu, wengi tunajua hali ya mahindi ki ukweli zile dawa za kuhifadhia mahindi usalama wake kwa binadamu ni mdogo, hata panya hawali mahindi yaliyo puliziwa hizo ‘ETG’ zenu...
Hatari sana hii sumu inamadhara gani kwa binadamu maana ugali kibongo bongo usipoula mchana utaula jioni hivi tutapona kweli
 
Back
Top Bottom