Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA @chadematzofficial Freeman Mbowe amesema kuna makundi yanayoratibu kufanyika mapinduzi ndani ya chama hicho na makundi hayo ndiyo yanayomsukuma Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara, Tundu Lissu kugombea nafasi ya Uenyekiti.
“Kuna kundi...
Heshima sana wanajamvi.
Baada ya tathimini ya hali ya juu kutoka kanda 8 Mhemiwa Mbowe anaongoza 81.5% huku mshindani wake mkuu Mheshimiwa Lissu akiambulia 17.3%
Wajumbe wengi wameonyesha msimamo wa kumuunga Mwenyekiti mkono kwa wivu mkubwa.
Ngongo kwasasa Mikocheni.
Nimeona mahojiano ya kikeke na mbowe.
Mbowe anasema amemfanyia mambo mengi ya kiutu ili kuboost safari ya mafanikio ya Lissu.
Kana kwamba anasema lissu hapaswi kumfanyia hivi kwa maana yuko liable na msaada wake.
But dude, this guy almost died for you and your people , hio yote bado haijalipa...
Yule Maria Sarungi haijulilkani hata anaishi wapi na ni Gener wa Keybord Worrior.
Humu sasa ndio kuna idadi isio hesabika ya Ma Keybord Worrior ambao front laini kamwe na daima huwezi waona na hutakaa uwaone.
Lisu anavimbishwa kichwa sana na hawa Keybord worrior ambao Ujasiri wao uko kwenye...
Huyu jamaa bado hajasema, mpaka aseme
Kwani kuna uhusiano gani kati ya sadaka alizozitoa kumpa Lissu linapokuja suala la Lissu kugombea nafasi ya Uenyekiti mpaka akumbushie sadaka alizompa Lissu?
Kumpa nyumba ya kukaa pale Dodoma inaleta uhusiano wowote kwenye kugombea nafasi aliyonayo mbowe...
Mfumo wa uongozi wa muda mrefu wa Freeman Mbowe kama Mwenyekiti wa CHADEMA unaweza kueleweka kwa kuangalia madhara ya kukaa katika cheo cha juu cha chama muda mrefu:
Kama Mbowe angaliachia madaraka baada ya muhula wake wa kwanza, angekumbukwa kama mtu aliye na maono ambaye kazi yake...
Mbowe kaanza visingizio mapema.
Kwani lissu Kula kitimoto na bia unahusika nini na uchaguzi?
Lissu Kula Sato na ugali wa mtama inakujaje kwenye uchaguzi kwa nini haukusema hayo mapema iweje Leo?
Mbowe atangaze Sera au aseme walikula wote hivyo vyakula, asilete ujanja ujanja kisa uchaguzi
Nimeona mh Mbowe akitaja fadhila ambazo amemfadhili mh Tundu Lissu tangu walipokutana mwaka 1995 na kuamua kushirikiana naye katika harakati za kisiasa nchini.
Wahenga wanasema, "tenda wema uende zako" na sio kusubiri fadhila. Mwl Nyerere aliwahi kupewa nyumba ya kuishi na marehemu Dosa Azizi...
Mbowe anaona vijana wake anao walea na kuwaleta mjini wana dharau. Lakini anasahau inawezekana kabisa wana nia njema ya kuiokoa Chadema na Tanzania. Kwa Watanzania wengi wnakubaliana na Lissu na wengine kwamba ni lazima mabadiliko yafanyike kwa manufaa ya umma.
Nimeona Leo Mbowe akimkaripia...
Akihojiwa na Kikeke nimemsikia Mbowe akisisitiza kwamba wapiga kura wataitwa mmoja mmoja na kuhojiwa hadharani (live) katika Kumchagua Mwenyekiti Mpya.
Binafsi nadhan hiyo sio sawa, wangepiga kura za Siri na baada ya hapo ndio kura zihesabiwe live, hili kuepuka intimidation kwa wapiga kura...
Mbowe analaumu Lissu kugombea Uenyekiti huku akilalamikia kumsaidia Lissu wakati tukijua yeye ni alimsaidia Lissu ili kufanikisha biashara zake za kisiasa.
Sasa kama walikubaliana abaki na umakamu wake kwanini alimsakazia wenje washindane nae?
Pia soma
- Tundu Lissu: Mbowe alimtuma Wenje...
Tangu Mbowe atangaze kuingia tena kwenye kinyang'anyiro cha kutaka kutetea nafasi yake ya uenyekiti hajaweza kusema ana agenda gani mpya kwa Chadema ili achaguliwe tena.
Muda mwingi amekuwa akijibu shutuma zinazomhusu na kujitetea kwanini anastahili kuendelea kukalia hicho kiti kwa miaka...
Natoa uzoefu kwa mambo nayoyakumbuka katika siasa za upinzani tangu nikiwa sekondari. Soma mpaka mwisho maana suala la Mbowe lipo mwisho mwisho.
Binafsi nimezaliwa enzi za Mwinyi. Hii generation ndio ambayo ilitarajiwa kukuza upinzani katika siasa za mfumo wa vyama vingi kwa sababu mbalimbali...
Mpo salama!
Ninachowakubali CCM wanajua kusukuma Kete zao kwa AKILI Sana na pale inapohitajika nguvu kidogo wanatumia
CCM KAMWE haitaruhusu Chama chochote cha upinzani kiwe chama cha siasa cha kitaifa.
CCM hawaoni shida wala haiwashughulishi chama cha upinzani kutawala kanda Fulani au Mkoa...
Liwalo na liwe this is too Much!Nikiri mimi ni Shabiki wa Lissu lakini anapoelekea hapana,kama anahama CHADEMA ahame tu namtakia Safari njema asituharibie Taasisi,sisi tutabaki Mashabiki wa CHADEMA hadi mwisho.
Hakuna asiyefahamu Mchango wa Mbowe kwenye Siasa za Upinzani Tanzania kama yupo...
Eeeh tusichoshane kwa mijadala isiyo na afya ooh Lisu hana adabu katumia sana pesa ya Mbowe haya sasa nguvu ya umma tunamtaka Lissu nyie timu mbowe leteni gharama alizotumia boss wenu tumrudishie
Mbowe kupitia Crown FM anasema kwenye uchaguzi wa kwanza Lissu akiwa CHADEMA Mbowe alimpa gari yake binafsi ili akafanyie kampeni. Pia anasema Nyumba aliyokuwa akiishi Lissu pale Dodoma ilikuwa yake aliyopewa na Serikali Ila akamuachia Lissu aishi yeye Mbowe akaenda kupanga.
Lissu nimemjenga na nimemsaidia kwa mambo mengi. Unapokuwa hauna Shukrani kwa mambo madogo hauwezi kuwa na shukrani kwa mambo makubwa. Kuna wakati ninajiuliza huyu ni Lissu, the boy, the guy, the friend ndiyo anayasema haya?”
Chama cha demokrasia na maendeleo chadema kilivuka salaama mwaka 2019 na hii nikwasababu mbowe hakuwa na mpinzani wake ! Hayo tumeyaona kipindi cha CHACHA WANGWE, NA ZITTO ZUBERI KABWE , tabia hizi za UASAAD ndiyo unakirudisha nyuma chama.
Mwaka huu sasa amekutana na wajanja wameshamshitukia...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.