09 Dec, 2019: Maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika. Wafungwa 5,533 wapata msamaha wa Rais. Mbowe ataka maridhiano ya Kitaifa

Slowslow fala sana atavaaje manguo ya chama kwenye dhifa ya kitaifa

Huyu jamaa naona yuko radhi hata jina la taifa lifutwe ili nchi iitwe ccm union republic
 
Tutambue kuna nchi hawana sherehe za Uhuru🙄🙄
 
Mbona kana kwamba wamekukanyaga hapo ulipo mpaka unakufuru. usitamke ovyo jina la Bwana kwa matakwa yako ya kisiasa. Mungu hayupo kwenye uroho wenu wa kisiasa mpaka nduguyo unamwona mchawi kisa yupo chama tofauti.
Bisha magufuli siyo mchawi bisha sungu sungu cyo magwiji
 


Rais John Magufuli ametangaza kusamehe wafungwa 5,533 na kuonya kuwa isiwe sababu ya watu kufanya makosa kwa kutegemea kusamehewa. Ametangaza msamaha huo leo jijini Mwanza wakati anahutubia Taifa kwenye sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara. “Sifurahi sana kuongoza nchi ya watu wengi wakililia magerezani.

Nitoe rai kwa Watanzania wenzangu mliopata msamaha huu kujutia makosa yenu mliyoyafanya na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa msamaha huu ambao kimsingi yeye ndie aliyewasamehe”amesema Rais Magufuli.

Amesema wafungwa watakaonufaishwa na msamaha huo ni wafungwa wote waliofungwa kati ya siku moja hadi mwaka mmoja, na wafungwa waliofungwa kwa miaka mingi na tayari wametumikia sehemu kubwa ya vifungo vyao na kubakiza muda usiozidi mwaka mmoja.

“Najua ni idadi kubwa na watu watashangaa lakini nimeguswa kwa moyo wangu ninasamehe wafungwa 5, 533”amesema Rais Magufuli na kubainisha kuwa Mkoa wa Kagera unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wafungwa wanaosamehewa. Amesema, kwenye mkoa huo amesamehe wafungwa 713, Dodoma wanasamehewa 385, Morogoro 365, Dar es Salaam 293, Mara 260, Mbeya 259, Kigoma 252, Tanga 245, Geita 230, Rukwa 214, Arusha 208, na Manyara 207.

“Hii ni mara ya kwanza kwa msamaha mkubwa namna hii kutokea na huenda usitokee tena kwa sababu miaka haifanani na kila mwaka una maajabu yake”amesema. Katika Mkoa wa Tabora Rais Magufuli amesamehe wafungwa 2017, Mwanza 190, Ruvuma 181, Singida 139, Simiyu 136, Lindi 129, Pwani 128, Iringa 110, Songwe 96, Katavi 74, Shinyanga 74, na Njombe wanasamehewa wafungwa 70.

“Na ni matumaini yangu hawa wafungwa 5, 533 wataanza kuondoka kuanzia kesho, na wasiwacheleweshe na kuwawekea mizengwe, na orodha ya majina yao ninayo hapa”amesema Rais Magufuli na kuongeza kuwa bila shaka misamaha waliopata wafungwa na mahabusu itasaidia kupunguza mlundikano wa wafungwa na mahabusu magerezani.
 

Katika watu walionisikitisha leo ni yule anayeitwa Shibuda kwa kuzungumza Kisukuma mwanzo mwisho pale alipotakiwa kufanya hivyo...Yaani huyo Shibuda ni shida kabisa alidhani wote waliohudhuria pale Kirumba ni Wasukuma...ameleta ukabila uliofutwa miaka ya mwanzoni mwa 1960...Baba wa Taifa mwalimu Nyerere hakukosea pale mwaka 1967 alipofanya Kiswahili kuwa lugha ya taifa...
 
