Hakuna wakati kama sasa katika historia ya nchi hii tokea tulipopata Uhuru ambapo wananchi wamekuwa katika hali ya wasiwasi mkubwa. Wananchi wameshindwa kuelewa Serikali inafanya maamuzi kwa kutumia vigezo gani na wananchi wengi wanakuwa na hofu kuhusu Usalama wao. Ukiwarudisha wabunge nyumbani...
Kama bunge likivunjwa Ina maana nchi inakuwa Haina bunge kwa kipindi Cha miezi kadhaa!! Hii imekaaje kwa mawaziri ambao ni wabunge?
Naona mawaziri wateuliwe na rais kutoka kwenye chama na wadhibitishwe na bunge ikiwezekana!!
Ni maoni tu
Hawa ni wale watia nia ambao wameacha nafasi zao ili wapate nafasi za ubunge ili kulinda maslahi ya chama chao.
Hawatakuwa kwa ajili ya maslahi ya umma na wananchi kama Luhaga Mpina
Spika Dkt. Tulia alivyowataka Wabunge kupunguza sauti na kuepuka kuongea na Simu na Wajumbe Bungeni; "Mnaanza kidogo kidogo, halafu zinapanda"
"Waheshimiwa Wabunge mnajadiliana mambo ya msingi sana lakini punguzeni sauti, wale mnaoongea na simu mnaanza kuongea kidogo kidogo lakini baadaye...
Wakuu,
Katika kipindi cha wiki moja tu, mbunge mmoja ambaye kwa muda wa miaka mitano alikuwa kimya na asiyeonekana mara kwa mara katika shughuli za maendeleo, sasa ameibuka kwa kasi ya ajabu.
Swali la msingi ambalo linaibuka kwa wananchi ni hili: Mbunge huyu alikuwa wapi kwa miaka yote mitano...
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Angasi Robert Okechi, amesema kuwa katika nchi zilizoendelea, Bunge ni mahali pa watu wenye upeo mkubwa wa fikra na maarifa, ambapo wabunge hukutana kuandaa mipango mikakati ya maendeleo ya muda mrefu kwa manufaa ya taifa.
Akizungumza leo Juni...
Rais mstaafu Jakaya Kikwete ametetea marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024 akihoji, "Hivi ni kweli kwamba, sheria zetu zinazohusu uchaguzi ni mbaya sana kiasi kwamba haziwezi kusimamia mchakato wa uchaguzi mwaka huu?"
Ameyasema hayo leo Juni 21 katika...
Habari Wana JF,Nimekuwa na Akili ya kujitambua tangu nikiwa na miaka15 hasa yanayohusu nchi na Wananchi. Mwaka 1985 Kulikuwa na chama kimoja tuu kwenye uchaguzi,Nakumbuka wabunge walikuwa wanaombea wawili kwenye chama kimoja!
Mmoja alitumia Alama ya Jembe, mwingine Alama ya nyundo,Na kumwaga...
Wakuu,
Mara baada ya kuwasilishwa kwa bajeti ya serikali bungeni mwaka wa fedha 2025/26 kumekuwa na maoni ya wadau mbalimbali kuhusu pendekezo la kutoza ushuru wa 10% kwenye mapato yaliyobaki (retained earnings) ambapo wataalamu wa masuala ya uchumi wanaonesha kuwa na wasisi dhidi ya pendekezo...
Kila zama na kitabu chake, na kondomu ilitengenezwa ili iweze kutumika mara moja tu na baada ya hapo kutupwa mbali kama uchafu hatarishi. Huenda hichi ndio kinaendelea vichwani mwa wabunge wa Covid 19.
Haijarishi watakuwa na hoja gani au watakimbilia chama gani, hakuna dalili yoyote kwa mbunge...
Ni jambo la aibu na fedheha kubwa kwa taifa kwamba kiwango cha parliamentary competence kimeporomoka kiasi cha kushangaza. Tunaona wabunge wetu wakibakia tu clapping hands na kugonga meza kama watoto waliokosa malezi, bila kuelewa kabisa the gravity of issues zinazowasilishwa mbele yao. Imagine...
Kipindi cha nyuma kumpata mgombea ubunge wa Jimbo kupitia CCM ilikuwa inahusisha wajumbe wachache, hii ilitoa mwanya Kwa wenye Hela, mawaziri na wabunge wazoefu kuhonga wajumbe.
Kanuni mpya za CCM wajumbe wa kupiga kura za kumpata mgombea wa ubunge wa CCM idadi Yao imeongezwa,unakuta jimbo Moja...
Wasalaam
Watanganyika tunapodai katiba mpya tunaebuisha hii aibu isiendelee kulikumba taifa. Angalau mtanganyika anaegombea ubunge awe na degree moja na sio sifa ya kujua kusoma na kuandika.
Hao ndo wabunge wetu wanaojadili bajati ya serikali 2025/2026, unategemea nn?
Ndo maana wengine...
Majiji makuu mengi hasa Africa huwa yana Wabunge moto sana na hii ni kwa sababu huwa ndio kitovu cha upinzani na pia ndio kumejaa Wasomi na watu waelewa wenye information zote.
Ila sasa njoo Dar ambako Jiji lina Wabunge Vilaza sana kuzidi hata huko mikoani, mtu kama Talimba eti ni Mbunge...
Ndani ya mbuga ya wanyama, kila mtu ana ombi la kumfanya aishi bila kujali mwenzake.
Hawa wabunge waliwahi kuomba wapigiwe saluti, ikashindikana. Karibuni kuna mbunge aliomba wenza wao pia wapewe hadhi ya VIP, ikapita kimya. Sasa kuna mwingine ameomba namba pekee za magari kwa wabunge.
Soma...
Wakuu,
Nakubaliana na hii hoja ya Oscar Oscar
Ni kweli kabisa kwamba mijadala ya Bunge letu mara nyingi huibua maswali kuhusu vipaumbele vya Waheshimiwa Wabunge. Lengo kuu la mbunge linapaswa kuwa kutimiza ahadi alizotoa kwa wapiga kura wake na kuwakilisha sauti zao, siyo kutafuta fursa za...
Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma, ameibua hoja bungeni akilalamikia mazingira yasiyo rafiki kwa viongozi na familia zao wanapopita katika maeneo mbalimbali ya VIP. Akizungumza bungeni, Musukuma amesema:
"Sisi humu ndani sio Wahuni ni Waheshimiwa tuna familia....Mhe. Spika sisi tumepewa...
Mbunge wa viti maalumu, Ester Bulaya ameibuka bungeni na kuuliza swali la kutaka kujua ni nini kilitokea hadi kuahirishwa kwa mechi ya dabi kati ya Simba na Yanga iliyotakiwa kuchezwa Machi 8, 2025 ambapo ameomba kupatiwa majibu.
Baada ya kuuliza swali hilo, Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.