Sanaa inaweza kutumika kuwasilisha fikra au mawazo yaliyo ndani ya akili ya mtu. Wasanii hutumia ufundi na ujuzi mbalimbali kubadili fikra na mawazo yao kuwa vitu vinavyovutia kwa hadhira zao.
Kazi za Sanaa zinaweza kuonekana kupitia tanzu za fasihi, uchoraji, ususi, uchongaji, ufinyanzi...