Vijidudu/virusi vya corona vinaweza kuishi kwa muda kadhaa kwenye nguo, ngozi ya mwili, vitasa vya milango na maeneo kadhaa mbalimbali kama vile simu, samani, viti, mikoba, kalamu, madaftari, nk. Ndio maana tunasema tunawe mikono mara kwa mara na kuepuka kujishikashika usoni, puani na mdomoni...