Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema kuwa juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan zimeifanya Tanzania kuwa kinara barani Afrika katika uzalishaji na usambazaji wa umeme.
Akizungumza na wanahabari katika Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) mkoani Pwani siku ya Jumapili Februari 16, 2025, Msigwa amesema kuwa mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu nishati uliofanyika Januari 27-28, 2025 jijini Dar es Salaam, ni uthibitisho wa mafanikio ya Tanzania katika sekta hiyo.
Kwa mujibu wa Msigwa, hali ya upatikanaji wa umeme nchini imeimarika na kufikia 78.4%, huku serikali ikipanga kuhakikisha asilimia 100 ya Watanzania wanapata huduma hiyo...