JamiiCheck - Tanzania

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Kuna madai kuwa Takukuru wameingia nyumbani kwa Kakoko leo ghafla na kumkuta na begi lenye $1,625,800 taslimu baada ya kusimamishwa kazi jana! Haijulikani hizo alizichota lini, lakini kama ni kweli inawezekana alikuwa akizichota pole pole kwa muda mrefu kidogo na huenda sasa hivi ana 'vijisenti' vingi sana huko Jersey au Switzerland kama yule mzee. Mkurugenzi wa TAKUKURU akanusha madai haya
Picha ambayo baadhi ya watu wanadai kuwa inamuonyesha raisi wa Urusi Vladimir Putin akitoa mafunzo kwa wapigania uhuru kusini mwa Afrika ilisambaa na kutumiwa na baadhi ya watu kuhalalisha kuwa nchi za kiafrika zinapaswa kuunga mkono Urusi katika vita vya Ukraine. Picha hiyo ilisambazwa sana mtandaoni baada ya kuchapiswa katika blogu za Zibwabwe mwishoni mwa mwaka 2018, machapisho hayo yalidai yanamuonyesha Putin katika mafunzo ya kijeshi ya Tanzania kwaajili ya harakati za kupigania uhuru katika nchi za Afrika mwaka 1973.
CEO wa Simba sports club Barbara Gonzalez kuna tetesi akafungiwa miaka mitano 5 au maisha kujihusisha na michezo haswa football Hii imetokea baada ya yanga kupeleka malalamiko TFF kuhusu tuhuma alizozitoa kwa team hiyo inapokea wageni ambao Simba ilikua ikicheza nao champion league na shirikisho Imeelezwa kua TFF wakiongozwa na karia bado wana hasira na huyo CEO kwakua aliwabania deal la GSM la billion 2 ambapo wanao huyo mwana dada ni kikwazo kikubwa kwao kwenye mipango yao ya kupiga pesa
Mwishoni mwa mwaka 2021 kuliibuka taarifa kuwa Serikali ya Uganda imeshindwa kulipa deni kiasi cha dola milioni 207 na kusababisha kutaifishwa uwanja wake wa nddege wa Entebbe. Taarifa hizo zilizochapishwa na vyombo mbalilmbali duniani vilieleza kuwa Uwanja wa Entebe sio mali ya Uganda tena, kwamba Wachina wameutwaa uwanja huo. Taarifa hizo pia zilisambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwamo Twitter.
Wakati Rais Samia akimpolea Rais wa uganda Yoweri Mseveni uwanja wa ndege jijini Dar kuna taharuki ya kuwepo mgonjwa wa kwanza wa kirusi kipya kilichogunduliwa Afrika ya Kusini siku tatu zilizopita. Mgonjwa huyo Mzungu Rais wa Botwana aliyedaiwa kuingia nchini kutokea mjini Johannesburg Afrika ya Kusini leo asubuhi kwa ndege ya shirika la ndege la KQ la Kenya. Rais Mseveni na mweyeji wake wamekutana eneo ambalo kwa sasa huenda ndio kitovu cha kirusi kipya cha Corona. Tanzania haijachukua hatua zozote za kujilinda na kirusi hicho kipya huku nchi za nyingi zikizuia ndege kutoka mataifa kadhaa ya kusini mwa afrika kuzuia kuenea kwa kirusi hicho kinachoadaiwa kuwa kinasambaa kwa kasi zaidi. Mgonjwa huyo alipimwa baada ya kuonekana kuwa...
Back
Top Bottom