JamiiCheck - Tanzania

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Wiki mbili zilizopita kwenye mitandao mbalimbali ilionekana mwendesha bodaboda asiye na woga akiwaacha wengi katika mshangao baada ya kupita kwa utulivu katikati ya kundi simba wenye njaa wanaokula mnyama waliyemuua. Inasemekana baada ya kuwapita Simba, pikipiki yake ilipata hitilafu ambapo alishindwa kuendelea na safari ndipo Simba waliweza kumshambulia na kujipatia kitoweo. Picha ya mwisho iliyobandikwa ilionyesha simba wakiwa wamekaa pembeni ya pikipiki hiyo iliyokuwa imebeba na ndizi, lakini mtu huyo hakupatikana, jambo ambalo liliwashangaza wengi na kuamini kuwa ameliwa na simba hao. VIDEO: Simba wakizunguka pikipiki huku dereva akiwa haonekani. Katika Mtandao wa Twitter, mtumiaji mmoja maarufu kama Mwaisa MtuMbad...
Jamani kichwa kinajieleza. Kwanza ni kweli mende anazalisha maziwa? Mende hawa hawa tunaowaona chooni? Sasa maziwa yenye yanakaa wapi na wanakamuaje? Halafu eti inasemekana maziwa ya mende yanavirutubisho kuliko ya ng'ombe, si makubwa haya! Mende walivyo wachafu na wanavyoogopesha leo mtu ukanywe sijui ule maziwa yake, yaani sitaki hata kupata picha kwakweli. Wakuu hili ni kweli?
Wajumbe, Hili dude la mkataba wa DP World na Serikali ya Tanzania ina makando-kando mengi. Katika kufukunyua nimekutana na wavaa miwani mieusi tena ni PSU. Huyu Bwana amenidokeza kwamba katika uwekezaji huu Rwanda ya Paul Kagame anayo hisa 17% katika kampuni ya DP World na ndiye amekuwa na ushawishi mkubwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan. Katika ziara ya Kagame siku za karibuni ilikuwa ni kukamilisha dili lenyewe. Ikumbukwe Kagame amekuwa na hamu ya kumiliki Bandari ya Dar es salaam kwa miaka mingi akiamini kwamba "tumeshindwa kutumia Bandari ya Dar es salaam kutuletea faida". Hata hivyo, mtoa habari huyo amedai hatua hiyo haijamfurahisha Jakaya Kikwete na ndiye yuko nyuma ya wapinzani wa mkataba huu wa kifedhuli. Paul Kagame, Rais...
Julai 12, 2023, Balozi mstaafu wa Tanzania Nchini Sweden, Dkt. Wilbroad Slaa akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari alitoa kauli inayotuhumu waandishi wa habari kwa kufanya upotoshaji wa matamshi yake kwenye sakata la uwekezaji wa Bandari. Baada ya kauli hii, wadau mbalimbali walianza kutoa maoni yao ambapo jioni ya siku hiyo ilianza kusambaa barua inayodaiwa kutolewa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) ikionesha masikitiko na kulaani kauli za Dkt. Slaa. Barua hiyo ilienda mbali zaidi kwa kumtaka Dkt. Slaa kumba radhi kwa matamshi yake.
Wakuu, Nimekutana na ujumbe unasambaa kwenye mitandao ya kijamii Twitter, Instagram na hata humu JF nimeona mtu kaweka uzi kuwa wanafunzi tena wakike kutoka shule ya wasichana ya Lucas Malia walifungiwa mlango na hivyo kulazimika kulala nje sababu eti walichelewa kufika siku waliyotakiwa kuripoti shuleni. Tukio hilo limetokea Julai 9 na mpaka sasa hawajapolewa wako wanaranda tu mtaani. Wakuu taarifa hii ni ya kweli?
Mdau wa JamiiForums ameweka Chapisho lenye kichwa cha habari "CCM kimeanza kuumana" akimaanisha kuwa hali imeanza kubadilika kwenye Chama cha Mapinduzi baada ya Serikali inayoongozwa na Chama hicho kusaini Mkataba na kampuni ya DP World kuhusu uwekezaji kwenye Bandari ya Dar es Salaam. Hali hii imesababisha kuvunjwa kwa mojawapo ya Ofisi za Chama hicho iliyopo Kinondoni. Ukweli wa suala hili upoje?
Mtumiaji wa Mtandao wa TikTok anayetumia jina la Leonard Clasic (User4692412178624), Julai 3, 2023 mchana, aliweka video moja kwenye ukurasa wake pasipo kufafanua chochote. Video hiyo inamuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akikemea baadhi ya watendaji wa Serikali wanaoingia mikataba mibovu na kusababisha hasara kubwa kwa taifa. Video hii inahusianishwa na Sakata la uwekezaji wa Bandari unaotarajiwa kufanywa na Kampuni ya DP World ya Dubai, imeendelea kusambaa sehemu mbalimbali huku baadhi ya watu wakimpongeza Rais Samia kwa kutoa kauli hiyo.
Juni 15, 2023, Mdau wa JamiiForums aliweka chapisho linaloelezea jinsi alivyokwenda kupata chanjo ya COVID-19 na kupatiwa cheti ya chanjo husika. Mdau huyu anaeleza kuwa alitishwa sana kabla ya kupata chanjo hiyo na wengine walimuomba alipie tu pesa ili apatiwe cheti kama sehemu ya uthibitisho wa kuchanjwa. Katika Mjadala huo, mchangiaji mmoja alisema kuwa Taasisi ya Msalaba Mwekundu (Red Cross) ilikuwa imetoa taarifa inayokataza watu waliochanja kuchangia damu kwa wahitaji. Taarifa hii ni sahihi?
Kumekuwa na debate kubwa kuhusu uchezaji wa Michael Jackson kwenye wimbo wa Smooth Criminal, kuna ile dance aliinama digrii 45 akiwa sakafuni mgongo ukiwa umenyooka, alikaa sekunde kadhaa kabla ya kurudi wima. Wataalamu wa uti wa mgongo wanaonya wengine dhidi ya kujaribu hatua inayoweza kuwadhuru. Wanadai uchezaji wa vile hauwezekani kabisa kwa binadamu yeyote. Wengine wanasema Mfalme huyo wa Pop alikuwa na kipaji kikubwa cha uchezaji hivyo suala lile lilikuwa jambo la kawaida. Wengine wanadai kuwa alivaa viatu vilivyoshikilia sakafu ili kumwezesha kuinama mbele digrii 45. Ukweli ni upi kuhusu 'Smooth Criminal Lean Dance'? VIDEO: Smooth criminal Lean Dance
Salaam Wandugu, Nimepata taarifa mtandaoni kuwa ndege ya Malaysia iliyopotea miaka tisa iliyopita imekutwa kwenye maji ikiwa haina abiria. Habari hiyo ilichapishwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwamo Twitter linaonesha picha ya mbele ya ndege yenye kutu inayosomeka: “Ndege ya Malaysia MH370 iliyotoweka miaka 9 iliyopita imepatikana chini ikiwa haina abiria. Ndege hiyo ilikuwa na abiria 239.” Je, kuna ukweli wowote? Picha inayoenea kwenye mitandao Picha ya ndege ya Lockheed Martin L1011 Tristar kwa upande wa pembeni Source: Deepbluedivecenter Video credit: Deepbluedivecenter
Back
Top Bottom