Zumaridi aiambia Mahakama kuwa Polisi walichukua Tsh. Milioni 19 nyumbani kwake

Zumaridi aiambia Mahakama kuwa Polisi walichukua Tsh. Milioni 19 nyumbani kwake

Polisi nchi zetu za kiafrika ni watu washenzi sana. Nimeshuhudia South Africa Jozi ukifika usiku polisi wenyewe bila kujali rangi wanageuka kuwa mafia kupitia upolisi wao. Wanajifanya wana ku suspect wakikudaka wanachukua hela na vitu vingine kimafia.
 
Anakaa na cash yote ya nini, bank si IPO.
 
Shahidi namba tatu katika kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ya Shambulio la kudhuru mwili Diana Bundala Maarufu kama mfalme Zumaridi ametoa ushahidi wake leo huku akidai kuwa Askari waliofanya ukaguzi katika nyumba yake wakati akikamatwa walichukua shilingi Milioni 19 na laki tano.

Shahidi huyo ambaye pia ni mtuhumiwa namba moja katika kesi hiyo namba 12 Diana Bundala maarufu Zumaridi amedai kuwa siku hiyo alikuwa akifanya usafi chumbani kwake ndipo maaskari polisi walivunja mlango wa chumba chake hicho na kuanza kufanya upekuzi kisha wakamuondoa chumbani humo na baada ya upekuzi aliporudhishwa akakuta hela zake, hati ya kusafiria pamoja na simu mbili hazipo

Kwa upande wake shahidi namba mbili katika kesi hiyo ajulikanaye kwa jina la Diana Michael ameeleza kuwa wakati anafika nyumbani kwa Zumaridi alikuta Polisi wametanda katika eneo lote la nyumba huku wakivunja milango, mageti na Madirisha ambapo yeye pia alifunikwa na polisi hao kwenye maturubai baada ya kupigwa kwa marungu, Mabomba na Waya.

Baada kusikiliza ushahidi huo Hakimu mkazi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mwanza Clescencia Mushi akaahirisha shauri hilo hadi Novemba 9 mwaka huu atakaposoma maamuzi ya kesi hiyo.

Shauri hilo dogo ndani ya kesi kubwa namba 12 ilikuja baada ya kuwepo sintofahamu kwenye maelezo yaliyodaiwa na upande wa mashtaka kuwa ni ya Zumaridi ambaye alikana mahakamani hapo hivi karibuni kuwa saini iliyowekwa kwenye maelezo hayo si yake.

Chanzo: EATV
Jeshi la Polisi livunjwe
 
Anakaa na cash yote ya nini, bank si IPO.
We nae mbwiga tyu ushawahi kuona watu wanaokaa na cash ndan mil 19 unasema hela nyng nenda nyamongo kaone mtu analala na bilion 6 ndan unashangaa dagaa kummeza sangara?
 
Hizo ni kweli? naona mnatanguliza chuki tu dhidi ya polisi
 
Polisi ni majambazi na wezi waliopewa sare na kulipwa mishahara.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hiyo pesa hawez ipata kamwe labda kama wameamua kupoteza muda tu

Kama unaandikisha vitu vyako ulivyokamatwa navyo mapokezi pale polisi na pesa zikiwemo lakin siku ya kutoka jamaa wanakuambia hukuwa na pesa utaambulia mkanda na viatu tu
 
Back
Top Bottom