Klabu ya Simba ambayo ipo nchini Misri katika maandalizi ya msimu mpya 2024/25, leo Julai 14, 2024 imecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Tersana FC inayoshiriki ligi daraja la pili Misri na kuambulia kichapo cha goli 6-2.
Mchezo huo ambao ulikuwa na lengo la kujaribu kikosi chao, Wanalunyasi walijikuta wakipokea kichapo hicho cha goli 6-2 baada ya kiungo wao Debora kupata kadi nyekundu dakika ya 36 huku matokeo yakiwa 2-1.
Magoli mawili ya Simba katika mchezo huo yalifungwa na mshambuliaji raia wa Zambia Fred Koblain dakika ya 32 na Kiungo wao mpya Yusufu Kagoma dakika ya 61.
Magoli 6 ya Tersana yalifungwa dakika za 12, 26, 41, 54,67 na 76.
Mara baada ya mchezo huo makocha wa Simba waligoma kuongelea matokeo hayo kwani ni...