JamiiCheck - Tanzania

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Baada ya Singida Fountain Gate FC kupoteza mchezo wao wa Ligi ya NBC Premier League wakiwa nyumbani dhidi ya Simba, kupitia mitandao ya kijamii walitoa malalamiko yao wakiituhumu TFF na Ligi ya Bodi kuwapangia refa kwenye michezo wanayokutana na Simba ambaye amekuwa akiibeba timu ya Simba SC baada ya kupewa maelekezo maalum ya kuwabeba Simba. Singida FG wamedai kuwa katika michezo ambayo refa huyo amekuwa akichezesha dhidi ya Simba basi yeye ndiye huibuka Man Of The Match, hivyo wamezitaka taasisi hizo zinazosimamia ustawi wa mpira wa miguu nchini kutolea ufafanuzi.
Aprili 27, 2023, akaunti ya Mtandao wa Twitter inayotumia jina la MainLandAfrica iliweka chapisho linalodai kuwa Bilionea wa Marekani Dan Friedkin amekodisha takriban Ekari 6,000,000 za ardhi nchini Tanzania. Chapisho hilo lilienda mbali zaidi kwa kudai kuwa Friedkin ni mmiliki wa Ekari zingine 25,000 za ardhi zinazounda pori la Akiba la Mwiba. Wanaojua kuhusu huyu jamaa watupe details anafanya biashara gani na ardhi kubwa kiasi hicho?
Tetemeko la aridhi nchini Morroco limeua zaidi ya watu 5000, kuna kijiji kimoja cha mlimani chote kimefutwa na tetemeko isipo kua majengo mawili tu, hayo majengo mawili ni msikiti wa kijiji na nyumba ya huyu alio jenga huo msikiti, hiivi hili lina uhusiano wote na Imani au ni ecological force tu, wenye uelewa mambo theology na geography tuambieni.
Wakuu, Habari hii imesambaa kwenye mitandao ya kijamii, kwamba huyu Daktari baada ya kumkosoa Rais wa Burkina Faso Kpt. Ibrahim Traore kuhusu kushindwa kupambana na magaidi, alikamatwa, akavishwa magwanda kwenda kupambana na magaidi hao kwakuwa yeye analiweza suala hilo kuliko jeshi. Hii taarifa ni ya kweli au tunapigwa kamba tu?
Ingawa ni kama utani na inachekesha ila huwezi amini kuwa ng'ombe akijamba/kutoa ushuzi basi kile kitokacho huambatana na gesi ya methane ambayo huzalisha joto na moto/mwanga. Wanaharakati mbalimbali wa mazingira wamekuwa wakidiscourage ufugaji/uzalishaji wa ng'ombe kwa wingi na kusema wazi kuwa ushuzi wa ng'ombe huleta mabadiliko ya hali ya hewa, kwa sababu ng'ombe hutoa methane, gesi chafu inayohusishwa na ongezeko la joto duniani. Ng'ombe akiwa anajamba, ukiwasha njiti ya kiberiti moto unawaka kutokana na gesi ya methane. Ningependa kujua ukweli wa hili jambo.
Video ya Kushtua ya Wanajeshi imetolewa ikimuonesha Jonas, wa Kamandi Kuu ya Ideal Zimbabwe, anapinga moja kwa moja serikali ya Zimbabwe na Kuomba msaada wa silaha zaidi katika video yake. Jonas Alitangaza Mrengo wake mpya wa Kijeshi mwezi uliopita na watu wengi hawakumchukulia kwa uzito wakati huo, ikijumuisha Gambakwe Media. Mahema na waasi wanaonekana kwa nyuma huku Jonas anazungumza katika kile kinachoonekana kama jumba la kijeshi linalofadhiliwa vyema. Video ya Tinashe Jonas akizungumza mpango wa kumwondoa madarakani Rais Emmerson Mnangagwa
Back
Top Bottom