JamiiCheck - Tanzania

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Taarifa kutoka TUCTA Ndugu wafanyakazi napenda kuwataarifu kwamba kuanzia mwezi huu mishahara itakua ikitoka tarehe za mwisho wa mwezi yaani tarehe 28-30. Lengo la kufanya hivyo ni kuondoa gap lililopo kati ya tarehe za mishahara wa sektabinafsi na sekta za Umma. Mwenyekiti wa TUCTA kasema hayo leo wakati akipongeza kuongezeka kwa asilimia ya Kikokotoo kutoka asilimia 33 mpaka 40.
Tangu Juni 18, 2024 nchi ya Kenya imetawala vyombo vya habari baada ya Wananchi wake kufanya maandamano wakipinga mswaada wa fedha (Soma hapa). Kufuatilia tukio hilo kumekuwa na picha mbalimbali zinasambaa mitandaoni na kuhusishwa na Maandamano ya Kenya ya Juni. Baadhi ya picha ni halisi na zinatokana na tukio hilo lakini nyingine zimezushwa na kuhusishwa na Maandamano ya Kenya. JamiiCheck itakusogezea baadhi ya picha zinazohusishwa na tukio hilo kimakosa.
Salaam Wakuu, Nimekutana na maandiko yanadai kuwa Lissu akiwa kwenye mkutano Singida alisema mtoto wa Rais Samia aitwaye Abdul aliwahi kumpelekea rushwa akamfukuza. Je, kauli hii ni kweli? Tunaomba mtusaidie kutafuta uhakika --- Video 1: Lissu akiwa Mkutanoni Singida akielezea kufuatwa na Abdul Video 2: Lissu akieleza kufuatwa na Abdul katika Spaces ya Maria Sarungi
Kumetokea uvumi unaosambaa sana kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na uwepo wa ugonjwa hatari nchini CONGO DRC. Ugonjwa huo unasemekana kuenea na kuambukizwa zaidi kwa njia ya ngono. Pia inasemwa muathirika huugua kwa kipindi Cha muda mfupi sana (kati ya siku 4 Hadi wiki 2) Hadi kupoteza maisha. Naomba wanajukwaa na JamiiForums kwa ujumla tusaidiane kuhakiki habari hii ambayo imekuwa ikisambaa kwa kuambatana na sauti inayoelezea ugonjwa huo pamoja na picha za waathirika na watu wakifanya mazishi (ya anayesemekana kafariki kwa ugonjwa huo) huku wakiwa wamevalia mavazi ya kujikinga mawili mzma na kuacha sehemu ya uso tu. TAHADHARI: Baadhi ya picha sio nzuri kutazama hadharani. Naomba radhi kwa hilo, nazi-attach kama nilivyozipokea...
Leo nimeona video ambao imewekewa sauti ya mtu akisema wametumiwa video hiyo kwenye group la shule ya Themihill, video hiyo inaonesha mtu akifungua kitu kinachoonekana kama pen (kalamu) ambacho ndani yake kina risasi na baadaye kufyatuliwa. Anayeelezea video hiyo anadai pen hizo zinagawiwa mashuleni na kuuzwa huku akionesha hofu ya watoto kuuana au wao wenyewe kujidhuru kwa peni hizo. Ningependa kufahamu ukweli kuhusu video hiyo.
Kamanda Tundu Lissu amekanusha madai yaliyotolewa hapo nyuma kidogo na Lema kwamba Mbowe ndio aliyeshika chupa ya damu wakati akipelekwa Nairobi kwa matibabu. Amesema aliyeshika chupa ya damu aliyokuwa akiongezewa ni Mchungaji Peter Msigwa mwanasiasa nguli asiyeogopa hila na figisu. Wataalam wa mambo ya siasa za kusini mwa jangwa la sahara wanasema hii kauli imebeba maana kubwa sana.
Katika jamii yetu ya kitanzania asilimia kubwa inatumia vyombo vya plastiki kunywea na kulia chakula, lakini nimekuwa nikisikia kuwa plastiki ina madhara makubwa kwa afya ya binadamu, wapo wanaodai inasababisha saratani, wengine inamaliza nguvu za kiume kwa wanaume na mambo mengi. Je, ni kweli ina madhara? Maana napata mashaka kwani sijawahi kusikia serikali ikisema kuhusu madhara hayo au kukemea matumizi yake wala kutoa elimu ya namna ya kuvitumia.
Back
Top Bottom