JamiiCheck - Tanzania

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Alhamisi ya pili ya Mwezi Machi kila mwaka, Dunia huadhimisha Siku ya Figo Duniani ili kutoa ufahamu na kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa afya ya figo na magonjwa yanayohusiana na figo. Kupitia maadhimisho haya, watu hupata fursa ya kujifunza kuhusu njia za kuzuia magonjwa ya figo, kudhibiti magonjwa ya figo, na umuhimu wa kuwa na maisha yenye afya ya figo. Aidha, maadhimisho haya huchangia katika kuongeza uelewa wa umma kuhusu haja ya kuchangia katika juhudi za kuzuia na kutibu magonjwa ya figo, pamoja na kusaidia watu wenye matatizo ya figo kupata msaada unaohitajika. Hata hivyo, ugonjwa huu huambatana na dhana nyingi potofu zinazofifisha kasi ya kupambana nao hivyo JamiiCheck imekuandalia ufafanuzi wa Dhana hizo kama sehemu ya...
Imezoeleka kuona watoto wachanga wakiwa wamefunikwa manguo mengi sana, hii sio shida iwapo hali ya hewa inaruhusu yaani ya ubaridi au ya kawaida. IIa kunaweza kuwa na hali ya joto kali watu wazima mnatamani kukaa kwenye feni ila mtoto mchanga bado kafunikwa mablanketi na kavishwa sweta, ukihoji unajibiwa watoto wachanga hawahisi joto. Wapo wanaotetea hoja hii kwa madai tumboni kulikuwa na joto hivyo mtoto hawezi hisi joto bali huhisi baridi muda wote. Je, hii ni kweli?
Kuna video inasambaa twiter na Instagram ikimuonesha mwanaume akiruka dirisha na kukimbia huku akiwa mtu kabisa bila nguo, watu hao wamekuwa wakishare video hiyo na kuweka ujumbe wa MKE WA MTU SUMU wakimaanisha mtu huyo alikuwa na mke wa mtu kisha akafumaniwa ndio anakimbia. Je, ni kweli mtu huyo anakimbia fumanizi na tukio hilo limetokea Tanzania? JamiiCheck, msaada wa kujua ukweli.
Salaam Wakuu, Ikiwa Ligi Kuu ya NBC imeisha leo 28/05/2024 huku Yanga akiwa Bingwa Azam nafasi ya pili na Simba nafasi ya tatu. Kuna tetesi kuwa Simba Sports Club na Yanga SC zitacheza African Football League, Azam FC watacheza CAF Champions League pamoja na Coastal Union. Taarifa hiyo inadai Kombe la Shirikisho limefutwa. Je, kuna ukweli wowote wa taarifa hii?
Mara nyingi nikiwa na stress na kupelekea kukosa usingizi, huwa navuta sigara ili kupunguza stress hizo. Hata iwe usiku wa manane nitajitahidi niende kwenye Club zinazokesha nikafuate sigara. Suala la kuwa inanisaidia au lah, sidhani lakini pale napokuwa navuta huwa nakuwa katika hisia nyingine kabisa. Chanzo cha kutumia sigara kama relief ya stress, ni baada ya kuona kwenye muvi mara kwa mara, na ushauri kutoka kwa marafiki. Nachotaka kujua kitaalam ni kama kweli sigara inasaidia kupambana na msongo wa mawazo tunaokumbana nao mara kwa mara.
Mwanafalsafa, mchumi na mwanasiasa wa India ya kale, Chanakya aliwahi kusema, “There is some self-interest behind every friendship. There is no friendship without self-interests. This is a bitter truth.” Kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili tunaweza itafsiri kama “Hakuna urafiki bila maslahi binafsi. Huo ndio ukweli mchungu.” Hii inaendana na msemo maarufu usemao. “There are no permanent enemies nor permanent friends, just permanent interests.” au “Hakuna marafiki wa kudumu wala maadui wa kudumu. Kuna maslahi ya kudumu tu.” Nimeanza makala hii na misamiati hiyo kwa nini? Ni kwa sababu lengo la makala hii ni kufichua unafiki ambao viongozi wa juu wa CHADEMA wamekuwa wakiufanya. Unafiki huu huwafanya waseme na kutenda kwa njia moja...
Kuna wazandiki huwa nawashangaa wanavyoponda pombe. Pombe haina madhara kama wanafiki wanavyotuaminisha. Pombe ni nzuri ukinywa kistaarabu, ina faida lukuki, ukibisha muulize Albert Chalamila. Tafiti zinasema kuwa beer zinasaidia kujilinda na magonjwa ya moyo. Kama mnavyojua magonjwa ya moyo yanaondoa watu kimya kimya hivyo mimi nawashauri tunywe beer kujilinda na magonjwa ya moyo. Hata Biblia inasisitiza tunywe pombe tufurahie, na mkituona tunakunywa pombe msitukwaze. Too much of anything is bad, but too much good whiskey is barely enough
Back
Top Bottom