Kwa hatua ya Leo Mbowe AME improve mbele strategically..

kama ilivyokuwa kwa Raila Odinga na hasimu aliyegeuka Rafiki Uhuru Kenyatta

good move KUB
 
Magufuli ni Mtu wa kusamehe
Eti nini ?!! Ni pesa hiyo kuwalisha na kuwatunza wafungwa hana, ameokoa pesa hapo, Ndiyo Uchumi wa awamu ya tano..
Pia anataka kujisafisha Kimataifa tu.. Hana huruma kihiiiivyo.
 
Rejea zako tu Kichwa cha Habari hapo juu, halafu anza tu Kutiririka na Kuserereka kwa Kutupa hasa Madini yako uliyonayo.
 
Ndomana nikasema mikutano ambayo ni ya wazi(sio ya kuzungumzia Siri za chama/kamati kuu ya chama.
 
MATHAYO 27:15-17, 20-30 MARKO 15:6-19LUKA 23:18-25 YOHANA 18:39–19:5
  • PILATO AJARIBU KUMWEKA YESU HURU
  • WAYAHUDI WAOMBA BARABA AACHILIWE
  • YESU ADHIHAKIWA NA KUTESWA
Pilato aliuambia hivi umati unaotaka Yesu auawe: “Sikupata msingi wa mashtaka yenu dhidi yake. Kwa kweli, hata Herode hakupata.” (Luka 23:14, 15) Sasa ili kujaribu kumlinda Yesu, Pilato anatumia njia nyingine, anawaambia hivi watu: “Mna desturi kwamba niwafungulie mtu siku ya Pasaka. Basi, mnataka niwafungulie Mfalme wa Wayahudi?”—Yohana 18:39.

Pilato ana habari kuhusu mfungwa anayeitwa Baraba, anayejulikana kuwa mwizi, mchochezi, na muuaji. Basi Pilato anauliza: “Mnataka niwafungulie nani, Baraba au Yesu anayeitwa Kristo?” Wakichochewa na wakuu wa makuhani, watu wanaomba Baraba afunguliwe bali si Yesu. Pilato anauliza tena: “Mnataka niwafungulie nani kati ya hawa wawili?” Umati unapaza sauti: “Baraba”!—Mathayo 27:17, 21.

Akiwa amefadhaika, Pilato anauliza: “Basi, nifanye nini na Yesu anayeitwa Kristo?” Watu wanasema kwa sauti kubwa: “Atundikwe mtini!” (Mathayo 27:22) Bila aibu, wanataka mtu asiye na hatia auawe. Pilato anawauliza: “Kwa nini? Amefanya kosa gani? Mimi sikuona jambo lolote linalofanya astahili kifo; kwa hiyo nitamwadhibu kisha nimfungue.”—Luka 23:22.
 
Huwiiii. Panya road wamerudi tena. Siasa na usalama.
 
Leo makomandoo wa jeshi walionyesha jinsi mtu maarufu akitekwa jinsi anavyoweza kuokolewa kirahisi sana, tena akiwa ametekwa na magaidi.

Sasa wanasahau bado tuna kumbukumbu za kutekwa kwa mtu maarufu na hao makomandoo walikuwepo kiliwashinda nini kumuokoa mtu mashuhuri au maarufu kama walivyomuita huyo mtekwaji?

Jambo la ajabu ni kuwa wanaonyesha uwezo wa kupambana na vitu ambavyo havipo ni nadharia tu nikama elimu yetu ilivyo ya nadharia kumbe na wanajeshi wetu wanapenda nadharia.

Kama si hivyo basi serikali ilihusika kumteka Mo sababu kama kuokoa mtu maarufu ni rahisi vile kwa Mo kiliwashinda nini?

Au makomandoo walisafiri? Ni jambo la ajabu sana Rais kufurahia maigizo kutoka kwa makomandoo, ni bora na wakina Wema Sepetu wangeigiza.

Naita maigizo rahisi kwakuwa hayana uhalisia na hali ilivyo. Ni sawa na mtu amuigizie shetani wakati hajawahi kumuona.

Hii nchi bado ni changa kwenye kila kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…