Taarifa potofu ni habari ambayo si sahihi. Taarifa potofu inaweza kuwa na athari hasi au kuwachanganya watu kutokana na ukosefu wa usahihi au udanganyifu.
Athari za taarifa potofu yanaweza kuwa makubwa au vinginevyo kulingana na unyeti wa taarifa iliyosambazwa ikiwa haina usahihi. Kadiri inavyozidi kusambaa na kuchukua muda mrefu bila kukanushwa au kutolewa ufafanuzi wa upi usahihi wake ndivyo huweza kuathiri kundi kubwa zaidi na kuleta madhara zaidi.
Pamoja na hatari iliyopo juu ya usambazaji wa taarifa potofu bado jamii hailichukulii kwa uzito suala la kufanya uhakiki wa taarifa unozopokea wala kusambaza wala kutilia mkazo elimu ya ya kutambua ubaya wa taarifa potofu, lindi la kusambaa kwa taarifa potofu kupitia mitandao ya kijamii...