ZABURI 35
Kuomba msaada
(Zaburi ya Daudi)
1 Ee Mwenyezi-Mungu, uwapinge hao wanaonipinga;
uwashambulie hao wanaonishambulia.
2 Utwae ngao yako na kingio lako,
uinuke uje ukanisaidie!
3 Chukua mkuki na sime yako dhidi ya wanaonifuatia.
Niambie mimi kwamba utaniokoa.
4 Waone haya na kuaibika...