Matumizi ya tumbaku ni moja ya maafa ya afya ya umma yanayojulikana sana. Licha ya ripoti nyingi kuhusu afya ya umma, matumizi ya tumbaku yanazidi kuongezeka katika nchi zinazoendelea na zilizoendelea.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), takriban watu Bilioni 1.3 duniani wanavuta sigara ambapo 80% kati yake wanatoka kwenye nchi zenye uchumi mdogo na uchumi wa kati. Aidha, takriban watu Milioni 7 hupoteza maisha kutokana na athari za moshi wa sigara unaotokana na kuvuta sigara moja kwa moja au pia kuvuta moshi uliotolewa na mvutaji wa Sigara.
Tumbaku huathiri karibu kila kiungo na mfumo katika mwili, ikisababisha matatizo mbalimbali kama vile saratani, Magonjwa ya mfumo wa upumuaji, Ugonjwa wa Mishipa ya Moyo, Kiharusi...