Video moja iliyowekwa kwenye mtandao wa Facebook inadai kuwa Naibu Rais wa Kenya William Ruto "ameichochea" jamii yake ya Wakalenjin dhidi ya Wakikuyu wakati wa mkutano wa kampeni kabla ya uchaguzi wa Agosti 9 2022.
Katika kipande hicho cha video kilichochapishwa tarehe 29 Julai, Ruto anazungumza kwa Kiswahili na Kiingereza, akimwambia rais aache kutaja jina lake.
Katika video hiyo Ruto anasema "Zungumza kuhusu mgombea wako,"Nilikuunga mkono ulipohitaji mtu wa kukusaidia. Ikiwa hutaki kuniunga mkono, niache peke yangu.”
Ruto alitofautiana na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na yeye akamuunga mkono kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuwania urais.
Katika video hiyo, Ruto anaendelea kuhutubia rais: “Sasa eti wewe unaanza kuni-threaten...