Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikiwa na historia ya miaka 48 ya uimara, umoja, na mafanikio makubwa, kimeendelea kuwa mwamba wa siasa za Tanzania huku kikijipambanua kama kiongozi wa maendeleo na mshikamano wa kitaifa. Kwa upande mwingine, vyama vya upinzani, kama CHADEMA, vimeonekana mara kwa mara kushindwa kuonyesha uimara wa kisiasa na kusimamia masuala ya msingi yanayogusa maisha ya Watanzania.
CCM, kupitia misingi yake imara ya kihistoria, kimefanikiwa kuimarisha uchumi, kuleta amani na utulivu, na kuendelea kushika usukani wa maendeleo ya kitaifa. Kwa mfano, katika awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, CCM imeonyesha jinsi ya kuendesha diplomasia madhubuti, kuimarisha miundombinu, na kutoa fursa kwa Watanzania kushiriki...