JamiiCheck - Tanzania

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Kumekuwepo na picha inayozunguka mitandaoni ikimuonesha mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akizungumza na Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho huku mandhari ya nyuma ya picha hiyo yakiwa na picha yenye chupa ya konyagi. Picha inayodaiwa kuwa na chupa ya Konyagi Ukweli wa picha hii upoje? Picha 1 kati ya 4 zilizowekwa na Tundu Lissu kwenye mtandao wa Twitter
Mdau mmoja wa Jamiiforums ameonesha wasiwasi wake baada ya kwenda hospitalini kupima VVU ambapo tofauti na namna alivyotarajia, daktari wake alimpima kwa kutumia mate yaliyotolewa kwenye fizi ya juu na chini. Jambo hili limemfanya atoe ushauri kwa watu kuwa makini wanapokuwa wanabusiana kwa kuwa tendo hilo linaweza kusababisha maambukizi ya VVU kupitia mate. Ukweli wa jambo hili upoje?
Kuna Taarifa zilizosambaa kwenye Mitandao ya Kijamii, zinazodai Tarehe 31 Januari 2023 wakati Tundu Lissu akifanya Mahojiano ya channel ya YouTube ya Jambo TV, kwamba alimpongeza Rais Samia kwa kuunda Tume mpya ya Kuchunguza Haki Jinai. Taarifa hizo ni Uzushi. Uzushi huo ulidai kuwa Tundu Antipas Lissu alisifia kuundwa kwa Tume ya Haki Jinai, hata hivyo, kwa mujibu wa video iliyorekodiwa wakati wa mahojiano hayo Lissu hakupongeza kuundwa kwa tume ya haki jinai wala hakuzungumzia kundwa kwa tume ya haki jinai bali alizungumzia mfumo wa haki jinai kwa kukosoa mfumo huo. Tarehe 31 Januari 2023 Rais Samia alizindua Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai. Rais Samia alisema Tume hiyo imeundwa kutokana na kuvurugika...
Kumekuwepo na madai kuwa Serikali imesitisha Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo baada ya Kushindwana na mwekezaji. Hapo awali Serikali ilifufua mazungumzo na mwekezaji kuhusu ujenzi wa Bandari hiyo ila mazungumzo hayakwenda sawa. Hayo yamesemwa na Waziri Prof. Makame Mbarawa NB. Kwenye suala na negotiation timu ya mama Samia ipo vizuri sana na ipo kwa maslahi ya watanzania wote.
Inadaiwa kuwa mabehewa 30 na vichwa 2 vya treni za SGR mali ya TRC vinapigwa mnada 25/11/2022, nchini Germany kufuatia mgogoro wa TRC na EUROWAGON Railways Limited (Turkey), iliyopewa kazi ya kukarabati na kutia nakshi. TRC wamelipa Sh. 23 bilioni (35% ya kazi). Inadaiwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa EUROWAGON, Yalçın Aydemir amesema wataanza na mnada wa mabehewa 17 ya awali katika mnada huo (hadi sasa wateja wawili wamepatikana kutoka Serbia), na mabehewa 13 na vichwa 2 vya treni za mwendokasi vitasubiri hadi mteja apatikane na kisha watavipiga mnada. Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kampuni ya EUROWAGON ya kutoka Turkey ziliingia makubaliano Oktoba 2020 kwa ajili ya ujenzi (ukarabati na utiaji nakshi) wa vichwa viwili vya treni ya...
Nanasi ni tunda lenye faida lukuki kwa afya. Miongoni mwa faida za tunda hili ni kuongeza kinga ya mwili, kutibu mafua, kupambana na saratani, kuondoa maumivu pamoja na kulinda moyo. Pamoja na uwepo wa faida hizi kwa afya, nanasi huhusishwa na changamoto ya kuharibika kwa ujauzito kwa wanawake, hivyo baadhi ya jamii huwashauri wasitumie tunda hili kama njia ya kulinda ujauzito wao. Ukweli upoje?
UVUMI Hivi karibuni baada ya Elon Musk kuununua mtandao wa Twitter kuliibuka uvumi kwamba bilionea huyo amepanga kurejesha akaunti zote za Twitter zilizofungiwa, kasoro ile ya aliyekuwa Rais wa Marekani kuanzia mwaka 2017 hadi 2021, Donald Trump. Kichwa cha habari cha taarifa hiyo kinasomeka kwa Kiingereza: “Elon Musk States Intention to Restore Every Banned Twitter Account, ‘Except For Donald Trump’, huku ikifuatiwa na maandishi yasomekayo kwa Kiingereza: "It may seem petty but I just don’t like him"- ikimaanisha kuwa ni jambo linaweza kuoneka dogo, ila yeye (Elon Musk) hampendi tu Donald Trump. Picha (screenshot) hiyo inayodaiwa kutoka ukurasa wa gazeti maarufu la Marekani, New York Times, imekuwa ikizunguka kwenye mitandao ya...
Siku chache baada ya kufariki nywele za mtu pamoja na kucha zake huonekana zikiwa zimeongezeka urefu. Jambo hili huonekana mara nyingi sana, linaweza pia kuthibitika kwa kutazama masalia ya binadamu yanayoibuliwa kila kukicha. Baada ya kufariki, sayansi inasema kuwa ukuaji wa kiumbehai kupitia seli hai zake hufikia mwisho, mifumo yote tendaji hukoma na hakuna jambo lolote ambalo huendelea. Kwanini ukuaji wa sehemu hizi unapingana na sayansi?
Tovuti moja inadai kutangaza nafasi za ufadhili wa masomo katika chuo kikuu nchini Norway na kusambaa katika mitandao ya kijamii. Tovuti hiyo ina ujumbe wa Kiingereza ulioandikwa vibaya unaotafsirika: "Kasome Nchini Norway Kozi Yoyote Uliyochagua Bila Malipo kwa Muda wote wa programu" "Programu ya Scholarship ya Chuo Kikuu cha Bergen Huwawezesha Wanafunzi wa Kimataifa Kusoma nchini Norway kwa Raha na Bure. Waombaji wajaze fomu hapa chini na kubofya Omba,” Tovuti hiyo ambayo ina muonekano wa kutilia shaka (norway.visa2abroad.online) imechapisha “nafasi” hizo kwenye makundi ya mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook, na katika nchi kadhaa ikiwemo Tanzania. Tovuti hiyo pia inaonesha "fomu ya maombi" ambayo inataka muombaji kujaza...
Back
Top Bottom