maambukizi

No Wikipedia entry exists for this tag
  1. beth

    #COVID19 Indonesia yaanza kulegeza kanuni za kudhibiti Corona baada ya maambukizi kupungua

    Kutokana na kupungua maambukizi ya CoronaVirus Taifa hilo litaanza kulegeza Kanuni kuanzia kesho Agosti 24 ambapo maeneo ya kufanya manunuzi na nyumba za ibada katika baadhi ya Miji zitaruhusiwa kufunguliwa. Maeneo ya Ibada na Migahawa itatakiwa kufanya kazi kwa kiwango cha 25% na maeneo ya...
  2. Kasomi

    Makala dhidi ya Maambukizi mapya ya ukimwi

    MAKALA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA YA UKIMWI Takwimu Zinasema Vijana Wenye Umri Wa Miaka 15 -24 Ndiyo Wanaongoza ! Hii Inaogofya ,Inatisha na Inanisukuma Moja Kwa Moja Leo Hii Hadi Kwa WATUNGA SERA , WATUNGA SHERIA ,WATUNGA KANUNI Nilio Wataja Hapo Juu Ni Mihimili ya Nchi Yenye Wajibu Katika...
  3. beth

    #COVID19 China haijarekodi maambukizi ya ndani kwa mara ya kwanza tangu Julai, 2021

    Mamlaka ya Afya Nchini humo leo imesema kwa mara ya kwanza tangu Julai, hakuna maambukizi ya ndani ya COVID-19 yaliyoripotiwa, hali inayoashiria huenda mlipuko wa hivi karibuni umedhibitiwa. Tangu Julai 20 zaidi ya watu 1,200 walithibitishwa kupata maambukizi ya Virusi vya Corona China. Hata...
  4. Cannabis

    #COVID19 Nani anayehusika kupeleka takwimu za maambukizi ya COVID-19 Africa CDC?

    Kwa mujibu wa taarifa zilizopo Africa CDC inaonekana mpaka tarehe 19 August 2021 Tanzania ina visa 16,970 vya maambukizi ya virusi vya corona na vifo 50.Pia WHO inaonyesha kuna visa 1,367 na vifo 50. Je, hizi taarifa ni rasmi ? Kuna makosa yaliyofanyika au ni hujuma ? Kuna umuhimu wa jambo...
  5. beth

    Iran yatangaza lockdown kudhibiti maambukizi ya Kirusi Delta

    Taifa hilo lililoathirika zaidi ya janga la Corona Mashariki ya Kati litaweka zuio la safari zote za barabara pamoja na Lockdown ya wiki moja Biashara na Ofisi zote ambazo sio za mahitaji muhimu zitafungwa kuanzia Jumatatu (Agosti 16) hadi Agosti 21, ikiwa ni jitihada za kukabiliana na Kirusi...
  6. Kasomi

    Wizara ya Madini yawasilisha Mpango Mkakati Kupunguza Maambukizo ya VVU Na TB Migodini

    WIZARA YA MADINI YAWASILISHA MPANGO MKAKATI KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA VVU NA TB MIGODINI Na. Emmanuel Kasomi - Dodoma Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Tume ya Madini na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeandaa Mpango Mkakati wa Usimamizi wa Masuala ya UKIMWI (VVU)...
  7. beth

    #COVID19 UAE: Maambukizi ya Virusi vya Corona yafikia 695,619

    Umoja wa Falme za Kiarabu umerekodi maambukizi mapya 1,334 ndani ya saa 24 zilizopita huku wagonjwa 1,396 wakipona na wanne wakipoteza maisha. Tangu kuanza kwa janga la COVID-19 watu 1,982 wamefariki dunia na idadi ya visa imefikia 695,619. Zaidi ya 80% ya watu UAE wamepata angalau dozi moja ya...
  8. beth

    #COVID19 India: Idadi ndogo zaidi ya maambukizi tangu Machi yaripotiwa

    Visa vipya 28,204 vya COVID19 vimerekodiwa ndani ya saa 24 zilizopita, idadi ambayo kwa mujibu wa takwimu za Serikali ni ndogo zaidi kurekodiwa katika Taifa hilo tangu Machi 16. Kwa ujumla, maambukizi yapatayo Milioni 32 yamerekodiwa India hadi sasa. Wizara ya Afya imesema vifo 373 vimeongezeka...
  9. Analogia Malenga

    #COVID19 UN: Taarifa feki kuhusu chanjo zinazidisha muda ambao ungetumika kudhibiti maambukizi

    Umoja wa Mataifa(UN) umesema taarifa zisizo sahihi kuhusu chanjo ya #COVID19 kunarefusha muda ambao ungetumika kudhibiti maambukizi ya Corona. UN wametoa wito kwa raia kuhakiki taarifa kabla ya kusambaza taarifa hizo kwa wengine ambazo zinaathiri mapambano dhidi ya Corona. Wamesema taarifa za...
  10. beth

    #COVID19 Maambukizi zaidi yaendelea kuripotiwa China

    China imeendelea kurekodi maambukizi zaidi ya Virusi vya Corona, ikiwa ni wiki ya tatu tangu mlipuko mpya kuripotiwa. Visa vipya 125 vimerekodiwa na baadhi ya Miji imeongeza jitihada za upimaji ili kukabiliana nao. Kirusi Delta kimegundulika katika Miji kadhaa Nchini humo tangu Julai 20. Katika...
  11. beth

