JamiiCheck - Tanzania

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Katika pita pita yangu ndani ya maktaba moja kubwa hapa nchini nimekutana na jina la huyu mtoto, Momčilo Gavrić na taarifa kuwa ndiye mtoto au mtu mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuingia vitani mpaka sasa, huku vita ya kwanza ya dunia WWI iliyoanza Julai 28, 1914 na kutamatika mwezi Novemba 11, 1918. Momčilo Gavrić inasemekana aliingia vitani akiwa na umri wa miaka nane tu na kuanza majukumu ya kupambania taifa la Serbia. Nimekuja huku ili nipate kufahamu je ni kweli kuwa Momčilo Gavrić alipata kujiunga na jeshi akiwa na umri huu wa miaka nane?
Kisayansi na kibaiolojia virusi wanasifa ya kutokuwa hai pale wanapokuwa nje ya seli ya kiumbe mwingine(host) na wanaweza kukaa muda mrefu bila kuwa na dalili zote za viumbe hai mpaka pale watapoingia kwenye seli ya kiumbe. Inakuwaje sasa tunaambiwa HIV haambukizwi kwa mashine za kunyolea saloon kwa kigezo cha kwamba hawawezi kuishi katika mashine na ilihali wao ni vijidudu visivyo hai wanapokua nje ya host?
Back
Top Bottom