Salaam Wakuu,
Kupitia WhatsApp yangu nimetumiwa ujumbe wa tahadhari kuhusu kuwepo kwa Mvua katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania. Ujumbe huo unaeleza:
Shinyanga, Dar, Pwani, Mafia,Tanga, Mwanza, Geita, Mara, Simiyu, Kigoma na Kagera tujiandae, kutakuwepo na Pacific El nino na Atlantic El nino, mvua zitakuwa kubwa na hatari sana, Mungu atunusuru. Hali ya hewa tayari imebadilika kuanzia juzi, upepo umeanza katika bahari za Atlantic, Pacific na Hindi, Wavuvi wameanza kuzuiwa kwenda kuvua na Meli za tafiti zimeanza kukumbana na dhoruba kali sana Baharini, picha za satellite sio nzuri kabisa. Tunatarajia magonjwa ya Kuharisha, Dengue, Malaria na Homa kuongezeka, tuchukue tahadhari mapema.
Tuangalie nyumba zetu kama zinavuja...