Kamati ya Maudhui ya TCRA, leo Jumatano imeipa onyo Wasafi Televisheni, pamoja na kuitaka iombe radhi mara tatu kwa siku, kuanzia kesho Alhamisi hadi Jumamosi, huku ikiiamuru ilipe faini ya Sh. 2 Mil., baada ya kukutwa na hatia katika kosa la kurusha maudhui yenye kukashifu dini ya Kikristo...