Yandex ni njia nyingine ya utafutaji inayotumika sana kufanya uhakiki wa picha.
JamiiCheck imekuandalia utaratibu wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kutumia Nyenzo hii kufanya uhakiki wa picha.
1. Fungua Kivinjari Chako
Anza kwa kufungua kivinjari chako kwenye kifaa chako cha mkononi au kompyuta.
2. Tembelea Tovuti ya Yandex
Ingiza 'Yandex' kwenye sanduku la utafutaji la kivinjari chako na bonyeza kwenye matokeo yanayofanana na tovuti rasmi ya Yandex.
3. Pakia Picha
Kuna njia mbili za kupakia picha kwenye tovuti ya Yandex
Bofya kwenye alama ya kamera iliyo kwenye sanduku la utaftaji la Yandex na chagua 'Pakia Picha' au 'Upload' kisha upakie picha unayotaka kufanya uhakiki.
Ikiwa picha tayari iko kwenye wavuti, unaweza kunakili URL...