JamiiCheck - Tanzania

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Kuna magonjwa mengi yanayosababisha upungufu wa Kinga mwilini ikiwemo maambukizi ya VVU. Kumekuwa na mijadala mingi pamoja na tetesi zinazohitaji majibu ya kina kuhusu uwezekano wa kupata VVU/UKIMWI kutoka kwa mtu aliye athirika hasa ikihusisha ushiriki wa tendo la ndoa pasipo kutumia kinga hata kama ni mara moja tu. Ukweli upoje na majibu ya kisayansi yanatoa picha gani? Baadhi hudai hauwezi kupata VVU/UKIMWI kwa kufanya tendo moja tu la ngono na muathirika pasipo kutumia kinga kwa kuwa maambukizi hayaji kirahisi hivyo kama tunavyodhani.
Kumekuwa na akaunti yenye jina la Luaga Mpina inachapisha taarifa mbali mbali kuhusu mambo yanayoendea nchini na kujibu hoja za Mbunge Luaga Joelson Mpina wa jimbo la Kisesa ndani ya mtandao wa X zamani twitter. Naomba JAMIICHEK inisaidia kujua ukweli kama akaunti hii ni mali halali au inamilikiwa na Luaga Joelson Mpina mwenyewe ambaye ni mbunge wa jimbo la Kisesa na kwa sasa yuko nje ya bunge kwa adhabu.
Habari wakuu, nimeshangaa sana kuona WASAFI TV ikitumia lugha ya kihuni tena yenye maudhi katika uwasilishaji wa taarifa. Chombo mahili hakiwezi kutumia neno 'usela mavi' katika kufikisha ujumbe wake kwa hadhira,binafsi siyo mtaalamu wa teknolojia labda nyie wajuvi wa mambo hayo tazameni hii video chini kisha mniambie kama ni editing au laa. Kama ni Wasafi kweli lazima tujiulize maswali yafuatayo: Je hii jeuri wanaipata wapi ya kutudhihaki sisi juu ya msiba mkubwa kama huo? Je wao wanatumika katika kuchochea maovu ya utekaji au wao wanajikuta akina nani labda na chombo chao? Je wamezingatia nini katika uwasilishaji wao wa hiyo habari na je wameelewa kweli nini maana ya kupinga na kupaza sauti kwa vitendo juu ya mauaji? Pia soma...
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu, amesema Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe amemzuia kwenda katika ofisi kutokana na yeye kueleza ubadhirifu unaofanywa ndani ya chama. Pia Lissu amesema sababu nyingine ya kuzuiwa kwenda katika ofisi hizo ni kutokana na kutoa siri za vikao ndani ya chama, na kumueleza ukweli kuhusu kitendo cha kuanzisha taasisi nyingine ndani ya CHADEMA. Aidha Mwanahalisi ina nakala rasmi ya barua ya siri ambayo Mbowe amemwandikia Lissu kwa kumpiga zuio la kwenda ofisini.
Akili Mnemba ni teknolojia iliyosambaa ulimwenguni ikiwa imerahisisha kazi za binadamu kutokana na kwamba inaweza kufikiri kama binadamu. Lengo la AI ni kuweza kufanya mambo kama vile kutambua mifumo, kufanya maamuzi, na kuhukumu kama binadamu. Akili mnemba (AI) ni seti ya teknolojia zinazoiwezesha kompyuta kutekeleza majukumu mbalimbali ya kina na kwa uwezo mkubwa kadri ya maelekezo ya mtumiaji, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuona, kuelewa na kutafsiri lugha inayozungumzwa na maandishi, kuchanganua data, kutengeneza picha na video na kutoa mapendekezo ya utatuzi wa matatizo mbalimbali. Akili mnemba ni muhimu katika shughuli za kila siku kwani husaidia kurahisisha utendaji kazi wenye ufanisi hata hivyo kama itatumika katika namna ovu...
Baada ya Afrika, bara la Amerika Kusini ndilo lenye watu weusi wengi zaidi wakikadiriwa kuwa zaidi ya milioni 170 huku Brazil ikiongoza ikiwa na watu weusi takriban milioni 120. Nchi ya Argentina inatajwa kuwa mpaka sasa watu weusi ni chini ya laki mbili wakiwa takriban asilimia 0.5% kutoka asilimia 48% miaka ya 1800. Inadaiwa watu weusi baada ya kuisaidia Argentina kupigana vita na maadui zake, watu weusi waliosalia waliwekwa kwenye maeneo maalumu ambayo kwa kipindi hicho kulikuwa na ugonjwa wa hatari unaosababishwa na bacteria “Plague” ambapo serikali iliwanyimwa huduma muhimu hivyo upelekea vifo vyao. Zitto kupitia ukurasa wake wa Twiiter aliwahi kumhoji jamaa kuhusu kuishabikia Argentina, nanukuu 'Una support argentina ambayo...
Back
Top Bottom