Zumaridi aiambia Mahakama kuwa Polisi walichukua Tsh. Milioni 19 nyumbani kwake

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Shahidi namba tatu katika kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ya Shambulio la kudhuru mwili Diana Bundala Maarufu kama mfalme Zumaridi ametoa ushahidi wake leo Novemba Mosi, 2022 huku akidai kuwa Askari waliofanya ukaguzi katika nyumba yake wakati akikamatwa walichukua shilingi Milioni 19 na laki tano.

Shahidi huyo ambaye pia ni mtuhumiwa namba moja katika kesi hiyo namba 12 Diana Bundala maarufu Zumaridi amedai kuwa siku hiyo alikuwa akifanya usafi chumbani kwake ndipo maaskari polisi walivunja mlango wa chumba chake hicho na kuanza kufanya upekuzi kisha wakamuondoa chumbani humo na baada ya upekuzi aliporudhishwa akakuta hela zake, hati ya kusafiria pamoja na simu mbili hazipo

Kwa upande wake shahidi namba mbili katika kesi hiyo ajulikanaye kwa jina la Diana Michael ameeleza kuwa wakati anafika nyumbani kwa Zumaridi alikuta Polisi wametanda katika eneo lote la nyumba huku wakivunja milango, mageti na Madirisha ambapo yeye pia alifunikwa na polisi hao kwenye maturubai baada ya kupigwa kwa marungu, Mabomba na Waya.

Baada kusikiliza ushahidi huo Hakimu mkazi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mwanza Clescencia Mushi akaahirisha shauri hilo hadi Novemba 9, 2022 atakaposoma maamuzi ya kesi hiyo.

Shauri hilo dogo ndani ya kesi kubwa namba 12 ilikuja baada ya kuwepo sintofahamu kwenye maelezo yaliyodaiwa na upande wa mashtaka kuwa ni ya Zumaridi ambaye alikana mahakamani hapo hivi karibuni kuwa saini iliyowekwa kwenye maelezo hayo si yake.

Chanzo: EATV
 
Shahidi namba tatu katika kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ya Shambulio la kudhuru mwili Diana Bundala Maarufu kama mfalme Zumaridi ametoa ushahidi wake leo huku akidai kuwa Askari waliofanya ukaguzi katika nyumba yake wakati akikamatwa walichukua shilingi Milioni 19 na laki tano.

Shahidi huyo ambaye pia ni mtuhumiwa namba moja katika kesi hiyo namba 12 Diana Bundala maarufu Zumaridi amedai kuwa siku hiyo alikuwa akifanya usafi chumbani kwake ndipo maaskari polisi walivunja mlango wa chumba chake hicho na kuanza kufanya upekuzi kisha wakamuondoa chumbani humo na baada ya upekuzi aliporudhishwa akakuta hela zake, hati ya kusafiria pamoja na simu mbili hazipo

Kwa upande wake shahidi namba mbili katika kesi hiyo ajulikanaye kwa jina la Diana Michael ameeleza kuwa wakati anafika nyumbani kwa Zumaridi alikuta Polisi wametanda katika eneo lote la nyumba huku wakivunja milango, mageti na Madirisha ambapo yeye pia alifunikwa na polisi hao kwenye maturubai baada ya kupigwa kwa marungu, Mabomba na Waya.

Baada kusikiliza ushahidi huo Hakimu mkazi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mwanza Clescencia Mushi akaahirisha shauri hilo hadi Novemba 9 mwaka huu atakaposoma maamuzi ya kesi hiyo.

Askari polisi wa Tanzania, hamkusikia wosia wa Yesu?

Luka 3:14 BHN​

Nao askari wakamwuliza, “Na sisi tufanye nini?” Naye akawajibu, “Msichukue vitu vya mtu yeyote kwa nguvu wala kumshtaki yeyote kwa uongo. Toshekeni na mishahara yenu.”
 
Back
Top Bottom