    Australia yarekodi idadi kubwa zaidi ya maambukizi

    Australia imeshuhudia idadi kubwa zaidi ya maambukizi ambapo visa 361 vya Kirusi Delta vimerekodiwa kutoka New South Wales, Victoria na Queensland Asilimia 60 ya Wakazi wa Australia (sawa na takriban watu Milioni 15) wapo Lockdown. Taifa hilo lenye visa zaidi ya 36,000 na vifo 937 kwa kiasi...
  12. Miss Zomboko

    #COVID19 RC Mtaka: Hali si shwari Dodoma. Wananchi waendelee kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona

    Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amewataka wakazi wa Dodoma kuchukua hatua za tahadhari dhidi ya ugonjwa wa corona kwa sababu hali si nzuri mkoani humo. Ameyasema hayo leo Jumanne Agosti 3, 2021 wakati akizungumza na askari wa usalama wa barabarani na viongozi wa masoko wa mkoa wa Dodoma...
  13. beth

    #COVID19 Japan yashuhudia ongezeko la maambukizi. Hospitali kupokea walio hoi tu

    Japan inatarajia kubadili Sera ili kuweka kipaumbele katika kulaza Wagonjwa wa COVID19 wanaoumwa sana ili kuepuka kudhoofisha Mfumo wa Afya. Hivi sasa Taifa hilo linarekodi zaidi ya visa 10,000 kila siku. Wagonjwa wengine watatakiwa kubaki nyumbani na Serikali itahakikisha wanalazwa hali zao...
  14. Pdidy

    #COVID19 RC Makalla, Mwamposa anamaIiza ibada 12 jioni, kuna Kanisa wanatoka saa 6 usiku huko Temboni mpo kimya! Tutaponaje na COVID-19?

    Dkt. Mwamposa aliwahi kuonywa hili, tunashukuru amekuwa msikivu Ukisikiliza matangazo yake aliwakuwa anatangaza wanaingia saa sita wanatoka 6pm mwisho akanza toa watu saa 3 usiku Vibaka walijazana sana sana wakaripoti husika, dk anaenda sawa 6pm kwenu Kuna kanisa Temboni Mh. Makalla, watu...
  15. Miss Zomboko

    Iringa: Muda wa kuswali Misikitini wapunguzwa ili Kudhibiti Maambukizi ya Coronavirus

    Muda wa kuswali wapunguzwa Mkoani Iringa, kuanzia jana, muda wa kuswali katika nyumba za ibada umepunguzwa kutoka zaidi ya dakika 30 za awali hadi kati ya dakika 10 na 15 siku ya Ijumaa. Shehe wa Mkoa wa Iringa, Abri Said alisema utekelezaji wa maelekezo hayo ulianza jana katika misikiti yote...
  16. kavulata

    #COVID19 Mkutano wa hadhara na Mpira wa hadhara kipi ni hatari kwa maambukizi ya Covid 19?

    Tanzania ni yetu sote hebu tuutangulize utanzania na Mungu mbele. Tunapofikiria kuzuia maambukizi ya Covid 19 kwa kuzuia mikutano ya kisiasa tufikirie pia kuzuia maambukizi kwenye viwanja vya mpira wa miguu kwakuwa watu ni walewale. TFF kupeleka mechi ya Simba na Yanga Kigoma kwenye uwanja...
  17. J

    Wanajeshi wa Korea Kusini wapata maambukizi ya #COVID19 wakiwa Pwani ya Afrika Mashariki

    Waziri Mkuu, Kim Boo-kyum ameomba radhi mbele ya Umma kwa Serikali ya Korea Kusini kushindwa kuzingatia #Afya za Askari wake wa Kikosi cha Maji Wanajeshi hao wa Korea Kusini wako kwenye doria maalum ya kukabiliana na Uharamia katika Pwani ya Afrika Mashariki Wizara ya Ulinzi imethibisha kuwa...
  18. Sam Gidori

    #COVID19 Japan: Wachezaji wawili wa Afrika Kusini wapatikana na maambukizi ndani ya Kijiji cha Olimpiki

    Wachezaji wawili wa Afrika Kusini ambao wapo nchini Japan kushiriki mashindano ya Olimpiki wamethibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona siku ya Jumamosi, wakitajwa kuwa washiriki wa kwanza wa mashindano hayo kupata maambukizi ya virusi vya corona wakiwa ndani ya Kijiji cha Olimpiki...
  19. Analogia Malenga

    Uingereza yarekodi Maambukizi Mapya 54,674 ndani ya saa 24 zilizopita

    Uingereza imetangaza kupata maambukizi mapya mengi tangu Januari ambapo yamefikia 54,674 ndani ya saa 24 zilizopita Aidha, kumerekodiwa vifo 41 ndani ya saa 24 zilizopita vilivyotokana na #COVID19 Hadi sasa Uingereza imetoa chanjo kwa 67.8% ya watu wake.
Back
Top Bottom